Bashiru Ally: Heshima ya nchi yetu imeshuka, tunadhalilika kwa njaa

Bashiru Ally: Heshima ya nchi yetu imeshuka, tunadhalilika kwa njaa

Bashiru ni dhahabu ya taifa shida mizengwe ya watu wale kutoboa ni ngumu! lile kundi linawaza kesho nani awe waziri, kesho nani awe mkurugenzi kesho nan awe Dc kesho nani awe RC , kesho nan apewe Uraisi, mijitu ya namna hii haiwezi kuwa na ubunifu mda wote yanawaza nani anataka kuwatoa kwenye ulaji na kuwapinga, ubunifu ni zero , tamaa ya madaraka ndiyo imo kichwani.[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji1787][emoji1787][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]View attachment 2502027
Nailiza tu. Hivi Kabudi bado yumo Bungeni?
 
Changamoto yake ni moja tu, hivi sasa akubaliki na wahafidhina ndani ya chama, kosa lake linaoneka linatokana na zoezi alilolisimamia kwa uadilifu mkubwa wa kuhakiki mali za chama tawala. Ukweli wake umemponza, uongo na unafiki wake ungalimuokoa.

Alishiriki moja kwa moja kwenye siasa za kishenzi za dhalimu. Ni mnafiki fulani anayekwenda na upepo.
 
lakini alihusika kuharibu uchaguzi 2020 period.
Niongezee hapa, hata kama sikumsikia mwenyewe akiyasema: kwamba, chama kinachotawala kikiwa na dola hakipashwi kupoteza uchaguzi!

Kama ni kweli aliwahi kuyasema maneno kama haya..., hata sielewi nimmchukulie vipi!

Lakini, kwa haya niliyomsikia leo Bungeni, akiyasema, heshima natoa.
 
Changamoto yake ni moja tu, hivi sasa akubaliki na wahafidhina ndani ya chama, kosa lake linaoneka linatokana na zoezi alilolisimamia kwa uadilifu mkubwa wa kuhakiki mali za chama tawala. Ukweli wake umemponza, uongo na unafiki wake ungalimuokoa.
Umeniongezea sababu nyingine ya kumheshimu huyu mtu: Kama ni kweli alisimamia kwa uaminifu kazi ya kuhakiki mali za chama, na zaidi ya yote "akawa mkweli"
Watu wa aina hii ni nadra sana kuwapata katika taifa letu leo hii.
 
Alikuwa Engineer wa wizi mkubwa wa kura kuwahi kutokea katika historia ya Tanzania, ana point lakini hakuna mtu na akili timamu akaamini mtu kama huyu, na akili zake za kikomunisti kufikiria sekta binafsi haiwezi kufanya kazi nzuri kwenye maji au nishati naona anazingua tuu, ajifunze na aheshimu sekta binafsi, akumbuke division one nyingi zimetoka sekta binafsi na za serikali zimejaza mafuriko ya division zero
Usitulazimishe kuamini kitu ambacho atukiona ila njaa na bei ya Michele tunaiyona,Dr badhiru ni sawa manyumbu wote
 
Yaani huyu mkundugu Bashiru kaona kupanda bei mwaka huu hajakaa akatathmin miaka yote ambayo nchi hukumbwa na ukame inakuaga vp hawa viongozi wajitahidi kupambana mafuta yashuke kwanza kuhusu suala la vyakula hili litajilekebisha kutokana na mavuno sisuala la muda mrefu

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Kaongea fact kama mwananchi amebuni kupiga pasi ndefu ya mlo, je serikali inashindwa vipi kubuni na kutafutia tatizo la upandaji wa bei bidhaa muhimu?
Nilikuwa sijaelewa hoja ila kupitia andiko lako nimeelewa hoja ya bashiru. Kwamba kama mwananchi amebuni mbinu ya kukabiliana na hiyo hali iweje serikali ikose ubunifu kwenye hili.
 
Kuna jambo sijawahi kulielewa nchi hii na hili limekuwa linatokea mara kwa mara. Kama tuko kwenye kipindi ambacho watu hawana pesa, bidhaa si zinatakiwa zipungue bei na si kuongezea? Watu wakiwa hawana pesa, inamaanisha wanunuzi wa bidhaa wanapungua, na hilo linafanya wauzaji kupunguza bei.

Nini huwa kinatokea kinafanya hii kanuni ya uchumi isiwe inafanya kazi?
Kuna mahitaji ya lazima kama chakula hayakwepeki. Nguvu ya kununua itapungua kama wanavyofanya hao wanaounganisha milo ila mahitaji yataendelea kuwepo. Ndio maana wafanyabiashara wanatamba.

Kwenye hili mkulima hahusiki. Bashe anafanya siasa tu.
 
Kipindi huyu mwamba akiwa Katibu Mkuu wa CCM chini ya himaya ya Mwendazake, Lissu aliibua hoja ya njaa kali kwa Taifa - aisee wakamshukia kama mwewe kwamba anapotosha umma.

What goes around...
 
Huyu mtu ana asili na uzoefu katika masuala ya taaluma, lkn pia ni mtu aliyekopwa kwa ajili ya sababu za kiutendaji za kisiasa. "Analysis" yake inaaminika na pia yenye mantiki, kwa mazingira na muktadha wa kijamii na kiuchumi tunayoyapitia kama taifa.

Baniani mbaya, ila kiatu chake ni dawa. Huyu ni mtu mwenye uaminifu wa milengo ya siasa za kijamaa, ila ni mtu mwenye msimamo wa kile alichoaminishwa na kukiamini.
Yes,Mr bashiru,huyu ni mtu makini,mwaminifu,na ni mzalendo halisi,Ninampenda sana huyu mtu kwa hoja na mawazo yake,utendaji wake kwa mda mfupi kwenye chama na serikali,amefanikiwa kujitengenezea maadui wengi sana,
 
Watawala waliweka pamba masikioni wakati wananchi wanapiga kelele kufungwa mipaka kwakuzuia kuuaza chakula nje ya nchi ...suala la chakula ni suala la National security....we rather be proactive than being reactive ,,hili tatizo tumelitengeneza wenyewe .....we must learn from the mistakes------
Kufunga mipaka ni kumnyonya mkulima
 
Bashiru amezunguuka wee, lakini nadhani mkakati anaokusudia Serikali ichukue ni kuzuia chakula kuuzwa nje, sio mwingine. Kwangu huu ni mkakati wa kipuuzi na haujawahi kuleta manufaa ya kweli toka huko nyuma. Suluhu ya kweli ni kuzalisha tu, no otherwise. Njaa imekuwepo nchi hii tangu wakati wa ukoloni na hata katika awamu za kwanza hadi ya 5 na mara zote hizo mkakati wa kuzuia mazao haukuwa na manufaa endelevu. Unafifisha uwekezaji na unaifanya sekta ya kilimo isiaminike kwa mtu kuweka mtaji wake.

Bashe na Samia nadhani ndo wana mkakati wa kweli wa kuondoa tatizo la njaa nchi yetu. Kuwaingiza vijana kwenye uzalishaji kwa kuwapa mafunzo, ardhi, mtaji, miundombinu na masoko ya bidhaa zao. Dkt Bashiru kuzungumzia tatizo la njaa bila kuchangia namna bora zaidi ya kuufanya mpango huu ufanikiwe ni kutukosea watanzania na kumkosea Rais wetu au ni unafiki kama unafiki mwingine tu.

Hakuna mikakati ya muda mfupi itakayoweza kuondoa njaa Tanzania zaidi ya kuongeza uwekezaji na kuzalisha chakula cha kutosha. Na bahati mbaya, Dkt Bashiru hasema kwenye mchango wake kama ni mikakati gani hiyo serikali ifanye zaidi ya huu unaofanywa sasa hivi wa "building better tomorrow", badala yake ameiuliza maswali Serikali badala ya kuishauri. Ingependeza mchango wake angeutoa Alhamis siku ya maswali kwa Waziri Mkuu.
 
Huyu mpuuzi alitakiwa sasa hivi awe jera alifuja mabilioni ya walipa kodi kwenda kununua wapinzani kwa kushirikiana na jiwe.
Hana cha kumfundisha bashe atutolee unafiki.
Umekula lakini maana mchawa mnashida sana
 
Nilikuwa sijaelewa hoja ila kupitia andiko lako nimeelewa hoja ya bashiru. Kwamba kama mwananchi amebuni mbinu ya kukabiliana na hiyo hali iweje serikali ikose ubunifu kwenye hili.
Samia hata kuumiza kichwa hajawahi ndo maana hata elimu yake ni ya kuungaunga
 
Mda si mrefu ataondolewa na kuchaguliwa kuwa balozi wa Zimbabwe ni swala la muda, ila jamaa jana aliuliza maswali mazuri.

Kiuhalisia sasa hivi wanaouza chakula ni walanguzi na si wakulima kwani karibia wakulima wote stock yao washamaliza kuuza na kubakisha chakula chao cha kula wao wenyewe.

So tuendelee kucheza ngoma za wafanyabiashara ukiwagusa kidogo utawasikia "vita ya Ukraine na Russia........mara kovid..........mara ukame.........".Ukija kwenye mafuta EWURA wakishusha bei vituo vinapewa mda wa kumaliza stock yao ya mafuta, ila wakipandisha tu siku hiyo hiyo mafuta yanaanza kuwa hadimu kupatika,ila ikifika saa sita ya iku mafuta yaanaza kupatikana kwa wingi.

2020 tulipitia ukame plus kovid ila bei haikupanda kama hii ya sasa kwani inapaa kwa speed ya rocket.
 
Kuna mahitaji ya lazima kama chakula hayakwepeki. Nguvu ya kununua itapungua kama wanavyofanya hao wanaounganisha milo ila mahitaji yataendelea kuwepo. Ndio maana wafanyabiashara wanatamba.

Kwenye hili mkulima hahusiki. Bashe anafanya siasa tu.
Ninaposema watu hupunguza matumizi ndiyo kama hivyo, unaweza kuwa kuunganisha milo. Effect yake ni ile ile, matumizi hupungua na kwa hivyo bei inatakiwa kushuka.

Bado nalitafakari hili jambo maana nimeliona sana likitokea.
 
Back
Top Bottom