DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally, amesema kuwa dhana ya maridhiano ya kweli haiwezi kujengwa juu ya makubaliano ya kisiasa pekee, bali lazima iyatokane na wananchi kama msingi wa mamlaka ya nchi.
Akizungumza katika mahojiano maalum na mtangazaji Chief Odemba wa kipindi cha Medani Kuu cha Star TV, Dkt. Bashiru amesema Katiba ya sasa inaweka mamlaka ya nchi mikononi mwa wananchi, hivyo lolote kuhusu maslahi ya taifa linapaswa kuanzia kwao na kuwanufaisha wao.
Dkt. Bashiru amesisitiza kuwa wazo lolote zuri, ikiwemo maridhiano ya kitaifa, halina maana bila kuwekwa katika mfumo unaowahusisha wananchi moja kwa moja na si kuwa kati ya pande za kisiasa tu.