Ila pasipo kushangalia ujio wa kishindo, na kwa namna ile ile ya awali, yaani ujio wa kivingine wa "ari mpya, nguvu mpya, na kasi mpya" slogan iliyoibuliwa na Prof. Mukandala huyu huyu.
Uongozi wa sasa unalazimika kuendeleza na kudumisha mazuri yaliyofanywa na mwendazake. Wananchi wa kada ya chini walimkubali, kumuhusudu na kumwamini.
Wakishindwa kufanya hivyo, utazaliwa upinzani ndani ya CCM, yaani CCM Mpya yenye kumuwakilisha na CCM Maslahi ya hawa wanamtandao na wafanyabiashara wanaokishikilia chama na serikali yake.
Hizi sauti zinazosikika kuhusu haja ya kuwaindoa wahuni waliopo ndani ya chama si za kubeza. Chama kikubwa na kikongwe husambaratika kupitia "its internal weaknesses" na wala siyo kwa kupitia "its external threats"