Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 13,075
- 11,682
Wanasiasa hawasaini hata mkataba. Hata hundi hawasaini. Hawawezi kumtia adabu mtumishi wa umma bila kupitia kwa accounting officer wake. Waziri hana mamlaka hata ya kumhamisha kituo mtumishi bila kupitia kwa Katibu Mkuu.Malipo yote ni lazima waidhinishe ma accounting officers.Mamlaka ya mwisho yapo kwa wanasiasa siku zote na sio hao wataalamu
Katibu Mkuu wa Wizara inayohusika anaweza kumkataza kiongozi kuweka namba pleti ya serikali katika gari lake binafsi. Katibu Mkuu anaweza kukataa kulipia hoteli au nyumba nyingine anayotumia kiongozi katika wizarq yake kama amejiridhisha kuwa kuna makazi mengine mazuri ya serikali. Waziri akileta ubishi anamshitaki kwa Katibu Mkuu Kiongozi ambae ndie mkuu wa civil service na mshauri Mkuu wa Rais katika mambo ya utawala.
Hawa ma accounting officers wana mamlaka makubwa sana. Wale ni watendaji na sio lazima wawe wataalamu.
Amandla...