Bashungwa Atoa Miezi Miwili kwa NIDA, Vitambulisho Milioni 1.2 Vilivyotengenezwa Kuwafikia Wananchi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ametoa miezi kwa miwili Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kuhakikisha vitambulisho milioni moja na laki mbili ambavyo tayari vimeshatengenezwa vinasambazwa na kuwafikia Wananchi walengwa.

Waziri Bashungwa amesema hayo leo Disemba 17, 2024 Jijini Dar es Salaam katika ziara ya kikazi ya kutembelea na kujionea utendaji wa Mamlaka hiyo.

"Niwajibu wenu (NIDA) kuhakikisha kadi hizi mnazifutilia na zinawafikia walengwa ndani ya miezi miwili kuanzia sasa, nitakapo rudi na kuomba taarifa ya kadi hizi zilizozalishwa nataka ziwe zimewafikia walengwa" amesema Bashungwa

Waziri Bashungwa ameiagiza NIDA kuhakikisha inatengeneza vitambulisho vipya bila gharama yoyote wala usumbufu kwa baadhi ya Watanzania ambao Vitambulisho vyao vilifutika maandishi kutoka na tatizo lililotokea katika Uzalishaji.

Aidha, Bashungwa ameitaka NIDA kuboresha utoaji wa huduma kwa Wananchi na kuondoka na tabia ya urasimu ambapo ameiagiza Menejimenti kuanza kuwachukuliwa hatua baadhi ya Watumishi wazembe ambao hawatoi huduma nzuri kwa Watanzania.

Bashungwa amewakumbusha watanzania kujenga utamaduni wa kujisajili kupata kitambulisho cha NIDA mara wanapotimiza miaka 18 na sio kusubiri mpaka kihitajike ili kuondokana na usumbufu ambao mara nyingi hujitokeza wakati wa Usajili wa Wanachuo na kipindi cha Vijana kujiunga na mafunzo mbalimbali.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uzalishaji wa Vitambulisho NIDA, Edson Guyai amesema Vitambulisho ambavyo havijawafikia walengwa ni kutoka na wanafunzi na watu ambao wamehama, na jithada zinazofanyika ni kukusanya vitambulisho vyote vilivyo kaa muda mrefu na kuanza kufuatilia wahusika kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili kuwatumia wananchi ujumbe wa sehemu watakapochua vitambulisho hivyo.

WhatsApp Image 2024-12-17 at 18.02.34.jpeg
WhatsApp Image 2024-12-17 at 18.02.38.jpeg
WhatsApp Image 2024-12-17 at 18.02.41.jpeg
WhatsApp Image 2024-12-17 at 18.02.43.jpeg
WhatsApp Image 2024-12-17 at 18.02.44.jpeg
WhatsApp Image 2024-12-17 at 18.02.46.jpeg
WhatsApp Image 2024-12-17 at 18.02.47.jpeg
WhatsApp Image 2024-12-17 at 18.02.48.jpeg
WhatsApp Image 2024-12-17 at 18.02.52.jpeg
WhatsApp Image 2024-12-17 at 18.02.56.jpeg

Pia soma ~ Uhamiaji Kibaha changamoto ni nyingi sana na hakuna hatua zinazochukuliwa
 
Vitambulisho feki,vina banduka maandishi,wajipange kutengeneza vitambulisho imara na vinavyodumu muda mrefu bila kuharibika kirahisi
 
Nina miaka 3 tokea nijisajiri na nida Ila nimeqmbulia namba ya nida tu kitamburisho sijapata
 
Kama ameuanza vizuri hivii.
ila mapema sana ngoja tuone
 
Taarifa zilizokosewa unafanya maombi inachukua hata mwaka na vielelezo vyote umepeleka unasubiri hadi mwaka na majibu akuna
 
Viongozi wa NIDA wakamatwe kwani ni wao ndiyo chanzo cha hii taasisi kuboronga. Haiwezekani mtu unaandikisha kupata kitambulisho na kila kila kitu umewapa wanakuambia usubiri miezi 6 kukipata na inafika hiyo miezi unaambiwa kitambulisho bado kutoka. Kikitoka sasa unakuta kina kasoro ama maandishi yanafutika ukikiweka kwenye pochi. Kamata hawa viongozi na kunyonga kabisa.
 
Hii NIDA ishanisumbua huu mwaka wa saba.....kubadilisha tu taarifa za imekuwa ngumu...issue nyingi sanaa nimekosa kutokana na kutokua na namba...nishatumia gharama sanaa Hadi imebibid nijikatie tu tamaa...mh wazir kama upo huku ebu tusaidie hapo makao makuu watuharakishie majibu kwa tuliotuma barua kubadili taarifa
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ametoa miezi kwa miwili Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kuhakikisha vitambulisho milioni moja na laki mbili ambavyo tayari vimeshatengenezwa vinasambazwa na kuwafikia Wananchi walengwa.

Waziri Bashungwa amesema hayo leo Disemba 17, 2024 Jijini Dar es Salaam katika ziara ya kikazi ya kutembelea na kujionea utendaji wa Mamlaka hiyo.

"Niwajibu wenu (NIDA) kuhakikisha kadi hizi mnazifutilia na zinawafikia walengwa ndani ya miezi miwili kuanzia sasa, nitakapo rudi na kuomba taarifa ya kadi hizi zilizozalishwa nataka ziwe zimewafikia walengwa" amesema Bashungwa

Waziri Bashungwa ameiagiza NIDA kuhakikisha inatengeneza vitambulisho vipya bila gharama yoyote wala usumbufu kwa baadhi ya Watanzania ambao Vitambulisho vyao vilifutika maandishi kutoka na tatizo lililotokea katika Uzalishaji.

Aidha, Bashungwa ameitaka NIDA kuboresha utoaji wa huduma kwa Wananchi na kuondoka na tabia ya urasimu ambapo ameiagiza Menejimenti kuanza kuwachukuliwa hatua baadhi ya Watumishi wazembe ambao hawatoi huduma nzuri kwa Watanzania.

Bashungwa amewakumbusha watanzania kujenga utamaduni wa kujisajili kupata kitambulisho cha NIDA mara wanapotimiza miaka 18 na sio kusubiri mpaka kihitajike ili kuondokana na usumbufu ambao mara nyingi hujitokeza wakati wa Usajili wa Wanachuo na kipindi cha Vijana kujiunga na mafunzo mbalimbali.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uzalishaji wa Vitambulisho NIDA, Edson Guyai amesema Vitambulisho ambavyo havijawafikia walengwa ni kutoka na wanafunzi na watu ambao wamehama, na jithada zinazofanyika ni kukusanya vitambulisho vyote vilivyo kaa muda mrefu na kuanza kufuatilia wahusika kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili kuwatumia wananchi ujumbe wa sehemu watakapochua vitambulisho hivyo.

View attachment 3178928View attachment 3178929View attachment 3178930View attachment 3178931View attachment 3178932View attachment 3178933View attachment 3178934View attachment 3178935View attachment 3178936View attachment 3178937View attachment 3178938
Vitambulisho vimetengenezwa "low standard " material zinachubuka haraka.
10%.
 
Nida wajinga mnooo zero brain kabisa.watu wanakosa deals sababu ya kukosa nida jinga kabisa
 
Hao nao kilasiku wanapewatu muda. Matapelitu wa kazi hao
Watu wamejaa mtaani hawana kazi halafu wao wanachezea kazi na mishahara wanapewa
 
Hii NIDA ishanisumbua huu mwaka wa saba.....kubadilisha tu taarifa za imekuwa ngumu...issue nyingi sanaa nimekosa kutokana na kutokua na namba...nishatumia gharama sanaa Hadi imebibid nijikatie tu tamaa...mh wazir kama upo huku ebu tusaidie hapo makao makuu watuharakishie majibu kwa tuliotuma barua kubadili taarifa
Serikali inachangia huu urasimu
 
Mimi nilisumbuka sana kwenye office za NIDA .., nilienda office kama tatu hiv kila office nakataliwa ...., lakini nikaenda ofisi ya NIDA Ilala, nilibadilisha/Rekebisha jina bila shida yoyote coz documents zote nilikuwa nazo ..., Mwenyezi mungu awape maisha mazuri wafanyakaz NIDA Ilala......
 
Back
Top Bottom