Bashungwa Atoa Miezi Miwili kwa NIDA, Vitambulisho Milioni 1.2 Vilivyotengenezwa Kuwafikia Wananchi

Bashungwa Atoa Miezi Miwili kwa NIDA, Vitambulisho Milioni 1.2 Vilivyotengenezwa Kuwafikia Wananchi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ametoa miezi kwa miwili Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kuhakikisha vitambulisho milioni moja na laki mbili ambavyo tayari vimeshatengenezwa vinasambazwa na kuwafikia Wananchi walengwa.

Waziri Bashungwa amesema hayo leo Disemba 17, 2024 Jijini Dar es Salaam katika ziara ya kikazi ya kutembelea na kujionea utendaji wa Mamlaka hiyo.

"Niwajibu wenu (NIDA) kuhakikisha kadi hizi mnazifutilia na zinawafikia walengwa ndani ya miezi miwili kuanzia sasa, nitakapo rudi na kuomba taarifa ya kadi hizi zilizozalishwa nataka ziwe zimewafikia walengwa" amesema Bashungwa

Waziri Bashungwa ameiagiza NIDA kuhakikisha inatengeneza vitambulisho vipya bila gharama yoyote wala usumbufu kwa baadhi ya Watanzania ambao Vitambulisho vyao vilifutika maandishi kutoka na tatizo lililotokea katika Uzalishaji.

Aidha, Bashungwa ameitaka NIDA kuboresha utoaji wa huduma kwa Wananchi na kuondoka na tabia ya urasimu ambapo ameiagiza Menejimenti kuanza kuwachukuliwa hatua baadhi ya Watumishi wazembe ambao hawatoi huduma nzuri kwa Watanzania.

Bashungwa amewakumbusha watanzania kujenga utamaduni wa kujisajili kupata kitambulisho cha NIDA mara wanapotimiza miaka 18 na sio kusubiri mpaka kihitajike ili kuondokana na usumbufu ambao mara nyingi hujitokeza wakati wa Usajili wa Wanachuo na kipindi cha Vijana kujiunga na mafunzo mbalimbali.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uzalishaji wa Vitambulisho NIDA, Edson Guyai amesema Vitambulisho ambavyo havijawafikia walengwa ni kutoka na wanafunzi na watu ambao wamehama, na jithada zinazofanyika ni kukusanya vitambulisho vyote vilivyo kaa muda mrefu na kuanza kufuatilia wahusika kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili kuwatumia wananchi ujumbe wa sehemu watakapochua vitambulisho hivyo.

View attachment 3178928View attachment 3178929View attachment 3178930View attachment 3178931View attachment 3178932View attachment 3178933View attachment 3178934View attachment 3178935View attachment 3178936View attachment 3178937View attachment 3178938
Hivi hao nida wana shida gani kutoa vitambulisho inakuwa shida hivyo?
 
Angewafukuza wote hapo na kuweka wapya.
Watu tunakosa baadhi ya michongo ya maana, kisa kitambulisho
Namba hawataki.

Bashungwa timua hao wapumbavu na wazembe.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, ameipa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) miezi miwili kuhakikisha vitambulisho milioni 1.2 vilivyotengenezwa vinawafikia walengwa.

"Nitakapo rudi na kuomba taarifa ya kadi hizi zilizozalishwa nataka ziwe zimewafikia walengwa," amesema Bashungwa.

Pia, ameagiza NIDA kutengeneza vitambulisho vipya bila gharama kwa wale waliopata matatizo ya maandishi kufutika maandishi kutoka na tatizo lililotokea katika Uzalishaji. Aidha, ameonya dhidi ya urasimu na kuagiza hatua zichukuliwe kwa watumishi wazembe wasiohudumia wananchi ipasavyo.
IMG_1754.jpeg
 
Back
Top Bottom