Bashungwa Atoa Miezi Miwili kwa NIDA, Vitambulisho Milioni 1.2 Vilivyotengenezwa Kuwafikia Wananchi

Hivi hao nida wana shida gani kutoa vitambulisho inakuwa shida hivyo?
 
Angewafukuza wote hapo na kuweka wapya.
Watu tunakosa baadhi ya michongo ya maana, kisa kitambulisho
Namba hawataki.

Bashungwa timua hao wapumbavu na wazembe.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, ameipa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) miezi miwili kuhakikisha vitambulisho milioni 1.2 vilivyotengenezwa vinawafikia walengwa.

"Nitakapo rudi na kuomba taarifa ya kadi hizi zilizozalishwa nataka ziwe zimewafikia walengwa," amesema Bashungwa.

Pia, ameagiza NIDA kutengeneza vitambulisho vipya bila gharama kwa wale waliopata matatizo ya maandishi kufutika maandishi kutoka na tatizo lililotokea katika Uzalishaji. Aidha, ameonya dhidi ya urasimu na kuagiza hatua zichukuliwe kwa watumishi wazembe wasiohudumia wananchi ipasavyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…