Basi kampuni ya Newforce limepata ajali Kitonga

Basi kampuni ya Newforce limepata ajali Kitonga

Kampuni iyo ambayo imemaliza mwezi uliopita kwa mabasi yake 12 kupata ajali na kuua abiria wengi Mwezi huu wa 7 pia wameanza kwa kasi ya ajali

Leo hatimaye wamepata ajali nyingine kitonga na chanzo kikuu ni mwendokasi

Serikali wamegoma kuifungia hii kampuni
LEO HATIMAE WAMEPATA AJALI NYINGINE.

Mnapenda sana damu za watanzania wenzenu kumwagika.
 
Kampuni iyo ambayo imemaliza mwezi uliopita kwa mabasi yake 12 kupata ajali na kuua abiria wengi Mwezi huu wa 7 pia wameanza kwa kasi ya ajali

Leo hatimaye wamepata ajali nyingine kitonga na chanzo kikuu ni mwendokasi

Serikali wamegoma kuifungia hii kampuni
Duuhh Kitonga!! Hawajatumbukia kweli?
 
Hivi hiyo njia hakuna mabasi mengine zaidi ya hayo,kwanini wasafiri wasiyasusie tu na kupanda kampuni nyingine mpaka wajirekebishe?watu wanakufa,watu wanapata vilema lakini wanaendelea kusafiri nayo, kutakuwa na shida mahali si bure...
Hii tabia siyo kwa Mtanzania, labda watanzania wa kizazi kingine.
 
Huwa natamani iwepo adhabu kwa abiria wasiochukua hatua yoyote waonapo uzembe wa madereva.

Hata viboko tu siyo mbaya maana unakutana na bus mpaka unajiuliza limebeba watu wazima au wafu?

MwendoKasi hauhitaji elimu wala seat ya mbele kujua tofauti na overtaking
 
Huyo Nforce mbona anakula sana vichwa vya watu?
New Force katokea kwenye garage ya wachina pale Sayansi, amepiga pesa sana kwenye dili za bima huko ndio alipatia mtaji kianzio.. Mabasi yake yote yako fully insured (comprehensive) kwa hiyo hizo ajali kwake ni faida tupu shida ipo kwa abiria na kama ni njia ya kuachana na hii biashara tutarajie ajali zaidi, maana ajali 12 ndani ya mwezi mmoja sio kitu cha kawaida hata kidogo serikali ilipaswa iwe imeshachukua hatua kitambo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu watanzania tusipoacha USHAMBA HUU wa magari, ajali zitatuandama kila kukicha.
Mfano unakuta mtu anasema " hii gari inakimbia sana" huu ni USHAMBA kabisa, watu kama hawa wana zile akili za kushindana barabarani na hatimae kuhatarisha usalama wa wengine. (gari linamwongoza binadamu.)

Au hawa wanaosema wanabett,,, yaani mtu mbele ya gari lililo mbele yake haoni vizuri lakini anaamua kuovertake hivyohivyo,,, USHAMBA KUPITILIZA""
Na hii siyo mabasi pekee, hata magari madogo (Private) yapo mengi sana.

VIONGOZI wajitathimini namna wanavyotii sheria za barabarani. NAHISI wananchi wanaiga tabia za VIONGOZI wawapo barabarani.
STL na ndugu zake ni kama hawaoni kama barabara inatumiwa na magari mengine zaidi yao.

TUACHE USHAMBA ILI KUPUNGUZA AJALI BARABARANI.
 
Back
Top Bottom