Tetesi: Basi la Tabora One latekwa kwenye pori kati ya Itigi na Tabora usiku wa jana

Tetesi: Basi la Tabora One latekwa kwenye pori kati ya Itigi na Tabora usiku wa jana

Mabasi yalikatazwa kusafiri usiku

Dah..mkuu...mie nadhani polisi wangeacha kwanza kusumbuana na wakina tundu lissu...badala yake wakafanye operesheni nzito ya kuwanasa hawa majambazi. Itakuaje wananchi wanakosa uhuru wa kusafiri usiku kwenye nchi yao? Africa mashariki yote hii wenzetu wanasafiri...ni sisi tu hili wimbi la majambazi limetushinda mpaka tumezuia safari za usiku. Inasikitisha sana
 
aiseeh!!watu wa huko acheni roho mbaya lloohh!!
 
Hali hii inatisha sana jamaa wamekuja na njia mbadala wanakuwa na mawakala kabisa wa m-pesa,airtel money tigo pesa yaani hauna pa kukwepea.
 
NBS anajua eneo hilo ndo maana akitoka asubuhi saa kumi na mbili lazima abebe askari wawili wenye silaha wanashukia manyoni then mabus yanayotoka dsm yakifika manyoni wanawapitia askari tena

Ndo usalama wa mabas ya nbs
Jamaa wanajua biashara
 
Barabara zingine kupita ni kutaka majanga tu

Kama hiyo ni kweli mkuu basi tutangaze rasmi kwamba hatuna jeshi la polisi. Yani wanalipwa na kodi zetu..wananunuliwa vifaa...halafu badala ya kwenda kudhibiti haya majambazi badala yake wanafukuzana na vyama vya siasa? This is wrong. Inasikitisha sana nchi huru halafu eti tuwe na barabara ambazo ukipitia "unajitakia majanga"...tuzuiwe uhuru wa kusafiri usiku...tulazimishwe kulipia escort za polisi tukisafiri maeneo flani. Very unfortunate!
 
Siku hiz nikiendaga Tabora napanda za Kahama nishuke Igunga nalala asubuh naamsha Tabora town kuna NBS za Tabora Town to Igunga pale Igunga unapata Kuku wa Kienyeji saafi
Hahah...mkuu, ulimaanisha kuku ndege or kuku binadam..!!
 
Issue ya kuteka magari ya abiria ni issue ndogo sana. Mabasi yote yafungwe GPS na police ndiyo wawe wanaziratibu na ikitokea usiku wakaona gari imesimama basi wapigie simu dereva au conductor. Na kukiwa na shaka basi polisi walio karibu na bus wahakikishe wanalifuatilia. Simple as that. Mabasi yakiwa tracked kwa gps yatakuwa salama sana hata ku overspeed watakuwa hawana tena.
 
Pole sana waliotekwa.....ni vitendo tulivyovisahau vinarudi tena,yote inatokana na kukusa pesa sababu ya mfumo uliopo mzunguko wa pesa hakuna....
 
Issue ya kuteka magari ya abiria ni issue ndogo sana. Mabasi yote yafungwe GPS na police ndiyo wawe wanaziratibu na ikitokea usiku wakaona gari imesimama basi wapigie simu dereva au conductor. Na kukiwa na shaka basi polisi walio karibu na bus wahakikishe wanalifuatilia. Simple as that. Mabasi yakiwa tracked kwa gps yatakuwa salama sana hata ku overspeed watakuwa hawana tena.

Sasa mkuu nyangoboli, hivi dereva basi akisema atembee speed 80 ambayo ndo inaruhusiwa kisheria, Dar-Mwanza atafika saa ngapi?
 
Mkuu tatizo hiyo njia ni ya kipweke sana,afadhali wangekubali kupitia ile ya kupitia nzega maana ina magari mengi sana na haina mapori makubwa
Hili nalo ni neno mkuu wangu,
Nilikuwa napoteza muda ili taarifa zitiririke, lakini mmmmmh
 
Issue ya kuteka magari ya abiria ni issue ndogo sana. Mabasi yote yafungwe GPS na police ndiyo wawe wanaziratibu na ikitokea usiku wakaona gari imesimama basi wapigie simu dereva au conductor. Na kukiwa na shaka basi polisi walio karibu na bus wahakikishe wanalifuatilia. Simple as that. Mabasi yakiwa tracked kwa gps yatakuwa salama sana hata ku overspeed watakuwa hawana tena.
Mkuu kutoka Itigi mpaka Tabora ni kilomita mia mbili na kitu na hapo katikati hakuna kituo hata kama watatoa taarifa watafika saa ngapi
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Back
Top Bottom