Basi laacha njia na kugonga magari saba Moshi, watu 15 wajeruhiwa

Vip hapo mkuu itokea hivyo huwezi kutumia hand break?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee hii ajali ilitaka kunipotezea rafiki yangu + mwanae kama masikhara tu. Basi lao ndo lilikuwa linaingia stand kutokea Dar likakutana na hekaheka hiyo. Kuna hiace iliparamiwa ikaenda kujibamiza ubavuni mwa basi hilo. Ile nanyenyua simu kumpigia kama kafika salama kumbe ndo walikuwa kwenye hekaheka za kupiga mayowe.
 
Sawa kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vip hapo mkuu itokea hivyo huwezi kutumia hand break?

Sent using Jamii Forums mobile app
Inategemea na aina ya handbrake systeam iliyofungwa kwenye gari. Kwa magari yanayotumia handbrake system ambayo iko intergrated na main brake system, once one fail means all fail. System ya pili ya handbrake ni ile inayofungwa nyuma ya gearbox na iko designed kushika propelor shaft. Shida yake ni kwamba hutumia shoe ambazo ni ndogo sana ambazo zina uwezo wa kuzuia gari ambayo ni static, gari ikiwa kwenye motion hazina uwezo wa kuzuia.
 

Nina video ya cctv camera asee Dereva ni hodari ingekua anaroho nyepesi angepita na bajaji zote


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Dereva kajitahidi,ila angenyoosha kwenye huo mnara angefanya jambo jema zaidi maana ameenda kuvaa magari ya watu.Inaonekana gari ilishamkataa tangu mbali sana.

Kama angenyooka na mnara mzee ilikua ni vilio mda huu na ata yeye mwenyewe maana pale zilikuepo bajaji na waenda kwa miguu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nilipita eneo la tukio na kuikuta hiyo ajali bahati nzuri hawakuwepo watembea kwa miguu wangepata madhara makubwa sana, mwaka huu pia kulikua kuna video ya ajali nyingine ya bajaji ilikosa break ikaingia hadi keepleft ndani. Hivi Chato na Bukoba bado hawajaweka hizo camera(kidding)
 
Mkuu gari ilitokea round about ya Arusha hii njia inayotokea bomani na ile njia inamteremko mkali sana na inasemekana break zilikataa

$ There's clear light at the end of the Tannel $
 


Kwa hali hiyo haiwezi kudhibitiwa na kuepukwa iwapo gari kama ingekuwa inafanyiwa regular service?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi namuona kijana wa bodaboda mwenye kofia ya buluu kushoto nadhani anaenda kuchomoa betri.
 
Kwa maana hiyo mkuu ikitokea ku fail kwa break ni no way inabidi uchague mti wa kusimamia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa maana hiyo mkuu ikitokea ku fail kwa break ni no way inabidi uchague mti wa kusimamia?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mzee unajua kuendesha gari kweli?

Kugonga mti ni sawa na kifo cha kujitakia wewe mwenyewe. Mara elfu upinduke lakini sio kwenda kugonga mti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…