Basi laacha njia na kugonga magari saba Moshi, watu 15 wajeruhiwa

Basi laacha njia na kugonga magari saba Moshi, watu 15 wajeruhiwa

Watu 15 wamepelekwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi nchini Tanzania kwa ajili ya kupata matibabu, baada ya basi la kampuni ya Harambee kudaiwa kufeli Breki na kuparamia magari mengine saba katikati ya mji wa Moshi.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Salum Hamduni, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo jioni Jumanne Desemba 17, 2019 na kueleza imehusisha magari saba likiwamo basi la hilo la Harambee.

"Ni kweli kuna ajali imetokea jioni hii eneo la Benki ya NBC, iliyopo katikati ya mji wa Moshi na kwa sasa nipo Mawenzi hospitali, ambapo majeruhi wapo 15 na mmoja ndiye aliyeumia sana lakini wengine wamepara majeraha madogo ya kawaida na mishtuko na wanaendelea kupewa huduma ya kwanza," amesema Kamanda.


Kamanda Hamduni amesema chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika na kwamba uchunguzi unaendelea na atatoa taarifa rasmi pindi utakapokamilika.

"Ni mapema sana kuelezea chanzo cha ajali, kwa kuwa uchunguzi bado unaendelea, lakini pia sijapata taarifa ya idadi ya abiria waliokuwepo kwenye basi na magari mengine madogo yaliyohusika katika ajali hiyo" amesema.


Tukio hilo la kuogofya lilinaswa na camera za CCTV, zikionyesha namna basi hilo lilivyoshindwa kuzunguka katika mzunguko huo wa magari na kuparamia magari saba kabla ya kusimama.

View attachment 1295572
Huu ushahidi tosha kuwa siyo kufeli breki, bali ni uzembe wa aliyekuwa akiliendesha.
 
Gari ilifeli breki,hata abiria wenyewe wamesema dereva alitoa taarifa mapema kwamba breki zimekataa...
Abiria wamempongeza dereva kwa kujitahidi kuokoa maisha yao....
Ila alisahau kupiga honi mfululizo. Panick bwana. Hata hivyo kajitahidi. Mie ndhani alitakiwa ailenge ile round about. Basi ingegonga kiukuta na kupunguzwa spidi kama sio kusimama kabisa.
 
Ila alisahau kupiga honi mfululizo. Panick bwana. Hata hivyo kajitahidi. Mie ndhani alitakiwa ailenge ile round about. Basi ingegonga kiukuta na kupunguzwa spidi kama sio kusimama kabisa.
Pale kwenye round about kuna mtaro,gari ingepata shida zaidi.
 
Ni nini kinachosababisha break ku fail?

Ni uzembe wa mmiliki wa gari na dereva.

Kwanini hawapeleki magari service regularly Kama inavyotakiwa?

Kwanini hawakubadilisha break pads?

Ni uzembe na uzembe lazima wawajibishwe wote dereva na mmiliki wa gari!

Waache kucheza na maisha ya watu!

Na iwe mfano kwa wengine wajifunze


Sent using Jamii Forums mobile app
Acha ujuaji mwanzoni ulisema dereva achukuliwe hatua kwa kuwa na speed kubwa. Ulipoambiwa kuwa alitoa taarifa ya kufeli breki kwa abiria na wakati alikuwa kwenye mtereko ndo unakuja na hoja za kufanya service. Hueleweki

Sent from my PBCM30 using Tapatalk
 
Ndo hapo sasa usihukumu kabla ya kupata ukweli
Acha ujuaji mwanzoni ulisema dereva achukuliwe hatua kwa kuwa na speed kubwa. Ulipoambiwa kuwa alitoa taarifa ya kufeli breki kwa abiria na wakati alikuwa kwenye mtereko ndo unakuja na hoja za kufanya service. Hueleweki

Sent from my PBCM30 using Tapatalk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha ujuaji mwanzoni ulisema dereva achukuliwe hatua kwa kuwa na speed kubwa. Ulipoambiwa kuwa alitoa taarifa ya kufeli breki kwa abiria na wakati alikuwa kwenye mtereko ndo unakuja na hoja za kufanya service. Hueleweki

Sent from my PBCM30 using Tapatalk



Mjinga ni wewe unaepanic kwa kuchukulia mambo kama ni personal issues.

Kwani maana ya majadiliano na uchambuzi wa mada ni nini?!

Kwenye majadiliano au uchambuzi wa swala fulani mtu huchambua kwa kuangalia marefu na mapana ya swala zima na kisha ku conclude.

Mimi siyo mtu wa kariri mambo kama wewe.

Kama ungeelewa maana ya majadiliano na uchambuzi wa maswala wala usingekuja na huu upumbavu wako hapa.

Acha kupanic kwa maswala ambayo siyo personal.

Mtu kama wewe siyo rahisi kunielewa mimi sababu ya tofauti kubwa ya kiwango cha ufahamu kati yako na yangu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama unausafiri yani gari usiseme ivyo... Izo ni technical issues brother unatakiwa kujua gari inatumia umeme kwenye mfumo wa break kwaiyo inaweza kutokea tatizo hata kama gari ina service mkuu... Kikubwa ni dereva yupo vizuri kupambana.... Subiri uwe na gari afu ifeli break utakuja apa kutuadisia

Sent using Jamii Forums mobile app



Nazani tufike mahala tuwe tuna admit mapungufu yanayojitokeza.

Tusiwe watu wa kutafuta kujitetea kila wakati.

Hakuna kitu kinaweza tokea bila sababu.

Hata hizo hitilafu za ufundi zina sababu.

Mfano kupuuzia service za mara kwa mara kadri itakiwavyo, kununua vipuli fake kwa kutafuta unafuu n.k


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliona hiyo clip jana niliogopa sana. Nikawa nawaza kama kuna watu walikua wanatembea barabarani hawakosi kugongwa na kufa. Sema baadae millardayo akapost kua hakuna kifo.
Kwel binadamu kifo tunatembea nacho jamani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Madereva wazembe sana, huo mwendo si wa kuutumia mjini,labda tuseme gari likifeli break kwenye tambarare speed huwa inaongezeka.
Naona kuna haja ya kufilisi makampuni yanayotumia madereva wasiofuata sheria ili mwisho wa siku Hawa wamiliki wawape taratibu madereva wao.
 
Hizo ngoma zinafukuzagwa over speend hata katikati ya mji bila kujali alama za barabarani za 50kmph kutembelea mjini zinavyoelekeza.

Angelikuwa na mwendo wa 'kistaarab', kosa lolote la kiufundi lisingeweza kusababisha kuparamia magari yote hayo!

Halali yenu huyo dereva mvuta bhangi, mhangaike naye!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo Bus hata kukimbia sina uhakika lakini niijuavyo Harambee huenda likawa ndio bus kimeo kwa njia hiyo.
Na ndio maana hata safar zake huanza wakati bus zoote zishaondoka
 
Back
Top Bottom