Yimakatso
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 7,060
- 9,468
Hujafika Dar hata ukielezwa tu ni kupoteza muda. Yaani jiji linalochangia uchumi wa nchi kwa zaidi ya 12% ulinganishe na takataka zingine ambazo bado zinashughulika na imani za kishirikina za kukata mikono albino na kuwaua vikongwe wenye macho mekundu?Kwan Dar kuna nini cha ajabu??
Dar ndiyo Tanzania kila kitu kinachohusu nchi kipo Dar.
Bandari kuu inayolisha nchi zaidi ya 6,kitovu kikuu cha biashara,matajiri wote wakubwa wanaishi Dar,miundombinu ya kisasa kama mabasi ya mwendokasi na flyovers zinapatikana Dar pekee.
Uwanja wa ndege wa kimataifa ambao unaunganisha nchi yetu na mataifa mbalimbali ya ulimwengu,uwanja mkubwa wa mpira sio ccm kirumba kama wa manungu mtibwa.
Serikali imehamia Dodoma lakini viongozi wakuu kutwa hawabanduki Dar kwasababu ndo jiji kuu la nchi.
Idadi ya watu inazidi 6 milioni na kwa sensa ijayo mwakani matarajio ni watu zaidi ya milioni 9 ambayo inakimbiliana na majiji kama Cairo,Lagos ama London.
Wilaya zote za Dar zina hadhi ya manispaa tofauti na Mwanza manispaa zipo mbili tu Ilemela na Nyamagana.
Nimekufungua ubongo angalau mengine utajazia mwenyewe.