BAVICHA kufanya Julai 1, 2021 kuwa siku ya Katiba

BAVICHA kufanya Julai 1, 2021 kuwa siku ya Katiba

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Nimesikia kuwa kesho ndo siku ya katiba.

Sina hakika hasa ni akina nani ndo wameipanga ila nahisi ni akina mwafulani.

C881B568-B461-4F74-A3AB-0EE01B4EC65D.jpeg

Shughuli itafanyika hapo Segerea. Tundu Lissu atakuwa mtoa mada. Au labda mmoja wa watoa mada?

Ni jambo zuri. Katiba mpya ni kitu muhimu kwa mustakabali taifa.

It is long overdue. Way long overdue.

Baada ya Rais Magufuli kufariki, vuguvugu la katiba mpya limerudi tena.

Na sasa hivi ‘Twitter advocates’ wa hiyo katiba mpya wanasema liwe liwalo litalokuwa, katiba mpya lazima ipatikane.

Mikwara na maneno kama hayo kuhusu hiyo katiba mpya sikuyasikia sana kipindi cha utawala wa Rais Magufuli.

I wonder why 😂 🤔.

Nimefanya ka observation kangu kadogo kwa hizi siku za mwanzoni za utawala wa Rais Samia na nimegundua kwamba kuna ‘perception’ ya yeye kuwa mpole, mlaini, mdhaifu, msikivu, na vivumishi vingnine kama hivyo.

Perception hiyo ndo naona imewapa moyo wale Twitter activists kusema liwe liwalo litalokuwa, katiba mpya ni lazima ipatikane.

Juzi Rais kasema apewe muda kwanza aisimamishe nchi kiuchumi halafu ndo labda tutazungumzia na kuyaangalia hayo mambo ya katiba mpya, baadhi ya raia tumemshukia kama gunia la mawe.

Kuwa mpole na kuwa msikivu si vibaya. Ila kilicho kibaya ni watu kuwa na perception ya kwamba wewe ni dhaifu na kwamba huwezi kuwa kichwa ngumu na huwezi kustahimili mashinikizo.

Kila la kheri hiyo kesho kwa washiriki wote wa kongamano hilo la katiba mpya.

Ila sitosahau yale maandamano ya UKUTA na yale maandamano ya Instagram ya yule dada enzi Magufuli akiwa Rais 🤣.
 
Una uhakikia gani kama hawatatoka na kwenda kuunda UKAWA tena mara baada ya kulamba posho ya katiba??
 
Uzuri mmoja mama ni kama jk anawaachaa wafanye mikutano yao lakini masikio kayaweka mbalii wao wenyewe watachoka na watatulia
 
Dai la katiba ni la watu wajinga wasiojua wanataka nini!

Ukiwauliza wana bavicha na hao wanaharakati wajinga kwamba unataka katiba mpya ili iweje, hana cha kujibu zaidi anafikiri katiba mpya itaweka mazingira mepesi ya kuwezesha wao kuingia ikulu kirahisi!

Kenya wana katiba tunayoambiwa ni nzuri sana lakini ni nzuri kwa wanasiasa tu maana ufisadi na maisha magumu kwa raia viko pale pale!

Wapeleke uhuni wao huko! Wao waendelee kupambana na mondi tu.
 
Uzuri mmoja mama ni kama jk anawaachaa wafanye mikutano yao lakini masikio kayaweka mbalii wao wenyewe watachoka na watatulia
Hili nilisema toka mwanzo kwamba Samia awasikilizee weee, ila mwisho wa siku hadi inafika 2025 hakuna kitu watapata, na watashiriki uchaguzi watake wasitake[emoji23][emoji23][emoji23]

Tena akiwaita na kina Mbowe ikulu wakanywe juis ndio kabisa atakuwa kawamaliza
 
Magufuli alikuwa muuaji na katika mbinu hiyo ya kuua wengi walijiweka kando na badala yake walitumia mbinu ya kuomba msaada wa jumuiya ya kimataifa kusaidia katika mapambano hayo ikiwa ni pamoja na kuomba serikali ya Magufuli kuwekewa vikwazo vya kiuchumi.

Kwa sasa mbinu lazima ibadilike nayo ni ya mazungumzo na hii inatokana na Rais mwenyewe kukubali kufanya mazungumzo na vikundi mbalimbali. Sasa watu wanavuta subira akizingua watamzingua naye kitu ambacho hakitegemewi.
 
Katiba inapofanywa kuwa hitaji la kisiasa, ndio kosa linaanzia hapo
 
Back
Top Bottom