Uchaguzi 2020 BAWACHA amkeni, uwezo wa kumfanya Tundu Lissu awe Rais wa Tanzania uko mikononi mwenu kwa sasa

Uchaguzi 2020 BAWACHA amkeni, uwezo wa kumfanya Tundu Lissu awe Rais wa Tanzania uko mikononi mwenu kwa sasa

Hatari Wana JF,

Baada ya takribani siku kumi za amshaamsha ya mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema ndugu Tundu Lissu kuigongesha CCM na mgombea wake kwenye majukukwa ya kampeni, ni dhahiri kuwa Magufuli na CCM yake waweza kuwa chama cha upinzani kwa Mara ya Kwanza katika historia ya taifa hili, 'assuming' Tume ya uchaguzi ni huru.

Mwitikio wa sera anazonadi ndugu Tundu Lissu na Chama chake miongoni mwa wananchi ni mkubwa sana na mijadala ya uwezo na maono yake makubwa kwa taifa la Tanzania vinazidi kushika Kasi.

Pamoja na ukweli kuwa ndugu Tundu Lissu anamhenyesha vilivyo Magufuli na CCM yake kwenye kampeni za majukwaani, lakini Kuna kundi hili kubwa la kina mama katika rika zao zote zile zenye umri wa kupiga kura.

Akinamama wa nchi hii mimi binafsi sijui saikolojia yao ikoje. Ila mara nyingi wakati wa kampeni hujazwa hofu na CCM kuwa iwapo watachagua vyama upinzani, basi vita itatokea na wao wataachwa wakiteseka na watoto.

Hofu hii hukipatia CCM kura nyingi kutoka kundi hili ambalo likiwekwa sawa likajiamini, Tanzania ya Tundu Lissu tunaweza kuiona.

Kwa maana hiyo ni rai yangu kwa Baraza la Wanawake wa Chadema liamuake sasa, sumu ya hofu imeshaanza kusambazwa kwa Kasi kubwa.

Ndiyo maana kukawa na BAWACHA, mambo yenu akinamama mnayajuwa wenyewe, msaidieni Tundu Lissu sasa mapema iwezekanvyo, msisubiri dakika za majeruhi, jeshi kubwa muanze sasa.

Heri mimi sijasema.
Jumamosi nilienda saloon fulani.. Bahati ilihoje nikakuta wamama kabisa wanaongea hawampi Kura Magufuli..wanampenda Lissu ..nilizizima kwa Raha..wamama wengi wamejitambua ..biashara kibao zimefungwa wasiamke mchezo!
Bawacha tupo nyuma ya Lissu ..
 
CHADEMA wanapaswa kuwa na mbinu nyingi ili kuweza kushinda uchaguzi.
Binafsi sijaona umuhimu wowote wa viongozi wote wa kitaifa kuambatana na mgombea uraisi.

Cha muhimu chama kilipaswa kuunda team mbalimbali kwa kuspot vichwa vizuri katika kushambulia jukwaa wapeleke mashambulizi pande zote za nchi.
Ni mambo ya ajabu sana kutegemea mbinu moja tu kupata ushindi.

Excuse isiwe eti uhaba wa fedha kwa nn hamkujipanga mapema zaidi before uchaguzi? kwa maoni yangu n bora mngeweka wagombea katika baadhi ya maeneo yanayoonekana watu wana mwamko wa mageuzi hii ingesaidia kuokoa fedha na kupanga safu nzuri kwa ajili ya kampeni ya kufa na kupona.

Mwisho watumieni vizuri watu wanaoupenda upinzani kwa dhati mfano watu km akina Malisa G kuliko kuwakumbatia waganga njaa ambao hawachelewi kuunga mkono juhudi.
Nimekuelewa Sana mkuu...tuwatumie vizuri hao kina Malisa
 
Mleta Uzi anawakumbusha wajibu wenu Kupambana katika kipindi hiki cha uchaguzi, ni Uzi mzuri though.

Let's meet at the top, cheers 🍻
Nimeuelewa Sana mkuu..tuko alive mkuu...Sisi tunasubiri tu mwaka huu undava undava tu
Bdw uliadimika sana mkuu..Bata la wapi Hilo?
 
Jumamosi nilienda saloon fulani.. Bahati ilihoje nikakuta wamama kabisa wanaongea hawampi Kura Magufuli..wanampenda Lissu ..nilizizima kwa Raha..wamama wengi wamejitambua ..biashara kibao zimefungwa wasiamke mchezo!
Bawacha tupo nyuma ya Lissu ..

😅😅 I guess ulim-double pay hadi muhudumu wa saloon hapo ulivyofurahi 😂

Let's meet at the top, cheers 🍻
 
Haya sasa @Bawacha mnaangushiwa jumba bovu,makamanda wameshindwa wanawatupia mpira nyinyi kikundi cha wakina mama wa kichaga.
 
BAWACHA NI KIKUNDI CHA MACHECK BABIES WA MJINI, HAWATAKUBALI KUFANYA KAZI KAMA ANAZOFANYA MAMA KABAKA KULE CCM, BWAWACHA KUFIKA VIJININI KWAO NI NDOTO WAKO MJINI TU, BAHATI MBAYA MIJINI HAKUNA WAPIGA KURA WANAOJITAMBUA, WENGI WANAHUDHURIA MIKUTANO NA KURA HAWAPIGI. TUNDU LISSU KUSHINDA SIYO RAHISI JAPO ANGEPENDA KUWA IKULU BY NOVEMBER
Waambie, kule kijijini hawamjui kabisa huyo mgombea. Wachahe sana wamewahi kusikia hilo jina na wanajua ni mbunge mstaafu wa singida
 
Jumamosi nilienda saloon fulani.. Bahati ilihoje nikakuta wamama kabisa wanaongea hawampi Kura Magufuli..wanampenda Lissu ..nilizizima kwa Raha..wamama wengi wamejitambua ..biashara kibao zimefungwa wasiamke mchezo!
Bawacha tupo nyuma ya Lissu ..
Vizuri, lakini Kuna vilinge vingi vya kina mama zaidi ya saloon, mfano masoko na maeneo mengine mnayoyafamu nyie wamama! Makanisa pia yana akina mama wengi na yanatumika sana chini kwa chini kueneza propaganda za hofu! Pigeni kazi msilale!
 
Ni kweli mkuu hapa inahitajika propaganda ya maana
 
Mkuu CCM ina wanachama wengi vijijini.

Ambako CHADEMA ili kuitaji wanachama wengi zaidi wanatumia lugha zenye mlango wa matusi na dharau kitu ambacho wamama na wazee wanabaki kushika vichwa.

Lakini kwa jambo hilohilo ambalo MJINI SI MATUSI NI SEHEMU YA SIASA.

Kwa sasa upinzani hauhitaji dola na kamwe LISU hawezi kuwa Raisi hata vyama vyote vikiungana.

ILA!
Kumuondoa NDULICCM inahitaji nguvu ambazo hazina tamaa ya RUZUKU NDANI YAKE. (UMOJA)

Mambo ya bashiri hayo buku 7 mpya. Kasi mpya. Tutawaona wengi.
 
Nimesema wachache. Kamwe Tundu Lissu hawi Raisi wa Nchi hii.
Abaki tuu kutazama picha zimepigwaje.
Ni Imani yako, hakuna ubaya, na kwa kuwa akili yako faida ya kuwa rais ni kupiga picha nimekuelewa!
 
Hatari Wana JF,

Baada ya takribani siku kumi za amshaamsha ya mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema ndugu Tundu Lissu kuigongesha CCM na mgombea wake kwenye majukukwa ya kampeni, ni dhahiri kuwa Magufuli na CCM yake waweza kuwa chama cha upinzani kwa Mara ya Kwanza katika historia ya taifa hili, 'assuming' Tume ya uchaguzi ni huru.

Mwitikio wa sera anazonadi ndugu Tundu Lissu na Chama chake miongoni mwa wananchi ni mkubwa sana na mijadala ya uwezo na maono yake makubwa kwa taifa la Tanzania vinazidi kushika Kasi.

Pamoja na ukweli kuwa ndugu Tundu Lissu anamhenyesha vilivyo Magufuli na CCM yake kwenye kampeni za majukwaani, lakini Kuna kundi hili kubwa la kina mama katika rika zao zote zile zenye umri wa kupiga kura.

Akinamama wa nchi hii mimi binafsi sijui saikolojia yao ikoje. Ila mara nyingi wakati wa kampeni hujazwa hofu na CCM kuwa iwapo watachagua vyama upinzani, basi vita itatokea na wao wataachwa wakiteseka na watoto.

Hofu hii hukipatia CCM kura nyingi kutoka kundi hili ambalo likiwekwa sawa likajiamini, Tanzania ya Tundu Lissu tunaweza kuiona.

Kwa maana hiyo ni rai yangu kwa Baraza la Wanawake wa Chadema liamuake sasa, sumu ya hofu imeshaanza kusambazwa kwa Kasi kubwa.

Ndiyo maana kukawa na BAWACHA, mambo yenu akinamama mnayajuwa wenyewe, msaidieni Tundu Lissu sasa mapema iwezekanvyo, msisubiri dakika za majeruhi, jeshi kubwa muanze sasa.

Heri mimi sijasema.

..uko sahihi kabisa.

..nadhani CDM walijitahidi kabla ya kampeni kuiimarisha Bawacha.

..Na hata katika mkutano mkuu wa CDM Mh.Mdee alisema kwamba Bawacha wako tayari kwa kampeni.

..Nadhani huu ni wakati wa kuyaweka maneno yao ktk vitendo-- putting words into actions.

..CDM lazima wa-test mitambo yao waliyoi-set ktk Bawacha.
 
BAVICHA nao sijui kwa nini wako kimya mitandaoni nana kama wanaidiwa na kundi la ccm
 
Back
Top Bottom