BAWACHA: Rais Samia asiwatambue Wabunge 19 wa Viti Maalum waliofukuzwa uanachama CHADEMA

Hili la wabunge feki wa Chadema, Uongozi wa juuuu kabisa wa Chadema, wanataa isiyoonekana na wanachama wengine
Isionekane nini boss.Ebu ongeza nyama tafadhali
 
Mimi tangu niamue kutokuwa na chama nina uhuru kupindukia.

Juzi tu hapa CHADEMA wametoka kumpigia kampeni pensioner HOSEA mzee wa TAKUKURU kuwa rais wa TLS kwasababu wana maslahi naye.

Usipojitambua dunia hii UTATUMIKA MNOOOOOOOOO.
 
Isionekane nini boss.Ebu ongeza nyama tafadhali
Mkuu, hao jamaa wa juu! Wana tochi inayowamlikia wao tu ili Hali wanachama wao wako gizani wasione, wamefumbwa kwenye koti la maamuzi ya balaza kuu la Chadema,

Siasa ndio iko hivyo, kuna wakati Masikini huchangishwa fedha ili viongozi wa juu wakafanyie sherehe
 
Nchi yangu ya ajabu sana.
 
Acha uzuzu ww bwege chadema walishawavua ubunge, kumbuka hata mahakamani rufaa inaweza kutupiliwa mbali km haina mashiko. CCM mlirogwa na nani mpaka mjitoe akili na kukojolea katiba? Nakumbuka mlishasema tundu Lissu alijimiminia risasi, mkasema azohori alijiteka na ben saa8 alijipoteza.
 
na kama wanadai wamewavua uanachama huku hawataki kusikiliza rufaa zao sasa kinachowasumbua nini ? mmemvua uanachama siyo mwanachama wenu kinachowafanya waanze kutaka kumsumbua mama avunje katiba kuingilia mhimili wa bunge ni nini?

Hilo bunge la majizi ya kura liingiliwe mara 2? Hukumbuki dhalimu alipomuagiza spika awatoe wabunge huko bungeni, kisha yeye awateke na kuwabambikia kesi huku nje?
 

Bunge lenyewe hilo la majizi ya kura, tunajua ni jinsi gani hilo bunge kibogoyo limepatikana, hivyo linashinikizwa maana tunajua halina uhalali wa umma.
 
Inajulikana wazi kuwa Rais Samia Suluhu kabla ya kukabidhiwa madaraka haya ya urais, aliapa kuitii na kuiheshimu Katiba ya nchi.

Katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, katika Ibara ya 67(1)(b) inaeleza wazi kuwa huwezi kuwa mbunge wa Bunge letu, bila kwanza kuwa mwanachama chama cha siasa nchini.

Tunajua pia kuwa chama cha CHADEMA kilishawavua uanachama wao hao wanaoitwa ni wabunge wa Viti Maalum wa CHADEMA

Sasa tunamtegemea Rais wetu Samia Suluhu, alihutubie Bunge baadaye leo majira ya saa 10 jioni na kukitengua kitendawili hicho.

Aidha awe upande wa Spika Ndugai, ambaye kila mwananchi anajua kuwa ameivunja Katiba ya nchi, kwa kuendelea kuwatambua na kuwakumbatia hao wabunge akina Halima Mdee, au asimamie Katiba ya nchi na kumueleza Spika Ndugai kuwa anakosea kuendelea kuwakumbatia wabunge hao, kwa kuwa siyo wabunge halali, kwa mujibu wa Katiba yetu.

Kwa kuwa Rais wetu ameonyesha wazi kuwa anaitii na kuiheshimu Katiba ya nchi yetu. kwa hiyo "ramli" ya nini kitatokea baada ya hotuba yake hiyo kuhusiana na wabunge hao kinatabirika
 
Mara nyingi wanaoandikaga ujinga huu ni watu vilaza sana waliokuwa wanaruka dirishani mwalimu wa hisabati akiingia kwa kifupi una tatizo kubwa sana kwenye ubongo wako hafu nahisi ulikuwa unatoroka darasani kila siku haujui unachoongea ni nn umekaririshwa maneno tu rubbish.
 
Jibu hoja na wala usibwabwaje.

Hivi Spika Ndugai kuendelea kuwakumbatia hao wabunge kina Halima Mdee, wakati inajulikana wazi kiwa chama chao cha Chadema kimeshawavua uanachama, je wako bungeni wakiwa wanachama wa chama kipi cha siasa?

Kwa kuwa inafahamika kuwa ni takwa la kikatiba, kuwa ili uwe mbunge wa Bunge letu ni LAZIMA uwe mwanachama wa chama cha siasa.
 
Rais yuko njia panda kwenye hili. Akisimamia katiba upande wa chama chake utanuna sana...! Sana sana anachoweza kufanya ni kufunika kombe....!
Ndiyo maana akamuita Spika Ndugai katika kikao cha "siri" pale Ikulu ya Chamwino Dodoma

Wananchi tutaifuatilia hiyo hotuba kwa makini sana na iwapo ataipitisha hotuba yake bila kugusia suala hili la wabunge wa viti maalum wa Chadema, basi tutajua ndiyo wale wale wanaCCM, na hakuna jipya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…