BAWACHA: Rais Samia asiwatambue Wabunge 19 wa Viti Maalum waliofukuzwa uanachama CHADEMA

Mi kwa ushauri wangu kama kuna sababu za msingi ni vema akavunja tu bunge ili tuanze upya, kila mmoja akapambane kivyake
Inaeleweka wazi kuwa kiburi chote alichonacho Spika Ndugai, alipewa na mwendazake.

Sasa mwendazake amepumzika katika pumziko la milele.

Macho na masikio yetu yapo kwa Rais wetu, Samia Suluhu, ambaye ameonyesha kutaka kusimamia haki.

Kwa hiyo kwa hili la wabunge wa viti maalum wa Chadema, hebu tuone huo mtinani mkubwa wa kwanza, atauvukaje
 
Rais anahusika vipi na wabunge wa Chadema kwani yeye ni Mwenyekiti wa Chadema??
 
Rais anahusika vipi na wabunge wa Chadema kwani yeye ni Mwenyekiti wa Chadema??
Hivi kuwa CCM maana yake ni kuwa mtu wa kujibu hoja "kipuuzi" kiasi hicho??

Kwani hujui kuwa Rais wa nchi anahusika na mambo yote yanayohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania "including" uendeshaji wa mhimili wa Bunge??
 
Hivi kuwa CCM maana yake ndiyo maana yake unakuwa mtu wa kujibu hoja kiasi hicho??

Kwani hujui kuwa Rais wa nchi anahusika na mambo yote yanayohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania "including" uendeshaji wa mhimili wa Bunge??
Hiyo katiba unayoizungumzia wewe inasemaje kuhusiana na mamlaka ya Rais juu ya Mbunge?
 
Hii issue ya wabunge 19 ni kikatiba na kwamba chama kitakuwa na nafasi ya viti maalumu bungeni endapo kitapata zaidi ya theluthi moja kwenye kura zote kwenye matokeo katika uchaguzi mkuu.

Pili, tukumbuke NEC ikishapeleka majina ya wabunge hawa 19 wa CHADEMA kuteuliwa katika nafasi za viti maalum bungeni baada ya chama chao kukataa kuwatambua na kukataa matokeo. Kwa hali hii CHADEMA ilisusia. Ni wazi kwamba hata kama mbunge amevuliwa uanachama na chama chake, bado rais ana mamlaka ya kuthibitisha uhalali kwa kufata katiba.

Ni wazi rais atabariki kilichoamuliwa na tume ya uchaguzi, bunge na katiba yenyewe.
 
Rais yuko njia panda kwenye hili... Akisimamia katiba upande wa chama chake utanuna sana...! Sana sana anachoweza kufanya ni kufunika kombe....!
Ndivyo atakavyofanya kuuchuna tu maana kuharibu walisharibu toka awali.
 
Mimi sioni kama ni mtihani mkubwa kwa kweli. Wahuni walitaka kuipindua Katiba ili asiingie Ikulu hivyo inabidi aiheshimu Katiba na kama ataiheshimu katiba basi hatasita kuisimamia vile ipasavyo ili kuwaondoa COVID-19 bungeni. Akiamua kuwasikiliza wahuni na kuwaacha basi itakula kwake na atapata tabu sana.
 
Tunamuombea kwa mungu mama aendelee kuitii katiba aliyoapa kuilinda, kina halima mdee wako bungeni kimakosa, spika hakupaswa kuwalinda kamwe, alipaswa kuwaondoa bungeni Mara moja.Maana wenye chama Chao wanasema hawawatambui, kwa nn kuwalazimisha?
 
Kweli shule ni muhimu, hivi Rais atafanya nini juu ya hilo suala? Maana yeye yupo kwenye muhimili wa serikali na hilo suala lipo kwenye muhimili wa bunge. Spika anadai alipelekewa majina na NEC, je Rais atawezaje kuingilia Muhimili mwingine wa nchi? Huoni atakua anavunja katiba ya nchi, ili tu awafurahishe baadhi ya watu.

Ikiwa ni kweli CHADEMA hawakupeleka majina NEC, kwanini wasiende mahakamani kupinga hilo suala, kwanini wasifungue kesi ya kikatiba mahakama kuu? Ushahidi si wanao? Shida kubwa sana ya sisi wananchi (wacheza mdumange) hatujawajua wanasiasa, hilo suala unaweza kukuta wakubwa wa chama wanalijua vzr, na walishapiga pesa. Wanachofanya ni kujikosha tu

Hivi Halima ni wa kumgeuka Mbowe?
 
Rais yuko njia panda kwenye hili... Akisimamia katiba upande wa chama chake utanuna sana...! Sana sana anachoweza kufanya ni kufunika kombe....!
Hii itakuwa msumari wa moto!! Sioni gumu waambiwe wakakidhi kwanza takwa LA kikatiba
 
Mkuu mbona wewe Ni mkongwe humu afu unaongea vitu simple Sana Sasa kwa akili yako unafikiri Mh Rais anaweza kuwafukuza hao covid 19?hao wamewekwa na serikali ili angalau wawadanganye mabeberu kua ni bunge la vyama vingi na Kuna hela hua serikali inapokea kwa budget ya nchi kutokana na kua nchi ipo kwenye mfumo wa democracy,
 
Kama mtihani haupo kwa mbowe ambae ni mwenyekiti wao yeye raisi inakuwaje uwe mtihani wajibuni rufaa zao wapeni barua za kuwafukuza zaidi ya hapo waacheni waendelee kula nchi tatizo lipo shinani wanapotokea!
 
Nafikiri hilo ni jukumu la Spika na wala sio Rais kuhakikisha katiba imefuatwa katikak suala hilo.
 
Kama mtihani haupo kwa mbowe ambae ni mwenyekiti wao yeye raisi inakuwaje uwe mtihani wajibuni rufaa zao wapeni barua za kuwafukuza zaidi ya hapo waacheni waendelee kula nchi tatizo lipo shinani wanapotokea!
Mtihani mkubwa kwa Rais, kwa kuwa anatakiwa kuhakikisha kuwa kila mtanzania anapaswa kuitii na kuiheshimu Katiba ya nchi
 
Spika ndiye mwenye kukumbatia hili, maana lipo kwenye muhimili wake. Kutaka kumbebesha lawama Mama sio sawa!!
 
Sijaona hoja zaidi ya dharau tu. Weka akiba ya maneno ndugu...!!
 
Huo ni muhimili mwingine joh...
waache wajisoti wenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…