BBT yaanza kukwama. Tulisema hapa kuwa BBT ni shimo la kuzikia fedha za Kodi zetu

Watanzania mna vichwa butu sana.
Badala ya kuchangia nia nzuri ya serkali kuondoa vijana barabarani, ninyi mna zomea na kufurahia matatizo.
Mna mindset za kushindwa1
 
Watanzania mna vichwa butu sana.
Badala ya kuchangia nia nzuri ya serkali kuondoa vijana barabarani, ninyi mna zomea na kufurahia matatizo.
Mna mindset za kushindwa1
Aliyeanzisha ndiyo ana mindset ya kushindwa. Wote tunatambua kuwa nia ilikuwa njema, lkn vijana wa aliowachukuwa siyo sahihi.


Angewapa fursa na uwezo huo vijana waliopo ktk kilimo na ufugaji moja kwa moja, badala ya kukusanya vijana wadangaji, wacheza pool na wapaka poda. Wao kila kitu wanakiona ni tatizo.
 
Kwa hiyo hao vijana watafutiwe mtaji, watunzwe, na pa kuuza watafutiwe, kwani faida inaenda kwa nani? Au Serikali inapata gawio kwenye huu mradi?
Serikali inaweza kuwaonesha masoko ya nje kwa kuwapa uwezo kushiriki maonesha ya kimataifa ya kilimo, huko watatafuta masoko wenyewe
 
Sounds good ila hivi ni kweli kwamba soko la hizi bidhaa mbali mbali za mashambani + mifugo Tanzania ni la uhakika kiasi hicho? Naona kama vijana wana hoja hivi
 
Huyo ng'ombe wa kuishia kilo 200 tu wanamlisha mchanga ?
Maana hata wafugaji wa kawaida kabisa ambao S100 hawapendi wanazalisha ng'ombe wenye kilo zaidi ya 200
 
Uliipinga kwa sababu gani za msingi ??
 
Unaenda sokoni unakuta wateja wanataka kumnunua kwa laki 5 huyo ng'ombe aliyekugharimu laki 7 kumfuga . Nchi hii aliyeturoga naye karogwa.
Eti kilimo bila ruzuku na kama KAZI haiwezekani!.kule ulaya na marekani serikali zinatoa ruzuku kwa wakulima wake.Kilimo na Ufugaji ni wito na si kipato.Hebu fikiria ulime eka Moja weka gharama za kukodi,kulima,kupandia,kupalilia,kuvuna,kukusanya,kubangua,kupaki na kupeleka sokoni,mbolea kupandia,kukuzia na kunenepeshea ,alafu uuze gunia tsh90,000.ndipo upate fedha ya kujikimu,hakuna kijana wa mjini na wale walioenda shule waliotoka familia zinazojiweza anaweza kufanya KAZI hiyo.ila kama itatolewa kwa wenye wito na kwa uwazi zaidi bbt itaweza kafanikiwa.
 
Wewe toka lini unalipa kodi?

Kwa mwandiko wako tu unaonesha hufanyi kazi.
 
Kwanini hauendi Ulaya ukalime?
 
Kwanini hauendi Ulaya ukalime?
Mimi ni Mkulima na pia Mfugaji najua shuruba za kulima na kufuga inahitaji moyo na uvumilvu na sio lelemama mtu hajawahi kufuga Wala kumuana mzazi wake akifuga atafuga huyo labda awe magereza au Jeshini,lakini kwa hiari ng'ooo
 
Waziri au serikali badala ya kuchukua watu kama wewe mkatengeneza mpango mkakati wa kuinua kilimo cha umwagiliaji, anaokoteza "nadharia" na wasomi wake wa kinadharia ambapo mwisho wa siku hakuna matokeo chanya yale yaliyokuwa yanasemwa.
 
Mimi ni Mkulima na pia Mfugaji najua shuruba za kulima na kufuga inahitaji moyo na uvumilvu na sio lelemama mtu hajawahi kufuga Wala kumuana mzazi wake akifuga atafuga huyo labda awe magereza au Jeshini,lakini kwa hiari ng'ooo
Kwani ulikatazwa kufuga na kulima Tanzania hii?

Au unataka mtu ambae siyo mfugaji wala siyo mkulima aje kukufundisha wewe mfugaji na mkulima?

Wewe utakuwa siyo mfugaji, ni mchungaji.

Pia utakuwa siyo mkulima (farmer) ni "peasant" (sifahamu Kiswahili chake), Kiarabu chake ni "falah".

Mana Watanzania tumewazowea, tu analima vieka viwili vitatu au anacchunga vingombe kumi au kumi na tano anasema mimi mkulima, au mimi mfugaji.

Tupishe huko, mkulima au mfugaji ana muda wa kuingia JF kubishana?
 
Wakulima wako huko chaka sahvi dada yangu kipenzi
Ila siyo hawa wa BBT ...wakulima wa Google,whatsap group na malaptop
[emoji1]
Kilimo kina wenyewe

Ova
Nchi ina danadana nyingi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…