BBT yaanza kukwama. Tulisema hapa kuwa BBT ni shimo la kuzikia fedha za Kodi zetu

BBT yaanza kukwama. Tulisema hapa kuwa BBT ni shimo la kuzikia fedha za Kodi zetu

Naunga mkono, capacity building kwa vijana wetu bado inahitajika.
P
Mimi siungi mkono ''Protectionism' kabisa. Ninatamani sana soko la ajira na Biashara liachwe huru waingie vijana kutoka mataifa mengine ili hawa wakwetu wajifunze. Vijana wetu siyo aggressive kabisa , ni kulia lia tu na porojo

Yaani mtu analeta habari hakuna soko la ng'ombe Tanzania! huu kama si ujinga basi sijui ujinga ni kitu gani.
Hao wafugaji na hawajui haya
1. Kwamba kuuza nyama kunaongeza thamani zaidi ya ng'ombe
2. Kwamba kuna soko la ngozi kwa hao ng'ombe
3. Kwamba kinyesi ni mbolea watakayoitumia katika mashamba ya Carrot , Biringanya, Nyanya n.k.
4. Kwamba kinyeshi wanaweza kukitumia katika Bio-gas na kupunguza gharama za mambo madogo
Kuna vitu vingi sana wanaweza kufanya , hawafikiri wanakimbilia kumlaumu Bashe

Nina wa 'challenge' tangu uhuru nitajieni Waziri mmoja tu aliyekwenda mbali katika kutafsiri kilimo kuliko Bashe

Hivi mnataka watu warudi kule kwa Waziri mkuu kuagiza mvua za mabomu kutoka Thailand!

Bashe anasema hatuwezi kufa njaa kwasababu tumekaa tunaangalia Mawingu ya mvua maji yakitirika kwenda Baharini na kwenye maziwa. Tunataka kilimo 365 days.
 
Watu siyo 'innovative' halafu hawana business acumen. Mtu anataka Waziri Bashe amtafutie soko! noo ni ujinga.

Badala ya kulalamika katika TV,wafugaji walipaswa watafute connections halafu ikihitajika Waziri ndipo wamwambie.
Mfano, wamepata soko Mauritius lakini kuna matatizo ya kibiashara , hapo waziri anahusika ku facilitate

Wafanyabishara nje wanakuja nchini, serikali za nchi zao hazishusiki na biashara lakini zinatengeneza mazingira ya biashara. Waziri wa Biashara wa Japana atawasiliana na Balozi wa Japan Tanzania kwa fursa za kuuza magari na vipuri. Research ya soko wanafanya Wafanyabiashara wenyewe.

Yaani Tanzania hii kuanzia Mtwara hadi Tanga, Pemba hadi Kigoma mtu hawezi kuuza ng'ombe.

Kwanini wafikiri kuuza ng'ombe na si nyama ! Mbona nyama ya Kongwa inang'ang'aniwa Dar es Salaam
Ubora wa nyama na mazingira ya kuuzia ni muhimu , siyo zama za kutwanga nyama kwenye magogo.
Ni mashine maji na usafi.

Huyu kijana anayetaka kuuza ng'ombe masikini hajui kuna ngozi .

Watu wanamlaumu Bashe! . Bashe hawezi kukufanyia kila kitu, anatengeneza mazingira mazuri ya wewe kufanikiwa.
Tena mifugo wala Bashe si wizara yake, hiyo wizara inaendeshwa na Waziri Abdallah Ulega.

Waliuona mpango waBBT wa Bashe ni mzuri na wao waka u adopt kwenye mifugo. Wame u plan vizuri tu, kwa kushirikiana hizi wizara mbili.

Halafu hao wanaolalamika naamini siyo hao vijana wa BBT ni mafedhuli fulani tu wapo katika kujitahidi kupakaza matope (gutter politics).

Ukienda kwa kina utakuta ni walewale wenye kusaliti mipango mingine ya maendeleo ya awamu hii ya mama Samia.
 
Misungwi hapo kuna matukio mawili matatu ya maendeleo hayakuwafurahisha taasisi yenye kumiliki ardhi kubwa hapo.

BBT ni mojawapo tu ya "fitna", maendeleo mengine yanayofanyika hapo kupitia serikali ambayo vingunge hao wa ardhi wanaona kama "fitna" na yamewaingiliwa kwenye himaya yao mfululizo na kuwaharibia malengo yao.

Tukio lingine la maendeleo ambalo hawalipigi vita moja kwa moja lakini nalo wanalipiga vita kivingine ni la Wilaya ya Misungwi kutowa eneo kubwa la kujengwa bandari ya kisasa.

Tutegemee BBT Misungwi kupigwa vita kali tu.

Ng'ombe hawajawahi kukosa soko Tanzania hii. Tunawafahamu wanaozusha uongo huo.
 
Tena mifugo wala Bashe si wizara yake, hiyo wizara inaendeshwa na Waziri Abdallah Ulega.
Nimeshangaa sana
Waliuona mpango wa VVT wa Bashe ni muri na wao waka u adopt kwenye mifugo. Wame u plan vizuri tu, kwa kushirikiana hizi wizara mbili.
Ni jambo zuri
Halafu hao wanaolalamika naamini siyo hao vijana wa BBT ni mafedhuli fulani tu wapo katika kujitahidi kupakaza matope (gutter politics).
Ni viumbe wa ajabu sana.
Mtu anatoka Oman anachukua ng'ombe Dodoma anafungua Bucha Dar anauza.
Kijana wa Tanzania yupo katika TV na mwingine JF wakitafuta soko la ng'ombe.

Hili ni tatizo la 'Protectionism', sera mbaya sana. Hatuna vijana wabunifu kwasababu hawana '' competitors'' katika Market. Natamani serikali iondoe vibali vya kufanya kazi na Biashara vijana wa Kenya, Uganda, Rwanda n.k wamiminike ili hawa wakwetu watie akili kidogo.

Nimewauliza hapa , waniambie Waziri wa Kilimo yoyote aliyewahi kuwa na maono na kuyafanyia kazi kama Bashe

Bashe anaweza kukosea, hoja si kukosea bali sisi kumsaidia ili sote tufanikiwe kwa jambo jema.

Tunataka tuwe 'food basket' ya Afrika, inawezakana. Bashe anaonyesha njia sasa leo analaumiwa

Hivi si tulikuwa na PM anayeagiza mvua Thailand. Huo ndio ubunifu kweli.

Nawa challenge tena, kwa baraza la mawaziri la sasa kuanzia PM hadi manaibu, nitajieni mmoja tu mwenye ubunifu zaidi ya Bashe, mmoja tu! Ukiniuliza naweza kusema Bashe anaweza kuwa PM mzuri sana, anajua details za kazi zake

Leo kamuulize Mbolea, bei ya ngogwe, matatizo ya karanga, shida za kisamvu atakupa details zote.

Kaulize, SGR inakwama wapi, hutapewa jibu. Kaulize kwanini serikali inataka kusikiliza watu wakiongea mapenzi VPN, hutapewa jibu. Kaulize kwanini viongozi wamerudi Dar na si Dodoma, hakuna jibu.

Badala ya kulalamika katika TV,wafugaji walipaswa watafute connections halafu ikihitajika Waziri ndipo wamwambie.
Mfano, wamepata soko Mauritius lakini kuna matatizo ya kibiashara , hapo waziri anahusika ku facilitate
Ng'ombe za kupeleka Mauritius ziko wapi? Hao vijana hakuna mwenye zaidi ya kumi.
Ni tambo tu ili waonekane wapo
 
Ng'ombe za kupeleka Mauritius ziko wapi? Hao vijana hakuna mwenye zaidi ya kumi.
Ni tambo tu ili waonekane wapo
Hii mada inaonekana haina maana , nili iona katika mtazamo huo unaousema. Nilipopitia maoni kutaka kujua zaidi nikagundua kuna tatizo kubwa kweli na mada inatusaidia kujua mambo mengi
1. Kwamba, Waziri Bashe anapigwa vita tu na haijulikani ni kwanini
2. Vijana wetu siyo aggressive, ni wavivu wa kufikiri na wazuri sana wa kuupepeta
3. Serikali ifute sera ya kulinda ajira na biashara kwa Wananchi '' protectionism' ili watu wa mataifa waje hapa pengine vijana wetu wataondoka katika lindi la usingizi kama huu wa kusbiri Bashe apite kila nyumba akiwatafutia soko.
 
Nimeshangaa sana

Ni jambo zuri

Ni viumbe wa ajabu sana.
Mtu anatoka Oman anachukua ng'ombe Dodoma anafungua Bucha Dar anauza.
Kijana wa Tanzania yupo katika TV na mwingine JF wakitafuta soko la ng'ombe.

Hili ni tatizo la 'Protectionism', sera mbaya sana. Hatuna vijana wabunifu kwasababu hawana '' competitors'' katika Market. Natamani serikali iondoe vibali vya kufanya kazi na Biashara vijana wa Kenya, Uganda, Rwanda n.k wamiminike ili hawa wakwetu watie akili kidogo.

Nimewauliza hapa , waniambie Waziri wa Kilimo yoyote aliyewahi kuwa na maono na kuyafanyia kazi kama Bashe

Bashe anaweza kukosea, hoja si kukosea bali sisi kumsaidia ili sote tufanikiwe kwa jambo jema.

Tunataka tuwe 'food basket' ya Afrika, inawezakana. Bashe anaonyesha njia sasa leo analaumiwa

Hivi si tulikuwa na PM anayeagiza mvua Thailand. Huo ndio ubunifu kweli.

Nawa challenge tena, kwa baraza la mawaziri la sasa kuanzia PM hadi manaibu, nitajieni mmoja tu mwenye ubunifu zaidi ya Bashe, mmoja tu! Ukiniuliza naweza kusema Bashe anaweza kuwa PM mzuri sana, anajua details za kazi zake

Leo kamuulize Mbolea, bei ya ngogwe, matatizo ya karanga, shida za kisamvu atakupa details zote.

Kaulize, SGR inakwama wapi, hutapewa jibu. Kaulize kwanini serikali inataka kusikiliza watu wakiongea mapenzi VPN, hutapewa jibu. Kaulize kwanini viongozi wamerudi Dar na si Dodoma, hakuna jibu.
Bashe hahusiki na mifugo, ingawa anawasaidia sana kwa kuwa BBT ni wazo lake.

Hapa hilo la kukosa soko la ng'ombe ni fitina tu hizo ambazo hazina ukweli.

Kwanza biashara ya ng'ombe haitegemei ng'ombe kuuzwa haraka haraka. Ng'ombe kama hajauzika na kishakuwa dume mkubwa anauzika mnada wowote ule, kama ni jike wala hafanyiwi haraka kama hajafika bei, anapandishwa hata kwa sindano, anazaa anatowa maziwa.

Kwanza nchi za nje kwa ng'ombe wazima hawataki kununuwa ng'ombe dume, wanataka ng'ombe jike ytena awe na mimba, hao wananunuliwa kwa kugombaniwa. Inawapunguzia gharama za usafrishaji wanunuzi.

Wanunuzi wa Saudi Arabia wananunua ng'ombe majike tu tena wenye mimba kwa ng'ombe hai. Na hiyo ni kazi ndogo sana kwa kituo cha kufugia ng'ombe.

Anaesema ng'ombe hawana soko, huyo ni mwehu mhujumu uchumi wa kupigwa risasi za kisogo.
 
Ng'ombe za kupeleka Mauritius ziko wapi? Hao vijana hakuna mwenye zaidi ya kumi.
Ni tambo tu ili waonekane wapo
Wala siyo hao vijana waliyoyaandika hayo. Hao ni watu wasioitakia mema Tanzania.
 
Bashe hahusiki na mifugo, ingaawa anawasaidia sana kwa kuwa BBT ni wazo lake.\
Simba wangefungwa na Al Ahly angelaumiwa Bashe na BBT. Hwajui tofauti kwasababu wanamwandama
Anaesema ng'ombe hawana soko, huyo ni mwehu mhujumu uchumi wa kupigwa risasi za kisogo.
OK tufanye kwamba Wizara ya Mifugo ni ya Bashe, waulize watu kwa ng'ombe kukosa soko , Bashe amekosea wapi?
Hwkuna jibu, analaumiwa tu.

Bashe kafanya ubunifu kuliko mawaziri wote akiwemo PM, huu ni ukweli hata kama unauma.

Treni ya Mwakyembe badala ya kufanyiwa improvement imeachwa ife kwasbabu mawaziri waliofuata hawana maono

Badala ya kufikiria tunaunganisha vipi Vyuo na shule za Sekondari katika mkongo wa Taifa wa Internet , kuna watu wanakaa vikao vya kudai VPN ili kusikiliza wanafunzi wa CBE wakitongozana na wale wa DUCE!

Mkongo huo huo wa internet unaopita kwetu kwenda Rwanda , unafanya vizuri sana Rwanda.
 
Projects za serikali za kukusanya wapiga picha, ma DJ, wacheza sarakasi na madalali wa nguo kwenda kuwapa "training" ili walime?

Kwamba Bashe haamini vyuo vya kilimo kama SUA na LITA vyote mpaka akakusanye wavaa pensi Dar awapeleke kwenye vituo mikoani? Bashe haamini vyuo vinavyosimamiwa na wizara ya elimu na ya kwake ya kilimo anaamini vijana aliookoteleza.

Yani siku wizara ya elimu ianzishe shule za sayansi mpya ianze kutafuta madalali wa vyumba ikawafundishe ufundi kisha ndio wawe walimu wakati wizara hiyohiyo inatoa graduates kibao wenye utaalamu huo.

Na wewe ukakaa ukisubiria matokeo chanya.
Kwa hiyo mkuu unataka kuhitimisha kuwa hiyo project kubwa ya kilimo ya mfano haikuhusisha wataalam husika wenye dhamana ya kilimo Tanzania.

Hii mbona inakuwa ngumu kuamini.
 
Afadhali umedhihirisha utupu wa fuvu lako,kwa hiyo ulitaka fursa hizo za kilimo wapewe watu waliosoma vyuo vya kilimo na ufundi tu!?..unajua malengo ya BBT au walau tatizo la ajira tz!?..lipo kwa wasomi tu!?..watu wenye elimu ya chuo ni wangapi tz!?
Pengine hukumuelewa mkuu,kamaanisha kuwa mradi umeanzishwa pasipo kushirikisha wenye dhamana ya sekta husika.
 
Simba wangefungwa na Al Ahly angelaumiwa Bashe na BBT. Hwajui tofauti kwasababu wanamwandama

OK tufanye kwamba Wizara ya Mifugo ni ya Bashe, waulize watu kwa ng'ombe kukosa soko , Bashe amekosea wapi?
Hwkuna jibu, analaumiwa tu.

Bashe kafanya ubunifu kuliko mawaziri wote akiwemo PM, huu ni ukweli hata kama unauma.

Treni ya Mwakyembe badala ya kufanyiwa improvement imeachwa ife kwasbabu mawaziri waliofuata hawana maono

Badala ya kufikiria tunaunganisha vipi Vyuo na shule za Sekondari katika mkongo wa Taifa wa Internet , kuna watu wanakaa vikao vya kudai VPN ili kusikiliza wanafunzi wa CBE wakitongozana na wale wa DUCE!

Mkongo huo huo wa internet unaopita kwetu kwenda Rwanda , unafanya vizuri sana Rwanda.
Unamuongelea Nape?

Nape siyo mtendaji ni mpoiga porojo zaa kisiasa. Sampuli yake ya uwaziri imepitwa na wakati. Uwaziri wa matamko.

cc Nape Nnauye
 
Miradi mingi ya serikali inakwama kwa sababu wanao ileta hiyo miradi wanakuwa na nia ya kiupigaji zaidi kuliko kuwainua wananchi kiuchumi.

Mf; kulikuwa na mradi wa kuwagawia wananchi wa vijijini mitungi ya gesi
Hivi unafikiri kipi bora kati ya kupunguza gharama za kujaza gesi au kuwagawia wananchi mitungi ya gesi bure ambayo baada ya gesi kwisha hawataweza kuijaza tena

Miradi kama Mkukuta, Mkurabita, tasaf, BBT, hiyo miradi imejaa upigaji mwingi.
Hao vijana hawajiongezi? Hii ni biashara bana. Masoko hutafutwa. Waende sekta ya utalii kuna mahitaji makubwa ya nyama na kuna baadhi ya mahoteli wanaagiza nyama ya ubora maalum kutoka botswana na Afrika Kusini.
 
Umeambiwa na nani? Unaamini habari za kuambiwa na mwanasiasa mtanzania?
Narudia kusema kama hujaleta fitina basi BBT haiwezi kufeli kirahisi hivyo Kwa sababu zifuatazo
-Serikali inawezaje Kushindwa kuingia mkataba na viwanda vya nyama eg TanChoice,wanunuzi wakubwa wanaouza Nje au wamiliki wa mabucha? Kwa nini wasiwe na bucha zao Mjini?

-Pili kwenye Kilimo inashindwaje kulima mazao maalumu ya kufanya exports kulingana na maeneo na hivyo Kwa utaratibu wa contract farming? Shule zote za bweni na vyuo?

Bashe ni business minded hawezi ruhusu BBT ifeli kizembe hivyo nakimsi gi lazima huu mradi uwe na gestation period walau ya miaka 5 kulelewa na Serikali kabla ya ku hand over Kwa Vijana.

Kama Wameshindwa wanipende kazi ya kuwasaidia mawazo.
 
E

Exactly, kilo ya nyama ni elfu 8, ngombe anatoa kilo 400 za nyama, wakitengeneza butcher ya kisasa qana uhakika wa milioni 7 kila siku yaani kuuza ngombe wawili kila siku
Hesabu za kwny karatasu hazijawahi kufeli.
 
Mtungi mdogo kujaza elfu 23, kununua mwanzo ukiwa imejaa ni elfu 55,ukipewa mtungi wa gas uliojaa ili ukiisha ujaze mwenyewe hujasaidiwa!?..na unadhani gas tunayotumia inatoka mtwara siyo kwamba serikali inaweza amua kupunguza tu!?..muwe mnafuatilia kwa undani mambo ya nchi yenu na kiuyachakata kifikra
Je umewahi kuyaishi maisha ya vijijini lakini?
Kuipata hela ya kujaza gas kwenye mtungi ni issue.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom