Behewa za SGR zaanza kuwasili nchini Tanzania

Behewa za SGR zaanza kuwasili nchini Tanzania

kwamba hizi behewa kama hivyo zinavyoonekana hatuwezi kuzitengeneza hapa bongo? mbona mabasi wanaunda mabodi? au si kuunda behewa tu tupu halina injini.
Yaani hata mimi nimewaza hivyo
Je tungeagiza chassis tu na body tukaungaunga kwetu tungeshindwa?

Mbona meli tunatengeneza
Hapo tutakuwa tunapigwa kwa kila kitu
Naaona hata shuka na mito inatoka China
 
kwamba hizi behewa kama hivyo zinavyoonekana hatuwezi kuzitengeneza hapa bongo? mbona mabasi wanaunda mabodi? au si kuunda behewa tu tupu halina injini.
Mkuu ata Veta wanaweza kutengeneza bila wasiwasi
 
Halafu muandae watu wa kutosha kusimamia wabongo ndani ya hayo mabehewa!

Maana wengi wamezoea maisha ya kuharibu haribu tu vitu, kutokana na kukosa ile culture of care and maintainance.
Hiyo kazi wapewe Jkt
 
Pascal Mayalla uzi kama hizi huwa yeye ashiriki kujibu hoja huwa ana like tuu nakupotea...
MADAI
Mabehewa 30 na vichwa 2 vya treni za SGR mali ya TRC vinapigwa mnada 25/11/2022, nchini Germany kufuatia mgogoro wa TRC na EUROWAGON Railways Limited (Turkey), iliyopewa kazi ya kukarabati na kutia nakshi. TRC wamelipa Sh. 23 bilioni (35% ya kazi).

Inadaiwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa EUROWAGON, Yalçın Aydemir amesema wataanza na mnada wa mabehewa 17 ya awali katika mnada huo (hadi sasa wateja wawili wamepatikana kutoka Serbia), na mabehewa 13 na vichwa 2 vya treni za mwendokasi vitasubiri hadi mteja apatikane na kisha watavipiga mnada.

Shirika la Reli Tanzania (TRC) na kampuni ya EUROWAGON ya kutoka Turkey ziliingia makubaliano Oktoba 2020 kwa ajili ya ujenzi (ukarabati na utiaji nakshi) wa vichwa viwili vya treni ya umeme na mabehewa 30 ya abiria ambao ulitegemewa kukamilika ifikapo Novemba 2021.

TRC ilisitisha mkataba huo Februari 25, 2022 kwa madai kwamba EUROWAGON wamechelewesha kazi na mazungumzo hayajawahi kuendelea. Kampuni ya RINA ilipewa kazi ya kuthibitisha kazi ya ukarabati na utiaji nakshi mabehewa hayo na kuthibitisha kwamba kazi hiyo imekamilika kwa 50%.

Hivyo EUROWAGON Railways Limited wanataka malipo ya Sh. 10 bilioni, ambayo ni 15% ya kazi iliyothibishwa na RINA kwamba kazi ya ukarabati na utiaji nakshi ilifanyika kwa 50% na malipo ya Sh. 23 bilioni ni kwa ajili ya 35% ya kazi hiyo. Malipo haya yalifanyika Desemba 14, 2020

Baada ya kuvunja mkataba huo Februari 25, 2022 na EUROWAGON, TRC wakaingia mkataba na kampuni nyingine kwa ajili ya ukarabati wa mabehewa na kutia nakshi. Kampuni hizo ni Zeller KG Engineer (Austria), Baltic Port Service GmbH na Lueckemeir Transport Logistics GmbH (Germany)

EUROWAGON kupitia Mwanasheria Duygu Seda, wakamuandikia barua Mkurugenzi wa TRC kwamba Tanzania Railways Corporation (TRC) wamevunja mkataba kwa njia ambazo siyo halali. TRC walivunja mkataba kwa kigezo cha EUROWAGON kushindwa kuwasilisha Dhamana ya Utendaji (performance Bond)

Mwanasheria wa EUROWAGON, Duygu Seda katika barua hiyo kwa Mkurugenzi wa TRC amemueleza kwamba kutokana na sheria za EU, Germany, Turkey na Austria na makubaliano kati ya EU na Turkey, TRC hawaruhusiwi kufika yalipo mabehewa na vichwa vya SGR wala kusafirisha isipokuwa EUROWAGON.

TRC hawakununua vichwa na mabehewa mapya kwa ajili ya SGR, isipokuwa, EUROWAGON waliopewa zabuni walinunua vichwa 2 na mabehewa 30 kutoka kampuni ya Reli inayomilikiwa na serikali ya Germany, DB Regio, ili kuvikarabati na kuvitia nakshi nakshi, kisha vilisajiliwa kuwa mali ya TRC

Mkurugenzi Mtendaji wa EUROWAGON, Yalcin Aydemir anasema kwamba TRC walimpa kazi bila dhamana ya Utendaji (Bank/performance guarantee) lakini ghafla TRC wakabadili gia angani na kuidai. Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa anasema EUROWAGON wanatapatapa tu hawana hoja.

TRC June 17, 2022 ilisema imesitisha mkataba na kampuni ya EUROWAGON, iliyokuwa ikitengeneza mabehewa hayo baada ya kushindwa kukamilisha ukarabati vichwa 2 na mabehewa 30 ya abiria, kwa ajili ya majaribio hayo, ni kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano TRC, Jamila Mbarouk

Vifaa hivyo kutoka EUROWAGON vilitakiwa kukamilika Novemba, 2021, TRC ilisitisha mkataba na kuwataarifu kwa barua Februari 25, 2022 na kuendelea na kazi ya kukamilisha ukarabati unaotarajiwa kukamilika Agosti mwaka 2022,” alisema mkuu wa Kitengo cha Uhusiano TRC, Jamila Mbarouk

Kwa mujibu wa Tanzania Railways Corporation, taarifa waliyoeleza kwa waandishi wa habari June 15, 2022, walisema Mkataba kati yao na EUROWAGON unaipa TRC haki ya kuchukua jukumu la kukamilisha ukarabati iwapo mzabuni atashindwa kuzingatia masharti ya mkataba.

View attachment 2424063
Hapa ninachokisoma na kinachokanushwa ni vitu viwili tofauti, kwanza Watanzania tunapaswa kuambiwa ukweli
1. Taarifa ya TRC inasema vichwa vipya na mabehewa mapya, lakini ukweli ni kuwa ni vichwa mitumba na mabehewa mitumba ya mwaka '1947'!.
2. Mkataba ni wa ukarabati na kutiwa nakshi nakshi kwa vichwa na mabehewa mitumba!, na sio kuundwa kwa vichwa na mabehewa mapya!.
3. Hakuna ubaya nchi kununua vichwa mitumba na mabehewa mitumba, kitu muhimu ni Watanzania tuelezwe ukweli!.
4. Jee hivyo vichwa viliundwa lini, wapi na vimetumika muda gani kabla sisi hatujauziwa?.
5. Mitumba hiyo imenunuliwa kwa bei gani na inakarabatiwa kwa bei gharama gani?.
5. Tufanyiwe comparative analysis, kama tungenunua vichwa vipya na mabehewa mapya, tungetumia gharama kiasi gani, compared na kununua vichwa mitumba na mabehewa mitumba, ili tujue tumeokoa fedha kiasi gani kwa kununua mitumba hiyo?.
6. Japo gharama za kununua vitu vipya ni juu ila maintance cost ni ndogo, unaweza kununua mitumba kwa bei poa kumbe ni mitumba choka mbaya, hivyo maintenance cost ikawa juu.
7. Sii wengi wanajua kazi ya CAG sio kutoa tuu zile ripoti za hesabu za serikali, CAG ni Mdhibiti na Mkaguzi, ufhibiti unafanywa kabla ya manunuzi, jee kulifanyika tathmini yoyote rail worthness report ya vichwa mabehewa hayo mitumba kabla hayajanunuliwa?. Then CAG atufanyie value for money audit, msikute mitumba hiyo tumepewa bure, huku watu wakipiga kubwa tunauziwa kwa bei ya mapya!.
8. Ukiingia mkataba wa manunuzi, mzigo ukanunuliwa, delivery ndio ikachelewa, huwezi kuvunja mkataba huo ukabaki salama, hivyo kesi ikifunguliwa, Tanzania tunashindwa hata kabla kesi haijaanza!.
9. Tulivinja mkataba wa Dowans, watu wakajiapisha "over my dead body", tulishitakiwa, tukashindwa, tukadaiwa tukasema hatulipi!, ukweli ni kuwa tumelipa kwa siri, Watanzania hatukuambiwa!.
10. Tulipo vunja mkataba wa Dowans, Zitto akashauri tuitaifishe mitambo ile, Wabunge wetu wakagoma kuwa Tanzania hatununui mitambo mitumba!.
11. Mitambo ile ikanunuliwa na Simbion, tukaingia nao mkataba ule ule wa Dowans tuliovunja, kwa gharama zile zile na tukawalipa!.
12. JPM alipoingia tukavunja mkataba wa Simbion, tukashitakiwa, tukashindwa, JPM akagoma kulipa!, ila baada tuu ya JPM kuitwa kule, huku nyuma, sio tuu tumelipa, bali pia tumeinunua ile mitambo kwa bei ya ajabu!, sasa mitambo ile tuliosema ni mtumba hatununui, sasa ni mali yetu na malipo yote yaliisha fanyika chap chap!, ila Watanzania hatuambiwi!.

Tuambiwe tuu ukweli!.
P
 
1669222314535.png




Nauliza tu, kwamba hivi haya mabehewa tunayoletewa toka Korea yana madirisha ya kufunguka, au yamefuata design za huko majuu ambako wao wana uwezo wa kuhakikisha air condition zinatumika na kufanya kazi wakati wote kwenye mabasi na matreni?

Isije tukaua watu kwa joto wakati tumeshindwa ku-mantain hizi air condition kwenye mabehewa, au labda safari kuahirishwa kwa kuwa air condition za mabehewa hazifanyi kazi. Nawaelewa sana Watanzania wenzangu, mambo ya maintance yanatupita kwa mbali sana, ndio maana hadi sasa mabasi yote yanayotumika nchini ni yale ya kufungua madirisha, tofauti na mabasi ya huko majuu.
 
Munataka muanze ingiria dirishani? Hewa inaingia kwa juu. Hayo madirisha kama ya ndege.
 
Mie nipo, hili suala la design ya madirisha nakuambia litakuja kuwa issue, labda kama yanafunguka. Hao watu walio pitisha design sidhani kama walifikiria hilo. Huenda walikuwa wanasiasa sio mainjinia. Yatakarabatiwa kabla hata hayajatumika.
 
Hapana.

Kama "mabehewa yanayokuja" muonekano wake ni sawa na hiyo picha iliyowekwa hapo, (picha #2), hayo yatakuwa siyo "mabehewa ya kawaida" hata kidogo!
Hata yale ya 'mete gauge' mbona yatakuwa ni bora zaidi kwa mwonekano wake kuliko haya!

Bado siamini kwamba hiyo picha ndiyo mabehewa yatakayotumika kwenye SGR.
hayo ndio yameletwa
 
Back
Top Bottom