Mwizukulu wa Buganda
Member
- Nov 19, 2024
- 94
- 307
Serikali imejikita kuhakikisha inapunguza bei ya mitungi ya gesi ya kupikia na kutoa ruzuku ya asilimia 20 ya mitungi hiyo Ikiwa ni sehemu ya kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa mwaka 2024-2034.
Naibu Waziri wa Nishati Judith Salvio Kapinga amesema hayo bungeni leo Januari 29 wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu Maryam Azan Mwinyi aliyetaka kujua mkakati wa serikali wa kupunguza bei ya gesi ya matumizi ya nyumbani.