Bei ya maharage Kenya ni 2861 Tsh/Kg huku Tz ni 4,200Tsh/Kg lakini wakenya wapo Barabarani huku watanzania tukipongezana miaka 2

Hili ni tatizo litokanalo na Mwenge wa Uhuru. Tambiko la Taifa
 
Hamna kitu kinanikera et kumpongeza mtu kwa kazi aliyoitaka mwenyewe kwa nguvu zote na bado asifanye yaliyotarajiwa alafu mkeshe mkisifia kisa ni utamaduni.... bladenfaka...
Kwani unapompongeza chama Kwa kufunga goli hiyo kazi hakuitaka mwenyewe? Wewe ukiona Huwa hupongezwi? Ulilazimishwa? Acha ujinga na chuki zisizo na msingi.
 
Njoo Chalinze kilo 4,200.
 
Nilitegemea utoke jf uwe Barabarani.kukiwasha kumbe ni wale wale nyumbu tuu.

Unategemea mtoto wa nani akaandamane wewe uwe unatoa updates?
 
Sio Kuporomoka ni msimu wa mavuno unaanza Kwa hiyo zitapanda Disemba
 
Mapinduzi hapo Mwananyamala?
 
60kshs ni Sawa na 1000tshs ,umepigaje hesabu Yako ,Ili ujue kwann wakenya wanaitika wito wa raila odinga ,ichukue hiyo bei ya Kenya harafu ichenji kwapesa ya Tanzania harafu uje na bandiko jipya hapa
 
Sijasoma kilichoandikwa ndani ya mada yenyewe, lakini kichwa cha mada kinajitosheleza kabisa.

Pongezi kwa ufundi wako wa kupanga maneno vizuri.
 
Bonge la point.
 
wamenunua Tanzania kwa bei ya juu na kuuza Kenya kwa bei chiniπŸ’ͺπŸ‡ΊπŸ‡¬πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‘
 
Utanisamehe kwa kukuita mwongo na hizo bei ulizoweka hapa. Naomba radhi kwa sababu sikutegemea nawe uwe sehemu ya upotoshaji.
 
Hiyo sio bei ya Tanzania nzima. Kiongozi
 
Na huu ndio ukweli sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…