Bei ya maharage Kenya ni 2861 Tsh/Kg huku Tz ni 4,200Tsh/Kg lakini wakenya wapo Barabarani huku watanzania tukipongezana miaka 2

Ukilinganisha mwenendo wa bei ya bidhaa na huduma 160 za Tanzania ambazo NBS inatumia kuangalia inflation.

Kwa vitu ivyo ivyo ukiangalia na Kenya si ajabu ukakuta Tanzania bei imepanda kwa bidhaa na huduma nyingi kushinda kwa majirani zetu.

Ajabu sisi tupo kwenye low single digit za inflation na majirani zetu wote inflation ni double digits. Bei ya kufunga umeme tu Tanzania imepanda kwa asilimia 1000% halafu eti national inflation ni 4.8% mwezi March.

Hakuna ata mtu mwenye kutaka kuwauliza hao NBS watoe hizo bidhaa na wenyewe wajionee hiyo 4.8% ya inflation wanaipataje.

Halafu wanatoka hadharani wanajigamba kabisa inflation ni low, kwa data ambazo obvious za kupikwa.
 
Kuna wanaoponda ila kupanda bei maharage ni mfano tu, hapa nazungumzia kupanda bei bidhaa kiujumla, pamoja na mambo mengine ya hovyo yanayoendelea kama migao ya umeme, maji n.k.
Nikishashiba sikumbuki Bei ya bidhaa tumbo kitu kingine Ila njaa ikiuma alafu mfuko hauna kitu lawama zote kwa mama
 
Emu hio inflation iweje kwa kiswahili kuna ngumbaru hawakuelewi unamaanisha nini
 
NIKO MOROGORO, BEI YA MAHARAGE NI 4000/KG,

ILA KUNA MINGENSE MINGINE INABISHA TU.

ILA NATAKA NIWAAMBIE SA100 AKIONDOKA KWENYE UTAWALA HATOAMINI ATAKACHOFANYIWA NA WALAMBA ASALI
 
Toka hapa na bei zako zakubumba mwanza bei ni 3200 ,2500 ya nyoko!?
 
Ni ngumu kuelewa hii lakini haya ni mambo ya kiuchumi zaidi.

Ukiambiwa gape la walio nacho na wasio nacho kenya na tanzania ni tofauti uelewe kwa namna hiyo.

Maisha ya masikini kenya ni makali sana ukilinganisha na TZ.
By the way mambo ya kupongeza ni uchawa.
 
Kenya unga kilo 3600 acha kusifia sifia majirani!! Kule njaa nikali
 
Mpaka hapo mtoa mada muongo mkoani maharage average price ni2500 halafu yeye kasema 4200 yaan impossible hata kama ni mjin daresalama
 
Nenda Kenya kanunie uje uuze Tz Fursa hiyo
 
Watu wachukue bei ya juu kabisa kufikiwa eneo lolote nchini (peak), hiyo ndiyo mjadala. Mara nyingi itakuwa kwenye miji au majiji yenye masoko na maduka ya tabaka mbali.
Akili ya watu wenye upeo mpana inawaza nchi nzima na wananchi wote kwa ujumla, siyo pale alipo yeye mwenyewe.
 
Kama mandamano ndiyo ufumbuzi, naomba yakisha hayo mandamano uje Tena hapa utueleze, namna bei ilivyopungua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…