Bei ya Petroli, Dizeli Oktoba sasa kitonga, sababu za kushuka zatajwa

Bei ya petroli na dizeli ya rejareja kwa Oktoba 2024 imeshuka nchini, ikilinganishwa na Septemba, huku sababu kadhaa zikitajwa, ikiwamo kushuka kwa gharama za soko la Uarabuni.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) inaonyesha bei za mafuta kuanzia leo Jumatano Oktoba 2, 2024 kwa yanayochukuliwa Bandari ya Dar es Salaam, Petroli imeshuka kutoka Sh 3,140 Septemba kwa lita moja hadi Sh 3,011 Oktoba, sawa na asilimia 4.1.
Pia, kwa petroli inayochukuliwa katika Bandari ya Tanga, lita moja imeshuka kutoka Sh3,141 Septemba hadi Sh3,016 Oktoba na kwa Bandari ya Mtwara pia imeshuka kutoka Sh3,142 Septemba hadi Sh3,016 Oktoba.

Kwa upande wa bei ya dizeli, taarifa ya Ewura inaeleza bidhaa hiyo inayopokewa Bandari ya Dar es Salaam bei yake imeshuka kutoka Sh3,011 Septemba hadi Sh2,846 Oktoba.

Soma: Petroli na dizeli zashuka bei soko la dunia
kitonga kivipi mkuu!
Nlijua imerudi bei 2000 na kitu kabla mama hajakabidhiwa mikoba
 
Tusubiri maumivu ya November
 
Back
Top Bottom