Bei ya vyakula vya mahoteli/migahawa ya njiani kwa wasafiri wa mabasi iangaliwe na mamlaka husika

Kweli hili jambo linakear sana. Kwa mfano, unapanda gari linalotoka Arusha/ Moshi bila kueleza wanasimama wapi kuchimba dawa, lakini akitokea abiria akaomba achimbe dawa dereva anagomba! Pia ukifika muda wa kula, unajikuta mnaingia LIVERPOOL penye huduma mbovu lakini kwa vile dereva na wasaidizi wake wanakula bure basi abiria wote mnakuwa hamna namna. Hili lilikuta nikiwa naenda TANGA basi lilisimama hapo LIVERPOOL kwa kweli chakula ni ghari alafu siyo standard kabisa. Ni vizuri abiria tukawa tunauliza mambo muhimu kama sehemu ya kuchimba dawa, kifungua kinywa au chakula lcha mchana ili abiria afanye uamuzi sahihi.
 
inabidi waziri aseme na hawa watu yaani chips kuku 7000 kuweni na huruma nakumbuka wakati Kilimanjaro motorway imefunguliwa bufee ilikua elfu sita halafu ni self service...... ila sa hivi tunahudumiwa japo bei ghali lakini mazingira mazuri na chakula kizuri
 
Ni kama umelazimishwa maana basi limesimama hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole shida sio viepe itakua ni nyama aka mishikaki na makachumbari kama uliweka
 
Na ukute ndio umekaa na pisi kali inabidi tu ujitutumue kula vya expensive
 
Sehemu 9, 10 ni pale panapoitwa LIVERPOOL labla ya Mombo. Chakula cha hapo ni bei ya juu lakini hakina ubora kabisa. Ni bora kweli Mamlaka husika ziwezekufuatilia maana kuna Watetzi wa Wasafiri, Wizara ya Afya, Mamlaka ya Chakula na Lishe. Tunaomba zifanyekazi kwa ajili ya haki za msafiri na usalama wa raia. Sasa kama mtu amekula chakula kibovu anataka kuharisha anakataliwa an konda, ni hatari kwa afya ya huyu mtu na abiria wengine iwapo atajizaidia ndani ya basi. Suppose ni Kipindupindu!
 
Niliwahi kula pale.
Wali nyama, maharage na mboga za majani 8000 wakati thamani yake haizidi 3000
Sent using Jamii Forums mobile app
 


🀣🀣🀣🀣🀣🀣
 
Umesema kweli. Bei ya chakula hapo ni shs 8,000. Afadhali kukata tiketi ya Shabiby ambao wanasimama kwenye mgahawa opposite na hoteli ya ABCπŸ˜€ Nafikiri tunapoelekea abiria tutakuwa tunasafiri na hotpot zetu zenye misosi
 
Mkuu hata kiswahili hujui kukiandika?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dawa ni kuwagomea tu.Beba vipande vyako vya kuku wa kukaanga unakula njiani
 
Salam kwenu wakuu...

Mimi naomba nijuzwe jambo kuhusu namna ya usimamizi wa hizi HOTEL ZA BARABARANI(Kiinglishi wanaita MOTEL)...

Ni kwamba serikali imezisahau ama?

Yaani zinajiendesha tu zenyewe zinavyotaka...

WANAUZA BIDHAA ZAO UTASEMA VYAKULA VYAO VYATOKA MBINGUNI...

CHIPS KAVU NA TUNYAMA TWA MISHIKAKI 7000/-

SODA ILE TAKE AWAY 2000...

Alafu wana mashine ya EFD Kama geresha tu...hakuna mtu anayepewa RISITI...Tujue kuna kodi yaenda serikalini...

Au tujue bei wanazouza vyakula na bidhaa zao ambazo ni bei za juu mno...tujue wazi kuwa hii ndio bei elekezi ya SERIKALI...

MBAYA NI WATU WASIOJALI AFYA ZA WATU...VYAKULA VINAVYOUZWA MARA NYINGI Chips Yai, HUWA ZIMEKAANGWA TAYARI, SASA HUWA ZINABAKI HATA SIKU 3 HADI 4...WANAPASHA MOTO...

SASA NA ILE KIMBIA KIMBIA YA BASI..."CHUKUA CHAKULA ULE KWENYE BASI", WANAJUA UTAPAMBANA TU HALI YAKO HUKO KWENYE BUS...ILA WENYEWE HELA YAO IMEINGIA...unakuta chips yai yavutika kama mlenda....

NA HII NIMEIONA KWA MOTELS ZA DODOMA...

Hebu serikali iziangalie sana hizi hotels, KUSAFIRI isiwe adhabu jamani...yaani wanakula kwa advantage ya safari...tunauziana kwa bei ya watalii kama wanavyouza MAEMBE WAZANZIBAR...UNAWEZA KUTA DODO LA 500 MPAKA 700, WANAKWAMBIA ETY DOLLAR MBILI...

NDIO MAANA HALI INAZIDI KUWA NGUMU...

TUNAKANDAMIZANA WENYEWE KWA WENYEWE...

Naomba kuwasilisha...hii sekta imepuuzwa au imesahaulika?
 
CCM ndio chanzo cha yote haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…