Bei ya vyakula vya mahoteli/migahawa ya njiani kwa wasafiri wa mabasi iangaliwe na mamlaka husika

Mimi hata sasa, tukusafiri na familia usiku tunaandaa viazi, ndizi za kukaanga na kuku au nyama, matunda, Juice na maji. Weka kwa foil then ndani ya food container... Cheap, high quality na hakuna kusumbuana....
Hapa tutarudi enzi za miaka ya 80's, nakumbuka tukiwa tunasafiri na bi-mkubwa basi lazima apike chakula cha safari kwenye kimfuko na naironi then kinatunzwa kwenye kikapu... mzee ukijisikia njaa tu bi-mkubwa nafungua kifuko acha kabisa.
 
Bei zimepanda sana kwa mgano kaskazini no kati Sh. 7000 na 8000 Rock Hill na wengine.. SUMATRA na wadau wa huduma na haki za wasafiri watusaidie.. Na madereva wa mabasi walazimishwa wasipeleke abiria maeneo ya kwenda kuwafilisi..
 
Unaanzaje kumshambulia labda ni mgonjwa... Lakini pia mabus nowadays wana tabia ya hovyo sana eti Bus ikitoka Dar kuchimba dawa ni Morogoro, next Iringa, sasa hawajui kwamba kuna baadhi ya watu ni wagonjwa...
[emoji16][emoji16][emoji16]raia hawakumshambulia kweli?
 
Magufuli amebana sana hela!
Pole mkuu
Halina uhusiano na Magufuli. Zamani mabasi yalikuwa yanasimama stendi na wasafiri wanachagua wale wapi na wale nini. Stendi zilikuwa na hotel nyingi na za bei tofauti. Huu ujinga wa mtu kwenda kujenga hotel porini halafu anapanga na wenye mabasi au madereva wasimame kwenye hotel yake ambayo amepanga bei anayoitaka yeye ni ufisadi. Kunakuwa hamna competition na wenye hotel wananyanyasa wasafiri wanavyotaka kwa sababu hawana jinsi nyingine.
 
Mimi hata sasa, tukusafiri na familia usiku tunaandaa viazi, ndizi za kukaanga na kuku au nyama, matunda, Juice na maji. Weka kwa foil then ndani ya food container... Cheap, high quality na hakuna kusumbuana....
kaka kama mnasafiri ki famiia unaweza kujikuta unateketeza karibia laki nzima kisa eti msosi tu wa njiani.
 
Kwa kweli inakera sana, safari inakuwa chungu wakati kwa wenzetu safari ni adventure.
Mimi siku hizi tukifika kwenye hizo hoteli sinunui chochote zaidi ya kuvuta sigara na kunyoosha miguu.(Ref.Nangulukulu e.t.c)
Mkuu tatizo ni kuwa wasafiri wengine wanakuwa na watoto au wagonjwa au wametoka muda mbaya na hawajala chochote. Suluhisho ni serikali kuingia kati na kulazimisha mabasi yasimame stendi kwa muda mrefu. Wapige marufuku kabisa mabasi kusimama kwenye hotel za vichakani.
 
Unaanzaje kumshambulia labda ni mgonjwa... Lakini pia mabus nowadays wana tabia ya hovyo sana eti Bus ikitoka Dar kuchimba dawa ni Morogoro, next Iringa, sasa hawajui kwamba kuna baadhi ya watu ni wagonjwa...
mgonjwa ndo ajinyee jaman tena mtu mzima[emoji849]

Ila hyo ya kuchimba dawa,Moro,iringa me mbona naona iko fair kabisa..au ilipaswa iwe kila baada ya kilometa kumi?
 
Aiseeee kwenye maisha ukitaka ukwame fanya kitu kwa kuhofia au kujilinganisha na wengine... Nyama buchani 7000 kg, nusu 3500 alfajiri wife anakaanga na ndizi 2 au viazi 4, funga kwa foil weka kwa food container.... Ndizi mtaani 100, embe 300, Azam juice kubwa 3000....
Wengine hua wananunua vyakula kama showoff , watu wajue kanunua kuku chipsi na mishkaki, kwahio lazima aende na wakati kwanini ale mkate na wengine age yake wale kuku na chipsi, peer pressure inachangia
 
Mmmmh Dar to Mwanza tulitoka Ubungo saa 12 asubuhi kufika saa 5 usiku... Hiyo sasa ni zaidi ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani...
Safari za Mwanza huwa sili kitu. Maana tumbo langu ni dakika tu linadai kutoa kilichoingia. Imesababisha nianze tumia loperamide kila safari ili nisiendechoo hata liume vipi
 
Hapo Nangurukuru niliacha kununua, sio kwamba sikuwa na hela ila nilikwazika na sikutaka kujialaumu, soda 2000 takeaway, samaki mhhhhh chakula sasa ndio balaa gharama kubwa. Ifike hatua sasa tujiongeze tu kuonesha msimamo, hakuna kununua acheni.
Halafu hii biashara sio huru kwa sababu madereva na makonda(wa gari sio wa RC) wanacheza dili na wenye mahoteli na wengine makampuni ya mabasi yana hoteli zao kwahiyo wanasimama hapo tu kwahiyo kama una njaa inakulazimu kura na kwa sababu wapo wenyewe basi wanauza kwa bei wanayotaka ambayo sio rafiki kabisa.
Sasa hii sio nguvu ya soko kwa sababu hata ukiweka hoteli zako za bei ya kawaida kabisa basi hao madereva hawaji hapo kwahiyo hautafanya biashara.
Tujiandae mapema ili kuwaeouka hao wezi wakubwa. Halafu hivi vyakula sio salama sana, andaa nyama yako yako na kinywaji basi kula njiani au nunua biskuti kula
 
Unafunga taiti? Subiri kwanza,we ni jinsia gan
 
Mm nakula mkate tu au biskuti na soda...it's what I can afford...

Kuna siku nilkuwa naenda Moshi bhn...Kuna kimgahawa Kiko porini hcho wali nyama au chipsi na kakidali kadogo ka mzoga wa broila n 7000....
Nilichoka yaan
 
kuna moja iko apa babati unapoingia njia ya kondoa asee zile bei ni hatari ukizangatia na ratio ya chakuoa plus kutoiva....serikali inapaswa iliangalie kwa umakini
 
Kusafiri na msosi tena!???! Hapana. Bora nisile tu safarini.
 
kitu pekee ambacho huwa kinanipa shida kwenye safari ni mkojo tu... na hiyo ni kama tu safari yangu inaanzia sehemu ambako kuna baridi... labda njombe to dar au mbeya to dar...

Huwa sina tabia ya kula vyakula vilivyopikwa njiani...
 
Tatizo pale panakuwa hapana option ya wewe kwenda kuchagua hivyo lazima ule manaa no sehemu moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…