Bei ya vyakula vya mahoteli/migahawa ya njiani kwa wasafiri wa mabasi iangaliwe na mamlaka husika

Pole Sana mdau, hapo Liverpool usirudie tena kula chochote ni wachafu sana.
 
Kiukweli kwanza nikupongeze kwa kulitoa hili ambalo wengi tumekuwa tukiumia na kukerwa nalo lakini bado tukakaa kimya pasipo kulisemea .
Lakini pia nikuunge mkono bei hizi haziendani na huduma inayotolewa.kifupi tunalazimishwa na mbaya zaidi mabasi mengi mnapewa na muda mfupi kupata huduma hiyo ya chakula.Hii maana yake nini,kwanza huna sehemu mbadala ya kupata huduma,pili unabananishwa na muda, mwisho wa siku unalazimika kuchukua "TAKE AWAY" kama option ya kuendana na mazingira hayo yaliyoandaliwa kisayansi...hapo sasa ndio utakutana na lugha ya "kama una kula hapa hapa 5,000/=AU kama TAKE AWAY 6,000/=
Hivyo basi naungana na mtoa mada kwamba mamlaka husika ziliangalie hili suala kwa jicho la kipekee kabisa.
 
Sisi wazambia tukiwa tunaenda dar.huwa tunafungasha bievarage ya kutosha pale tunduma
Njia nzima sisi ni kula tu kuku tukifika All Jazeera ama Comfort ni kuvuta cigarette na kuñywa konyagi,prince,feldo,win,jambo gin,ama verve with in 15 minutes vibe kwa hewa
 
Hahaha pole sanaaa[emoji1787]
Mimi hiyo ya kuhara haijawahi kunikuta,ila watu wana moyo
Kule kasuru,uvinza ukienda ,mishkaki inauzwa kwenye stand yenye vumbi na watu wanakula tu
 
Hapa tutarudi enzi za miaka ya 80's, nakumbuka tukiwa tunasafiri na bi-mkubwa ilikuwa lazima apike chakula cha safari kwenye kimfuko cha naironi then kinatunzwa kwenye kikapu... mzee ukijisikia njaa tu bi-mkubwa nafungua kifuko acha kabisa.
Mimi mpaka leo nikisafiri na maza,anapika chips na nyama ya kukaanga
Huko njiani ni soda tu
 
Tatizo ni uvivu uliosheheni ndani ya familia zetu; ukisafiri na wazungu kwenye hayo mabasi wanakuwa wamejiandaa kwa safari na bite zao lakini sisi wabongo hata "Apple" hatuchukui
 
Kama leo pale karibu ya msata kitumbua hiki hiki cha mama K mtaani 200 pale buku, sambusa ya bi kiboga ya jero pale buku. Tulivyofika Mombo sasa, yule mwarabu nyama choma finyango 8 buku 7. Kwa kweli wasafiri tunanyooshwa.
 
Mkuu nimesafiri sana kuanzia njia ya mwanza-dar, dar-mtwara mpk mbeya uko naweza sema hoteli mbovu kupita zote ni Nangurukuru asee nliwai fikilia niamzishe hotel maeneo ayo kwa kuweka Hotel na huduma zote za muhimu sema nlipigwa bit na kutishiwa mambo ya kuuliwa kwa ulozi
Kilwa ni moto kwa mambo ya Ndumba
Pale hotelini soda take away 2000 chips kavu mshikaki mmoja 5000
Wahudumu wachafu chafu, samaki wabovu wanafunza na wanalala, chakula kingine kibaya hakina ladha kabisa, viazi avimenywi vikaisha maganda asee bale ni balaa nliapia sitokuja kula pale so nkitoka zangu nyumbn uwa nafungasha kabisa mahala ambapo nakua free kula ni hotel za Kilimanjaro express tu maana kuchimba dawa tu 30dk chakula uwa napata pale chips nyama ya mbuzi elfu 7000 yangu naenjoy na soda au maji nliyopewa kwenye gari
 
Hata soda njiani sio za kuziamini, babati ilishawahi kuuziwa sprite imepita expire date miezi minne nyuma, wakati huo basi limeshatoka stand
 
Kuna mgahawa mmoja maeneo ya mayoni asee nilikuwanatoka iringa, msosi kidogo afu umepoa bei sasa kaki yako mkooni asee, anzia hapo mi ni maji na keki na fegi basi
 
Tumia akili kutatua tatizo hili,
Tunasoma ili tusaidie jamii inayotuzunguka sio binafsi. mimi nimesafiri na mama mmoja anamtoto mdogo anamlisha karanga njia nzima na tulipofika eneo la kupata chakula alishindwa kujihudumia ikabidi majirani tumchangie ampatie mtoto chakula. So nikiandika hapa si kwasababu yangu peke yangu, ni kwa ajili ya maslahi mapana ya jamii haswa maskini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…