Bei ya vyakula vya mahoteli/migahawa ya njiani kwa wasafiri wa mabasi iangaliwe na mamlaka husika

Bei ya vyakula vya mahoteli/migahawa ya njiani kwa wasafiri wa mabasi iangaliwe na mamlaka husika

Mimi nalia na vyoo tu hasa njia ya kati, mabasi yanapaki hotel wanazotaka kisa wao wanakula bure, hawaangalii facility zingine zikoje, vyoo ni vichafu sana, juzi juzi hapa tulipelekwa kwenye hotel fulani vyooni hakuna hata maji. Wenye mahotel ya kulisha abiria tafadhali boresheni huduma za maliwato pia ni muhimu sana kwa afya za wasafiri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu watumie fursa kufungua migahawa ya bei nafuu
 
Muwe mnaaadaa vitu vyenu nyunbani..
Kuku ukikaanga vizuri na biazi au ndizi unafunga vizuri kwny take away njiani unajichena tu...
Badala ya kulipa efu kumi kula msosi mbovu hyo efu 10 kitaa unandaa kuku mzima kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa muda mrefu nimekuwa nikikerwa na hili jambo.

Bei ya chakula cha hizi hoteli/migahawa ya njiani kwa wasafiri haiendani na huduma wanayopewa lakini naona mamlaka husika zimekaa kimya. Na hili naomba lisichanganywe na suala la wakulima kujipangia bei, msafiri sio mkulima ni mtu anayekuwa hana option maana pengine amesafiri masaa kumi na mbili au ishirini bila kuonja kitu na analazimishwa anunue chankula kwa bei ya juu. Au anaenda hospitali kupeleka mgonjwa.

Kiuhalisia sahani ya wali nyama ni 1500 - 2000 lakini kwenye hiyo migahawa wali nyama wanauza 5000 - 6000. Mbaya zaidi vile vidada vihudumu vinanyodo utafikiri vinahudumia hoteli ya nyota tano kumbe mgahawa wa barabarani tena kwa wasafiri (ref: nangurukuru). Ukiviambia dada ongeza kidogo basi ili nishibe kanakukata jicho utafirikiri umetoa mawe kumbe umetoa 6000.

Wanaosafiri wengine ni wagonjwa, watu wa vijijini na wengine hawajiwezi kabisa, unapomlazimisha mtu kuwa tutachimba dawa hoteli fulani na kupata chakula hapo ni ukiukwaji wa haki za wasafiri. Kwanini mamlaka wasimoderate na kucontrol hili suala? ikiwezekana sehemu ya kuchimba dawa ijitegemee na sehemu ya kula ijitegemee ili hao watoa huduma wasiwalipishe watu bei kubwa kisa umechimba dawa kwao.

Madereva na makondacta wao huwa hawalipii hiki chakula kwasababu ni deal kwa mwenye hicho kihoteli. hii ni ajabu sana, ndio maana inapelekea hawa madereva wanawapeleka abiria sehemu ambayo mwisho wa siku watalazimika kulipia hata kama hawataki.

Naomba mamlaka husika waaanze na Nangurukuru, Singida, Shinyanga, Morogoro, Alj jazeera na sehemu zingine ambazo mimi sijafanikiwa kupita huko kwasababu inakera sana na ni ukiukwaji wa haki za wasafiri kabisa kuwalazimisha kupata huduma wasipopenda halafu mbaya zaidi kwa bei ya juuu kuliko uhalisia.

Bei ya choo cha kulipia inajulikana ni 300, Bei ya wali maharage inajulikana 1500-200, bei ya wali kuku inajulikana ni 3000-4000, bei ya kile kitake away inajulikana kuwa ni 300. Iweje tutozwe bei zisizoendana na uhalisia?

Wakuu wa nchi wao husafiri na private mara nyingi kwahiyo hii inweza isiwe na mashiko sana kwao, lakini kiuhalisia vyombo vya dola na mamalaka za miji na halimashauri ambako huduma hizi hutolewa inabidi walichukulie serious.

Wakuu Nawasilisha, naomba ndugu zangu tusaidiane kupinga huu unyanyasaji kwa abiria.

Pia soma

Mwenzako niliwahi kimbia pale njia panda ya machame wanapaita kwa dar xpress nikaenda kwa maama ntilie Jilani tu nikaumega kwa 1000 badala ya 6000
 
Tanzania ukikata tiketi ya basi unasafiri kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine unageuka kua mtejwa wa hoteli ya mweye basi by default. Dereva ndie mwenye uamuzi mtakula hoteli gani.

Swali langu, kwa nini hakuna utaratibu wa abiria kua na uhuru wa kuchagua hoteli watakayokula kuliko kulazimishwa kula hoteli ambayo dereva anaamua.

Kwanza hii itasababisha bei ya chakula kwenye hizi hoteli za njiani kupungua kuliko ilivyo sasa, mnatembezwa masaa 8, mnafikishwa kwenye hoteli ambapo abiria unakua huna namna una njaa unalazimika kula, chakula kibovu bei ghali.

Basi ziwe na utaratibu wa kuwajulisha abiria wanaotegemea kusafiri na basi yao kua watakula hoteli flani ili mtu awe na taarifa kamili kabla hajaamua kusafiri na hiyo basi au lah, ama abiria waee na uhuru wa kuamua watakula hoteli gani.

Sumatra, wizara ya afya waliangalie hili.
 
me naona kila abiria akichagua hotel anayotaka kula itakua majanga. Mtachukua muda mrefu sana kufika.

Unless ungesema kila basi unapikata tiketi wawe wanasema tunaondoka Ubungo saa 12 Asubuhi, saa 4 tutapata chai sehemu fulani, saa 8 tutapata lunch sehemu fulani, saa 12 tutachimba dawa sehemu fulani, saa 6 usiku tutawasili Mwanza.
 
Yes wenye mahoteli wanashirikiana na madereva kulifanya hili,na vile vile tunachangiwa na mifumo mibovu ya miundo mbinu yetu,hizi barabara zetu kuu bado sana,sielewi why umbali wa Dar to Arusha +600kms lazima bus lisimame kituo Fulani kwa chakula?maana bus ikiondoka pale ubungo 6am tunategemea by 2pm liwe limeshaingia Arusha,sawa na Dodoma,Tanga,Iringa (mabus yote haya yana yalitakiwa yasafiri kutoka Dar ndani ya masaa 8) na why mubus hayasafiri usiku hata baada ya Lugola kuja na lile tangazo lake la majambazi?,kipindi nchi ina heshima na adabu Scandanavian bus inaondoka Dar saa 6am,Ilula mnaingia 6mchana,1600 mpo border na mnavuka !!!
 
hivi itakuja kutokea kampuni ya usafirishaji abiria kama Scandnavia
 
Tanzania ukikata tiketi ya basi unasafiri kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine unageuka kua mtejwa wa hoteli ya mweye basi by default. Dereva ndie mwenye uamuzi mtakula hoteli gani.

Swali langu, kwa nini hakuna utaratibu wa abiria kua na uhuru wa kuchagua hoteli watakayokula kuliko kulazimishwa kula hoteli ambayo dereva anaamua.

Kwanza hii itasababisha bei ya chakula kwenye hizi hoteli za njiani kupungua kuliko ilivyo sasa, mnatembezwa masaa 8, mnafikishwa kwenye hoteli ambapo abiria unakua huna namna una njaa unalazimika kula, chakula kibovu bei ghali.

Basi ziwe na utaratibu wa kuwajulisha abiria wanaotegemea kusafiri na basi yao kua watakula hoteli flani ili mtu awe na taarifa kamili kabla hajaamua kusafiri na hiyo basi au lah, ama abiria waee na uhuru wa kuamua watakula hoteli gani.

Sumatra, wizara ya afya waliangalie hili.
Kwahiyo sasa mtachagua wangapi ndani ya hilo bus ili dereva awasikilize

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hivi itakuja kutokea kampuni ya usafirishaji abiria kama Scandnavia
yes/no inategemea mambo mengi including uchumi wa nchi,mwelekeo wetu wa kisiasa je ni rafiki kwa wawekezaji,uboreshaji wa barabara zetu,why Intercape ichukue 16hrs kusafiri 1400kms kati ya widhoek na katima mulilo,wakati mabus yetu yanatumia 12hrs kusafiri umbali wa 600kms kati ya Dar na Iringa.ni crazy
 
Wenye mabasi nao wazembe tu,

Kama wanaweza kutoa biskut na maji kwa nn wasianzishe huduma ya chakula ndani ya gari?

Waanzishe tutalipa tu, ila msosi uwe mzuri wali nazi[emoji119][emoji23]

Sato[emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mfano hao ABC BUS mwenye hiyo kampuni ana hotel yake inaitwa cath hotel, ipo dar, moro na dodoma ukipanda hili gari lazima mkale kwenye hiyo hotel yake ya morogoro (mpya) na vitu ni bei ghali.. tumbua tu ni 1000 kimoja jamani[emoji30] services wako vizuri gari zake zote ni luxury unaenjoy shida ndio hiyo tangu afungue hiyo hotel moro aisee[emoji1430] kula ni hapo na vyakula ni very expensive na ni vya kawaida tu!!!
 
Back
Top Bottom