Bei ya vyakula vya mahoteli/migahawa ya njiani kwa wasafiri wa mabasi iangaliwe na mamlaka husika

Bei ya vyakula vya mahoteli/migahawa ya njiani kwa wasafiri wa mabasi iangaliwe na mamlaka husika

Hata niende mwanza huoni kufakamia michakula ni mwendo wa ndizi mbivu na matunda ya maji maji ,na
 
Logic yakuuza bei juu ni nini? Hapo ndio pamsingi.. Haiwezekani chakula chao kikawa bei Mara mbili Au tatu ukilinganisha na maeneo ya mijini.. Wanatumia advantage ya bus kusimama Hapo Tu wanajua huwezi pata chakula sehemu nyingine Yeyote lazima ule Hapo... Hii si Sawa. Serikali iingilie Kati hili suala kuweka hata bei elekezi ya vyakula njiani...
 
Kwa muda mrefu nimekuwa nikikerwa na hili jambo.

Bei ya chakula cha hizi hoteli/migahawa ya njiani kwa wasafiri haiendani na huduma wanayopewa lakini naona mamlaka husika zimekaa kimya...
soko huliaa, dawa hapo si kununua chakula chao jiandae tangu mwanzo wa safari kama walivyokuwa wakifanya wazee wetu miaka ya nyuma.

suala la haja hapo ndio shida. hoteli hizo kwanza wanakuwa na maunganiko na watu wa mabasi .hivyo usipojiandaa utakuta mnasimamishwa kwenye hoteli ambayo wao wanakula bure , ILI UEPUKANE NA HII SHIDA TUMIA ILE METHALI MSAFIRI KAFIRI.
 
Makampuni ya mabasi angalieni bei zenu za vyakula kwa wasafiri, au ikiwezekana wekeni vituo vya chakula sehemu za center ili watu wawe na uchaguzi wanakula nini kulingana na bajeti zao. Mtu unakuta eti andazi la 500 unauziwa 2000, soda ya 500 unauziwa 1000, chips ya juzi imekakamaa eti 3500, na vingine vingi. Yani kila kitu bei umiza. Mjitathmini.
 
Beba chakula chako nyumbani
 
Beba chakula chako nyumbani
Na vipi hatokei nyumbani?

Yaani mtu analalamikia ulanguzi wewe unaona suluhisho kubeba chakula, sasa ulanguzi ukifanyika kwenye cement, sukari nk vyote hivyo atangeneza vya kwake?
 
Mimi navyosafiri kama sina hela huwa naoda nyama kitimoto kilo nzima nakula kwenye basi mdogo mdogo mpaka safari inaisha
 
buffet 8,ooo/= - 10,ooo/= barabara ya DSM - Tanga - Moshi
 
Opportunity Mtu aanzishe route yenye Chakula cha Bei Nafuu....

"Opportunities Multiply as they are Seized" Sun Tzu
 
Me ndio maana sipendagi kula njiani na uwe na bahati mbaya wali wenyewe uwekwe amila
 
Mie sili chips safarini, nilishawahi kupatwa na masahibu. Nilitoka Moshi kwenda Dar, tulivyofika Mombo tukaingia kula hoteli inaitwa Liverpool, nikala viwepe na mishikaki. Uwiiiiii yaani hata hatujafika mbali, tumbo likaanza kuuma, mharo unataka kuchomoza.

Nikawaza, nikimwambia konda nataka "kuchimba dawa" atasema hilo zoezi ilikuwa lifanyike hotelini tulipokula. Basi bwana akili ikaja ya ziada, nikamwendea konda, nikamdanganya kuwa NIMEANZA KU BLEED GHAFLA hivyo wasimamishe gari nikajisetiri, hahahaha, konda kusikia hivyo akamwambia dreva, gari ikasimama nikaenda kwenye hoteli mshenzi mshenzi, nikahariiiiiiishaaaaaa mpaka basi!
Hahaha
 
nilikuwa natokea dodoma kuja dsm nimepanda shabiby tukaingia hotel pale msavu ..dah yaliyonikuta nilikumbuka kiepe cha dsm....niliwekewa viazi pices 8 na mayai mawili bei 4500/= nilichoka kabisa...kusema kweli nilighafirika sana lakni ndo ilikuwa hamna namna tena
 
Mie sili chips safarini, nilishawahi kupatwa na masahibu. Nilitoka Moshi kwenda Dar, tulivyofika Mombo tukaingia kula hoteli inaitwa Liverpool, nikala viwepe na mishikaki. Uwiiiiii yaani hata hatujafika mbali, tumbo likaanza kuuma, mharo unataka kuchomoza.

Nikawaza, nikimwambia konda nataka "kuchimba dawa" atasema hilo zoezi ilikuwa lifanyike hotelini tulipokula. Basi bwana akili ikaja ya ziada, nikamwendea konda, nikamdanganya kuwa NIMEANZA KU BLEED GHAFLA hivyo wasimamishe gari nikajisetiri, hahahaha, konda kusikia hivyo akamwambia dreva, gari ikasimama nikaenda kwenye hoteli mshenzi mshenzi, nikahariiiiiiishaaaaaa mpaka basi!
[emoji23][emoji23]pole. Ila ni mabasi gani hayo siku hizi yanakula liverpool

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom