TANZIA Beki Ally Mtoni Sonso afariki dunia, amewahi kuichezea Taifa Stars na klabu za Yanga, Kagera Sugar, Lipuli

TANZIA Beki Ally Mtoni Sonso afariki dunia, amewahi kuichezea Taifa Stars na klabu za Yanga, Kagera Sugar, Lipuli

Daah sonso pumzika kamanda uliyewahi kututumikia wananchi .

Anyway majeraha ya mguu yamepelekea kifo au kuna kingine kati kati hapa..
 
Majeraha ya mguu inawezekana kabisa kusababisha kifo
Kuna jamaa nilikuwa nafanya naye kazi sehemu fulani aligongwa gari akavunjika mguu, hospital wakashauri akatwe mguu. Ndugu wakagoma, wakampeleka kwa mganga aliyekuwa anaaminika kwa kuunga mifupa kwa njia za asili
Haikuwezekana. Baadaye wakamrudisha hospital mguu ukiwa umeharibika sana haikuchukua muda akafariki
 
Pumzika kwa amani Ali Mtoni Sonso. Umeondoka ukiwa bado ni kijana mdogo! Halika umeacha pengo kubwA sana kwa familia yako, na Taifa kwa ujumla.
 
Beki wa KMC, Ally Sonso amefariki dunia leo katika Hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa akisumbuliwa na jeraha la mguu.

Marehemu enzi za uhai wake aliwahi kuchezea timu za Yanga, Lipuli, Kagera Sugar na Ruvu Shooting.

View attachment 2116314
Haiingii akiliii...mtu amecheza mechi za hivi karibuni....majerehaa ya mguu wapi na wapi? toeni taarifa kamili
 
Matukio kama haya yawakumbushe wachezaji wakate bima ya matibabu manake nimesikia Ally Sonso R.I.P alikua akisumbuliwa na mguu akachelewa kwenda hospitali.
 
apumzike kwa amani alikuwa na beki nzuri wakati yuko na wananchi
 
May his soul fly high.
Dogo alikuwa anaujua sana
 
Huo ugomjwa matibabu yake ni ya asili zaidi ukipelekwa hospitari ni mara chache kupona mgonjwa anaishia kufa umewaimpata rafiki yangu alitibiwa kwa dawa za asili atimaye alipona
 
Back
Top Bottom