Ben Saanane: Ninatishwa kuuawa kwa kuikosoa Serikali

Kwa nini hiyo namba ilipotezewa hivyo?! Siyo ajabu walishaitupa, wakafanya mpango akapewa mwingine kutoka huko madongo-kuinama.....
Halafu ati kuna watu na akili zao timamu wanawaunga mkono hao wauaji!
 
Ila hivi vyama vingi wangefutaga tu Ben saanane na IQ yote ile pamoja na elimu kubwa aliyokuwa nayo yote inamalizwa njiani kisa tu kutofautiana mitazamo mbona hao waliotuletea demokrasia haya hawayafanyi ila sisi tuliopokea ndio tunajifanya tuna mahaba sana na vyama vyetu hadi kuua wengine kwani hata saanane alikuwa na madhara gani kiusalama kuzidi wale wauza madawa,majangili,majizi ya ESCROW EPA na makinikia kiasi afe kikatili hivi na hakuna aliyechukuliwa hatua

Mwanzoni nilifikiri masihara ila sahivi nahitaji kuamini kuwa sitowahi kumuona ben saanane tena akiwa hai wala maiti so sad ila kitu kimoja tufahamu kuwa siasa zinapita na kuna maisha baada ya kifo wanaofanya haya wajiulize wataenda kujibu nini siku wakifika mbele za Mungu???

Mimi ningeshauri wapinzani wapeleke muswada bungeni wafute vyama vyote wajiunge CCM maana...... Dah niishie hapa tu inauma sana

Cc Salary Slip Zitto Erythrocyte
 
Huyu ben saa nane muongo kama viongozi wake wanataka kuanza kama enzi za akina zitto akiwa chadema yeye mwenyewe ben walikuwa wanajiteka halafu wanasema wametekwa.
[emoji850][emoji850][emoji850][emoji850][emoji850][emoji867][emoji867][emoji867][emoji867]
 
Meseji hizi nadhani zilitoka CDM penyewe wakiwa na mission ya kumaliza Ben
 
Mungu akuweke mahali salama ndugu yetu, aidha uko hai au la
 
Amen!
 
sikuwa namfuatilia huyu jamaa Ben Saanane lakini nilishangaa kila nikipita kununua gazeti naona kupotea kwa Ben saanane.Nimeamini kuna watu wakiamua kukuwinda huwezi vuka hata umbali wa kiwanja,,ukifuatilia uzi huu na wachangiaji unaweza pata picha kuwa kuna waliokuwa wanaelewa ambacho kingempata Ben Saanane na walianza kumuonya mapema,,achilia mbali waliokuwa wanamwona mpuuzi;Kama kuna sehemu watu wenye ajenda kama za Ben wanafichwa,basi huyu Mtanzania atakuwa hai lakini kwenye mateso yasiyoelezeka,lakini kama alishazimisha jumla apumzike kwa amani,hata watesi wake watamkuta huko ahera.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…