Benard Membe: Musiba hasimami tena na kujifanya yeye ni Mungu Mtu. Huko uliko naomba hela zangu

Benard Membe: Musiba hasimami tena na kujifanya yeye ni Mungu Mtu. Huko uliko naomba hela zangu

Hizi hukumu za mfululizo zinazomkabili Cyprian Musiba kutoka kwa wanaccm wenzake hazina afya kwa chama.

Enzi za Mwalimu Nyerere huyu Musiba na Membe au na Fatma wangeitwa mbele ya vikao vya maadili vya chama na kusikilizwa na Uamuzi au Suluhu kupatikana

Ni aibu kubwa kuthibitishiwa na mahakama kuwa CCM ina watu wahuni wahuni wasioheshimu wazee wetu.

Kumtukana Membe au Kinana ndani ya chama ni ushenzi uliopitiliza.

Na nyie vijana mliobaki mjifunze kuheshimu waliowatangulia.

Maendeleo hayana vyama!
 
Mzee muoe tu musiba awe mke wa pili kawadhalilisha sana kina Kinana..Hakuna mzee humble na msikivu kama Kinana niliumia sana alivyodhalilishwa
 
Mwenye namba ya Membe anipe nimsisitize asisamehe deni by hook or by crook
 
Hizi hukumu za mfululizo zinazomkabili Cyprian Musiba kutoka kwa wanaccm wenzake hazina afya kwa chama...
Wakati akitukana hao watu, chama (CCM) hakikumsikia? Kwa nini uone kwamba ingekua busara chama kuwasuluhisha wakati chama hicho kilikua kinamsikia akitukana watu tena kwa majigambo makubwa.

Nadhani labda hoja yako ingekua kwamba, "wakati wa Nyerere hakuna mtu kama Musiba angeweza kuvumiliwa ndani ya chama", kwa nini ukae unasubiri kusuluhisha watu dhidi ya mtu mhuni kama Musiba!?

Pale tu alipoanza kuwachafua watu kwa jina la chama, alitakiwa kupata haki yake. Sababu za Musiba kuachwa achafue watu unazijua.
 
Tunazingatia alphabet. Bernard alipwe then Fatuma

Kama mnazingatia alphabet then atalipwa Anna [mama Mbona] kwanza halafu Benard and then Shangazi Fatma!

Akishindwa kulipa, pitisheni bakuri watu watachanga tumfunge jela mpaka atakapolipa!!
 
Enzi za Mwalimu Nyerere huyu Musiba na Membe au na Fatma wangeitwa mbele ya vikao vya maadili vya chama na kusikilizwa na Uamuzi au Suluhu kupatikana
Na wakati wa Nyerere mtu kama Musiba asingelitokea, mtu mavi kama yule akasimama kuwatukana wenzake. Kwanza nafasi kweye chama angeliitoa wapi? Labda kufagia ofisi, siyo kusema lolote...
 
Unajidanganya! Deni linafunga. Unaweza kufungwa as civil prisoner kwa gharama za anaekudai mpaka utakapolipa deni.
Kabisa.....na lazima ataenda ndani....waliotukanwa ni wengi...wanaweza kuchanga mtu akafungwa hata miaka mitano
 
Huku membe,kule shangazi na mama Tibaijuka.Ila Membe na shangazi wangemwacha kwanza mama Tibaijuka avute mil 80 zake alafu wacheki upepo,kama bado ataendelea kupumua Membe amkandamize then shangazi ammalizie.
 
Musiba itabidi aanze kudanga sasa atapata wapi hizo mapesa au ambetie Man utd.
 
“Niwaambie Watanzania wenzangu hakuna Mtanzania awe Ndovu au sisimizi mwenye kusimama juu ya sheria hakuna aliye juu ya sheria, ukimdhalilisha mwenzako...
Bao la kisigino dakika ya 89!
 
Mzee Membe kumbuka pia kwamba deni kalifungi.
Nani kakudanganya Deni linafunga njoo unikope mimi kisha uniambue Maneno hayo nitakulipia Magereza Gharama zote ili Mradi nikufunge tena nitakuchagulia na Gereza
 
Mdharirishaji mwingine ni "power kaaya"!

Kijana miaka 31 unamtongoza Mama mwenye miaka 60, huu ni udhalilishaji wa kijinsia!!

Nasubiri kusikia kutoka kwa Rais mwenye ngonjera ya jinsia ya kike atasemaje kuhusu Power kaaya!!
POWER KAAYA ni kama Alimtongoza Mama wa Kumzaa mjinga sana
 
Back
Top Bottom