Benard Membe: Musiba hasimami tena na kujifanya yeye ni Mungu Mtu. Huko uliko naomba hela zangu

Benard Membe: Musiba hasimami tena na kujifanya yeye ni Mungu Mtu. Huko uliko naomba hela zangu

“Niwaambie Watanzania wenzangu hakuna Mtanzania awe Ndovu au sisimizi mwenye kusimama juu ya sheria hakuna aliye juu ya sheria, ukimdhalilisha mwenzako ukadhani kwamba utaendelea kupiga miluzi na kufurahia kana kwamba wewe umefika Duniani kama Kiongozi au ndio mkubwa au Mungu Mtu, Mahakama Kuu ni jibu kwamba ukidhalilishwa fika Mahakamani uitafute haki yako nimefika hapa kwa niaba ya watanzania wote na Viongozi Wastaafu walionyanyaswa na kudhalilishwa na Mtu huyu"

"Naomba wajue hili halitotokea tena, hasimami tena kudhalilisha Wazee na Viongozi wake, hasimami tena na kujifanya yeye ni Mungu Mtu, hasimami tena kuwatukana Watu walioifanyia kazi Nchi hii kwa uaminifu na uadilifu wote, anasimama Mtu kwa kutumwa na kulipwa akadhani kwamba ataendelea kuishi Duniani katika hali hiyo hamtomuona tena akifanya hivyo na Musiba huko uliko naomba hela zangu"

Bernard Membe

Pia, soma=> Mahakama yaamuru Cyprian Musiba kulipa faini ya Tsh bilioni 6 kwa kumchafua Bernard Membe
Huyu nae ni mzee wa hovyo tuu...
A hell of a hypocrite. Miaka yote ya Magu akiwa Rais hakumuunga mkono, leo hii anajipendekeza kwa Mama.

Mpuuzi. Mnafiki.. Mhaini.

Na kama Mama eti atamuunga huyu... Atafeli vibaya mnoo.

Be Warned.
 
Kusaga meno kwa zamu,
Kuondoa magufuli NI kilio cha wengi sanaa.laiti wangejua
 
Zama za magu alikata Sana viuno,aliona watz wote ni mbuzi tu Dunia duara.
Jiwe kaacha wajane zaidi ya wajane.
Usicheze na watu kesho huwezi jua utakuwa nani
 
Mdharirishaji mwingine ni "power kaaya"!

Kijana miaka 31 unamtongoza Mama mwenye miaka 60, huu ni udhalilishaji wa kijinsia!!

Nasubiri kusikia kutoka kwa Rais mwenye ngonjera ya jinsia ya kike atasemaje kuhusu Power kaaya!!

Hahahaa mkuu lakini kumtongoza mtu sio kumdhalilisha hata Kama amekuzidi umri
 
Mzee msamehe kijana alikuwa anatafuta maisha.

Ajira wakuu hawakutoa kila mtu alibuni njia zake za kujipatia kipato wengine tuliamuaga kuwa wamachinga hata sisi tunahama tu taratibu kwa amri ya serikali sikivu ya mama yetu Mh Samia.

Ukimsaheme utajiongezea thawabu.
Pamoja na hukumu ya mahakama, Cyprian Musiba anatakiwa kuomba msamaha HADHARANI ili kufuta makosa yake kwa aliyotenda,kwa vyombo na njia zilezile. Pia anatakiwa kutubu ili apate kusamehewa na kupokelewa na mwenyezi Mungu.
Amen
 
Back
Top Bottom