Bendera mpya ya Syria yapandishwa Leo katika ubalozi wa nchi hiyo Mjini Moscow Urusi

Na waasi walishasema majeshi ya russia yaendelee kubaki na hawatashambulia mali na assets za russia.
Hapa ndo wanazidi kutuchanganya kabisa .nimesoma sehemu Tena ndege za uturuki zinawashambulia waasi wa kikurdi huku tunaambiwa hichi kikosi kilichomuondoa Assad kinasaidiwa na uturuki. Syria ina mchanganyiko wa hatari
 
Zaidi Urusi anawahitaji sana waasi hawa na atafanya chochote watakacho ili kile kilichompeleka pale cha kuzuia kujengwa kwa bomba la gas kutoka Qatar kwenda Europe kisifanikiwe.
Hofu ya dhahiri ya Russia ambayo ndiyo ukweli ni kitendo cha Ulaya kuwa huru na kuondokana na utegemezi wa gas yake



 
Unaona sasa, hivyo ndivyo chess linavyochezwa.

Shukurani kwa kujazia details.
 
Usigeuze GIA angani rejea post Yako ya mwanzo umeeleza vizuri kwamba hilo jengo la ubalozi lipo Syria na kwamba hapo siyo Urusi. Ila pia nashukuru kwa kuniitia dogo japo hatuonani basi tupeane heshima tu huwezi kujua labda nimekuzidi umri.
Ndio lipo Syria kama unaelewa maana ya ubalozi. Kama hujui, usinichoshe. Ahahahahaha!!
 
Wewe ndiyo unataka kuleta ubishi usiokuwa na maana, suala la ubalozi wa tz kuwepo marekani Lile eneo la ubalozi linatambulika ni ardhi ya tz lakini haiondoi maana ya kusema Hilo eneo la tz lipo marekani,

Hapo ubalozi wa Syria uliopo urusi ulipandisha bendera mpya, hapo limetaja urusi ili kuleta maana

Labda nikuulize ubalozi wa Syria uliopo urusi, marekani na ufaransa kwa mtazamo wako unaweza ukaelezea vipi kwa pamoja na ukaeleweka????
 
Putin anakuwa mtu wa kushirikiana na hata fisi ilimradi tu yeye mambo yake yawe sawa, maana huko anakoenda anakujua mwenyewe
Mataifa makubwa hayana rafiki wala adui wa kudumu ila yana maslahi ya kudumu ndo maana kiongozi aliempindua Assad CIA walishatangaza dau la karibu bilioni 30 kwa atakaemkamata ila jana Biden kampongeza kwa kuleta mwanga mpya Syria.
 
Dah!
 
Nimekuwekea hapo "The Vienna Convention". Nenda kaisome. Msinichoshe na kutokuelewa kwenu. Hili sio darasa.
 
Hamna cha chess wala nini Pro NATO mmepigwa chenga za maudhi na DUBU,ngoja mtaona baadae kwamba chui kavishwa ngozi ya kondoo kwanza
 
Mambo yanaenda chap kwa haraka!!! Ila confidence hii ni kwa sababu Kuna taifa kubwa sana la magharibi liko nyuma ya hii serikali mpya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…