Bendera ya Israel ndani ya magari ya Dar ni siasa tu au kuna la zaidi?

Ukiataka kujua mgogoro kati ya Palestina na Israel urejee kwenye historia. Wanaolalia kwenye Historia ndio wanaoiunga mkono Israel, na wanaosimamia mikataba na makubaliano ya Umoja wa Mataifa, wanailaani Israel.

Ukirudi kwenye historia ya kale, hilo Eneo lote la Palestina lilikuwa sehemu ya Israel. Baada ya waisrael kutawanyika Duniani kote, Wapalestina waliweza kuyachukua maeneo yote, hata yale ambayo kabla ya Waisrael kutawanyika, yalikuwa yanakaliwa na Waisrael.

Kama ingekuwa ni rahisi, hao wote Waisrael na Wapalestina, wote walistahili kuwa kwenye Taifa moja. Kihistoria kulikuwa na matukio mengi ya Waisrael kushambuliwa na kuuawa na Waarabu kuliko Waarabu kuuawa na Waisrael. Siku zote binadamu akidhulumiwa sana, atatumia muda wake mwingi kujenga ulinzi imara ili uonevu utoweke, na ndiyo walichofanya Waisrael.

 
embu soma zaidi kuhusu Israel sio unakariri tu unadhani Israel inapewa economic aid kama Tanzania?nyway wengi wa matajiri wakubwa ndani ya marekani ni wahayuni ,mind u any jew is a citizen of Israel
Israel inaogoza kwa kupokea misaada mikubwa ya kiuchumi na kijeshi kutoka marekani na misaada isiyo na masharti. waafrika tumedanganywa kuwa tunapewa misaada walati Israeli government inanufaika na misaada ya kweli sisi tunaambulia misaada midogo tena yenye masharti magumu. ikitokea siku ambayo Marekani atasitisha misaada na uhusiano na Israel huo ndio utakuwa mwisho wa Israel.

Amini usiamini Israel inapokea misaada kuliko nchi yoyote ile Afrika, Tanzania tunapokea misaad a kidogo kuliko Israel inavyopokea misaada kutoka Marekani
 
mbona inasemekana hitler aliwapiga sana au miaka hiyo walikuwa hawajajipanga
 
Bariki taifa la Israel nawe utabarikiwa
Mwanzo47:1-10
 
Jiulize kwanini hawatundiki bendera ya nchi nyingine zaidi za Israel zimezidi,people know what they are doing
 
kwanini ulimsikiliza Mtumishi mjinga na muongo.... hana akili pia.... hajui kuwa vizazi vya waisrael ndio hivyo hivyo hadi leo hii.... Most of christian followers hawajui Mungu wao anaitwa jina gani na anataka aabudiweje.... Roman empire ilifanikiwa kuwapumbaza ili kuenda tofauti na Mungu wa Waisrael so watumishi wake hubabaika na majibu ya kijinga kama hilo alilokupa.... Waisrael ndio Wenye Mungu huyo ambaye Yesu Myahudi alikuwa akimuabudu tena Siku ya Saba ya Juma... siku hiyo kazi unasema basi yaani ni kuget rest. ndio imeandikwa hivyo... Roman akaipindisha watu waende maboya hao hao Watumishi Wakiulizwa hujibu kijinga ati siku zote ni za Mungu sio ya Saba pekee....Wao ndio waliotoa maagizo ya uungu? STUKA.. kwa akili ndogo Watumishi ni wapotofu... na ukiwafuata ndio njia potofu.... Ukitizama Mafundisho ya Wayahudi ni tofauti na huu uitwao Ukristo yaani ni total different yaani hapo unabakia kutowaelewa wakristo hizi njia za kuabudu wanafuata Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo? maana wanaofuata ni Waisrael wao wana Mungu wao? Mkuu kama Dini watu wengi wanapotoshwa sana sometimes huwa Natamani Nilie maana ni Sawa na mtu unasafari ya kwenda Arusha kibao cha kuelekea Mtwara ndio kimeandikwa ARUSHA ukishika njia hiyo Arusha hufiki hakika.... STUKA ndugu
 
Jiulize kwanini hawatundiki bendera ya nchi nyingine zaidi za Israel zimezidi,people know what they are doing
Za saudi Arabia tunatundika mbona Sana..... ila Nadhani za Israel zina market zaidi....
 
Kwa wale ambao sio Wakristo,si rahisi sana kuelewa tendo hili.Katika Biblia hata hivyo yapo maandiko yanayo-onyesha kwamba ukiibariki Israel kama taifa by whatever means na wewe utabarikiwa.Sina hakika kama ukiweka bendera ya serikali ya Israel kwenye gari lako umeibariki Israel,nadhani umeonyesha solidarity with the government of Israel.Andiko ambalo watu wengi wanali-quote ni Mwanzo 12:3.Hata hivyo hili linamzungumzia Ibrahim zaidi as a person.Ambalo liko straight forward zaidi ni Zaburi 122:6.

Kwa upande mwingine kuna jambo ambalo watu wengi hawalifahamu.Israel inayo ongelewa kwenye biblia ni Israel as a nation,not the Israel government.The foundations of the Israel government are Satanic.Ndio maana mfadhili mkuu wa taifa la Israel ni familia ya Rostchild ambaye ni kati ya zile familia 13 za Illuminati.Hii inathibitishwa na nembo ya Freemason ambayo ipo kwenye lango kuu la Mahakama kuu ya Israel(The israel Supreme Court). Ile alama ya nyota iliyopo kwenye bendera ya Israel ukiifuatilia utagundua kwamba ni satanic (uki-google satanic symbols utaliona hili).It follows therefore that it represents the government of Israel and not the nation of Israel.Kwa mtu anayejua maana ya bendera ya Serikali ya Israel kwa hiyo hawezi kuitumia huku akidhani kwamba he is in solidarity with the nation of Israel.
 
halafu wanamwita eti ni mwenye haki!!
 
Kwanza kimtazamo wangu wengi hufikiria kuwa Israel ni taifa la kikristo wakati si kweli israel ni taifa la wayahudi na ndani yake kuna waarabu ambao ndio wakristo na waislamu
 
na ukiwauliza wanatokwa na povu na kutukana mbaya
 
Bendera ya Israel inaitwa 'the star of David.' Wanaoitundika popote pale ni wakristo na wanaihusisha na imani yao ya kikristo. Wengi wetu tunafahamu uhusiano kati ya mfalme na nabii Daudi na masihi Yesu Kristo. Hakuna siasa katika hili.
Wengi hawajui hili
 
Wanaweka ktk kuonesha love &support kwa Israel, ambapo wakristo wengi wanaamini ktk baraka za mzaliwa wa kwanza, na wanaamini kuwa Israel ni mzaliwa wa kwanza kati ya mataifa kwa Yehevoh

Nembo hiyo naitwa STAR of David au King david shield inaaminika ilikuwa ni ngao ya Mfalme Daud, na Muhuri wa Mfalme Suleiman.

Daudi ni moja ya wababu katika uzao wa Yesu kristo wanaoheshimika sana na wakristo pamoja na wayahudi

Lazima ukumbuke kuwa japo wahayudi si wakristo, lakin ukristo umetokana au umeundwa kwa misingi ya historia ya uyahudi.

Inafahamika kuwa founders wa taifa jipya la Israel, walikuwa ni wajenzi huru na hata uchaguz wa bendera hyo ulikuwa na utata sababu kuna ambao waliamin kuwa kuna symbols nyingine ambazo zina maana kubwa zaid ktk uyahud na hata ukristo mfano Taa ya vinara 7 .lakin inasemekana ma fore fathers hao walifanikiwa kuifanya nembo hyo ya kuwa bendera japo ina mahusiano sana na alama za wajenzi huru.
 
Hakuna utumwa mbaya kama utumwa wa akili,baada ya miaka mingi ya kufanywa watumwa,iwe slavery au colonialism au religion waafrika tumekuwa nothing but zombies,hatujitambui matokeo yake ndio hayo ya kuweka bendera za nchi za watu ambao hawana huruma na wewe hata chembe....NOTHING CAN FREE OUR MINDS BUT OURSELVES..BLACK PEOPLE WAKE UP !!
 
Hawa wana wa Ibrahim yakobo(Israel) na ishmail(mwarabu) wasiopendana wanaisumbua dunia kwakweli. Sisi wala ugomvi wao hautuhusu lakini tunatumika km marungu yao . Kila mmoja wao anataka dunia itambue dini yao, wanaiburuza dunia huku kule km tambara bovu, ni mkorogano kila wanakopita
 
Tofautisheni kati ya kabila la waisrael na Taifa la KIZIONIST , wayahudi wengi hawana imani na siasa za kiisrael. Taifa la Israel ni la watu wenye itikadi za kidini za Judaism, Christianity, Islam na Druz, unfortunately wale wenye ability ya kiArabu ndio hao wa madhehebu mengine matatu.

Lakini mbona sisi waafrika tunakuwa wapumbavu sana, kwa nini tunaumizana roho kwa sababu ya ugomvi wa mwarabu na myahudi?

Sisi ndio Ndugu, majirani tanaosaidiana pakitokea Tatizo, tunazikana. Sasa tuudhiane kisa bendera ya Israel?????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…