Benjamin Mkapa: Natamani kuwe na Tume Huru ya Uchaguzi, Wapinzani wahusishwe kwenye kupiga na kuhesabu kura na kutangazwa mshindi

Benjamin Mkapa: Natamani kuwe na Tume Huru ya Uchaguzi, Wapinzani wahusishwe kwenye kupiga na kuhesabu kura na kutangazwa mshindi

Madaraka ni kama uraibu wa vilevi. Mtu anafanya ubabe akiwa nayo na akiyaachia ndio anaona ukweli.

Ukilewa unaweza kufanya mambo ya ajabu halafu ukiwa sober unajiuliza niliwezaje kufanya vile?
 
Vyama vya upinzani wala wasilikubali kuwe na Tume Huru wala kuhusishwa kwenye hiyo tume. Mkikubali tu, huo ndio utakuwa mwisho wenu wa kufanya siasa Tanzania.

Siku zote mmekuwa mkiwaaminisha wanachama na wafuasi wenu kuwa mnaibiwa kura. Na hicho ndicho kinawafanya waendelee kuwaamini. Sasa siku ikianzishwa hiyo tume na mkashirikishwa halafu mkashindwa. Mtawaeleza nini?
 
Uliwachukia wapinzani kwa kiwango cha hali ya juu. Kauli za "wapumbavu" ulizozotoa hadharani zinathibitisha hilo!
Nimesoma mahali ukitamani wapinzani washirikishwe katika tume huru ya uchaguzi na wawepo kuhesabu na kuhakiki kura. Ni jambo la heri umeliona hili wakati uko hai na ni muda wako kushauri/kumshauri Rais Magufuli kuacha chuki dhidi ya watanzania wa vyama vya upinzani.

Kwa nafasi yako, lifanyie kazi maana mwenzako amekuzidi chuki dhidi ya wapinzani!

 
Pamoja na yote

Hiki anachokiongea ndio haki na ukweli halisi
I second u. Tuangalie maneno yake yana ukweli kiasi gani. Hili analosema linahitajika sasa au haliitajiki?
Kwamba ni mnafiki, muongo hilo halina maana kwa sasa, wote wako hivyo hivyo.
Tusiangalie ukweli unasemwa na nani, hata ungesemwa na shetani utabaki kuwa ukweli, na alichosema Che-nkapa ni ukweli pamoja upungufu uliokuwa nao ktk uongozi wake.
 
Back
Top Bottom