TANZIA Benjamin William Mkapa, Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tatu afariki dunia

Status
Not open for further replies.
We jiropokee tu,kama Nick anaweza kufanana na dingi ake(Mkapa) na akawa ni mtoto wa Mramba then hio itakua ni matunda ya Ccm mpyaaaaaaaaaaaa.
Uliza wahenga watakuambia ukweli mkuu
 

Kwani alikuwa na mchango gani kwa umoja wa nchi hii, mpaka useme kuondoka kwake kunaweza kuwa tatizo la umoja wa nchi hii? Yeye aliamua kuishi kama MwanaCCM, na hajawahi kujali umoja zaidi ya kuhakikisha CCM ndio inakuwa nchi.

Tuache sifa za uongo kwa watu wasiostahili sifa hizo, eti kisa wamefariki.

Ni kweli amefariki kama binadamu wengine, tunamuombea asemehewe kama anastahili. Lakini hakuwa na jipya lolote ambalo kuondoka kwake watanzania wote watalikosa.
 
Mzee Mkapa Alale kwa amani. Sisi sote Ni wapita Njia Hata ungekua na Nguvu ya pesa na Madaraka wewe utakufa siku moja.
Watu inabidi walitambue hili na kwa hivyo wasipapatikie sana mambo ya dunia hii Itamfaidia nini mtu kuupata ulikwengu wote na kuukosa uzima wa milele? Mbona tuko duniani kwa kitambo kidogo tu.

1 Timotheo 6:6-10 inasema,"6Walakini utakatifu na kuridhika ni faida kubwa. 7Kwa maana hatukuja na kitu duniani tena hatuwezi kutoka na kitu, 8 ila tukiwa na chakula,nguo na makazi tutaridhika na vitu hivyo. 9 Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu, tanzi na tamaa nyingi zisizo na maana zenye kudhuru ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu.

10 Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha,ambayo wengi hali wakiitamani hiyo, wamefarakana na imani na kujichoma na maumivu mengi."
 
RIP mzee Mkapa, Duniani tunapita na mbele yetu ni hukumu ya milele. Tuishi tukitenda haki kwa wote bila ubaguzi wa kikabila au ukanda
Tuishi vyema na wengine, usiwatendee wengine kitu ambacho wewe hutaki kutendewa.

Again, RIP Mkapa
 
Mwenyezi Mungu amlaze mahala Pema peponi. Alishikwa mkono na Nyerere naye akamzika kidogo kabla ya term yake yapili Naye kamshika mkono Magu ambapo Magu anamzika kidogo Kabla ya kipindi chapili... Mungu na amrehemu
 
Reactions: SMU
Asante, ila wakati tunasubiri hizo taarifa za uchakachuaji, acha tuendelee na hizi zinazoletwa na wadau wa ukweli.
sasa kama mnavyanzo vyenu mnataka taarifa nyingine za nini??
 
Pumziko la amani Apate huko aendako Mzee Mkapa.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…