TANZIA Benjamin William Mkapa, Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tatu afariki dunia

TANZIA Benjamin William Mkapa, Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tatu afariki dunia

Status
Not open for further replies.
Umri siyo warrant ya Kifo. Hata wewe waweza kufa ukiwa na umri unaoringia.
Hayo maelezo kila mtu anayafahamu usijidai unajua sana hapa, nilichokiandika na ulichokiandika wewe ni vitu viwili tofauti.
 
Hata huyo Omar Juma makamu wake wa Rais walimfanya kitu kibaya wenyewe
Mr Omar Juma was a trusted friend and close ally of Mr Mkapa and had been his vice president since the Tanzanian leader came to power in 1995. He was seen as a possible successor to Mr Mkapa when he steps down in 2005.

Although the 60-year-old Juma had a history of heart problems, his death last night came as a complete surprise.

The vice president was seen in public only hours before his death, bidding farewell to Democratic Republic of Congo President Mr Joseph Kabila at Dar es Salaam's international airport, and looked in good health.
 
Hivi watu hawaoni Watanzania wengi wanavyokufa tena vijana na hakuna anaeshoboka ila kafa mmoja tu basi nchi inasimama. Ni watu wangapi wamekufa kwa siku ya leo pekee na hawana hata miaka 60.

Mzee mkapa keshakula chumvi nyingi APUMZIKE KWA AMANI

Ndo uone akili za watz zilivyo. Watu wastani wao wa kuishi umri haufiki miaka 70, mzee kapiga zaidi ya 80, bado wanatafuta wachawi. Watanzania wangapi wanafikia umri wake?

Na kwa mwili wa mzee huyu miaka yote lazima alikuwa na magonjwa kadhaa kama BP, Kisukari, etc. Sema tu quality ya maisha yake ilimsaidia kuishi vizuri. Sitashangaa wakisema alipata stroke au heart attack. Mwili wake unaruhusu magonjwa hayo.
 
Ninachoshukuru Mungu huyu mzee alibadilika sana mwishoni. Hata akiongea alionekana alikuwa anajutia maamuzi mengi aliyoyafanya huko nyuma ikiwemo kumpigia chapuo Magu kuwa raisi. Siku moja aliwaponda hadharani watu wanaosema raisi Magufuli amefanya hivi akawaambia waseme CCM imefanya hivi..
Ni kawaida viongozi wengi wa kiafrica wakitoka madarakani hujutia mabaya waliyofanya.

Hakuna Jipya hapo. Apumzike alipojiandalia.
 
Huu msiba utaleta changamoto kwa ccm dhidi ya upinzani hasa Membe
Hili ni pengo kubwa sana kwa Taifa letu. Hakika MOLA wetu ndiye alitoa, na pia ndiye ambaye amemtwa mja wake. Jina lake BWANA na likapate kuhimidiwa. Amen [emoji120] Pole nyingi sana kwa familia yake, na pole nyingi pia kwa Watanzania wote ambao wanaguswa na msiba huu mzito.
 
Ufunuo wa jambo hili,ulinitokea takribani mwezi mmoja uliopita,,nikaona nikae kimya nione kama itakua au ni ndoto tu,,

Hili ni pengo kubwa mno kwasasa.
 
Duu! Ni msiba mkubwa kwetu sote watanzania na familia ya Marehemu Mh. Mkapa! Nilianza kuziona dalili hizi tangu alipotoa kile kitabu" MY LIFE, MY PURPOSE" na hata kuanza kuungama baadhi ya makosa aliyoyafanya katika utawala wake!

Tunakushukuru HAYATI BENJAMINI WILIAM MKAPA kwa kutuachia wasia kupitia kitabu chako kile, nina imani yapo mengi yatatusogeza mbele kama taifa! Mwenyezi Mungu aipumzishe Roho yake Pahala Pema peponi. Amen!
 
Hata mimi nahisi itakuwa ni hayo mawili: heart attack au bp.

Na jamaa alikuwa obese kiasi...
iPerhaps Corona pia maanna gathering zote za vikao vya ccm Ila muhumbili wanajua zaidi
 
Kuna jambo la kujifunza kwa kifo cha mzee Mkapa
1.Binadamu wote njia yetu ni moja
2.Kifo sio Mali ya Binadamu bali ni Mungu mwenyewe hivyo hatuna sababu yakutoa uhai wa MTU awaweyote kwa sababu yoyote...
Ufisadi wa kutisha
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom