Benki kuu: Nchi ina fedha za kigeni za kutosha hata kama shughuli za uzalishaji zitasimama kwa miezi sita!

Wewe jamaa ni mjinga sana (samahani kwa kukuita hivyo) .kukusanya kodi kwa kutumia nguvu bila akili utakusanya fedha kidogo sana kwasababu walipa kodi wengi watakuwa waoga na wengine hawatafanya biashara kabisa.ukitumia akili utakuwa na walipa kodi wengi na utakusanya fedha nyingi.
 
Ingekuwa hivyo, ndiyo hiyo serikali ishindwe kuwalipa nyongeza za mishahara, ambayo ni kwa mujibu wa sheria kwa miaka 5 mfululizo??
 
Ni kweli kwa wenzetu Ulaya nk kodi si ya kubembelezana lakini pia kodi kila mtu analipa hakuna sekta isiyo rasmi inayobweteka. Hivyo wigo ni mpana lakini pia mifumo iko imara, madhubuti na ya wazi na imetengenezwa kulipa kodi bila shuruti kwa kwa viwango rafiki. Maafisa wa kodi ni waadilifu. Hapa kwetu tofauti.
 
Kinadharia walio soma uchumi wanajua kuwa ni shariti kwa nchi yeyote ile iwe na reserve ya pesa za kijeni ya kujiendesha kwa muda wa miezi sita,kwa hiyo hilo ni takwa la kisheria na nilazima,,ili kujua hiyo pesa ipo au haipo angalia janga la korona lilipo tokea serikali ilifanya jitihada gani kusaidia wananchi wake!!!!!! Kenya,Uganda na Rwanda sehemu ya hiyo reserve ilitumika kipindi Cha korona.kusema tu serikali ina reserve ya miezi sita inaweza kuwa blaa blaa Kama tulishindwa kununua mashine za dharura za kupima corona hata ziwepo kwa kila mkoa.
 
Mmeanza tena mapropanganda yenu ya kitoto afu baadae mnapata aibu hamjifunzi kuwa wakweli
 
Hata siwaamini viongoz wetu hata magu mlisema ni mzima
 
Basi tu, ni bahati yetu nzuri, ambayo hadi sasa hatuna maelezo juu yake; vinginevyo Corona ingechachamaa kama huko kwingine nchi yetu ingeaibika vibaya sana.

Magufuli kapiga danadana kuficha hali mbaya ya kutokuwa na uwezo wa kulikabili gonjwa, kama alivyokuwa hana uwezo wa kuwaliwaza wafanya kazi wake miaka mitano mfululizo!
 
Wameanza uongo wao. Hivi nchi yetu ina reserve ya mafuta ya kutosha muda gani bila kuagiza?
 
Aliacha hakuna kitu, serikali ilikuwa inakopa kwa wafanyabiashara kina rostam!
Safari kila uchao unadhani fedha za kigeni zitabaki?
Hao wafanyabiashara wana mfuko mpana kiasi gani?
Huyo Rostam ina maana alikuwa anakopwa tu halipwi? β€”Si angefirisika?.

Na pia labda hujui Rostam alikimbia nchi lini hadi ulete stori hizi za vijiweni

Wastani wa Makusanyo ya mwezi kipindi cha JK ilikuwa shilingi bilion 850, na kila mwaka tulikuwa tunatoa ajira kedekede, kupandisha kima cha chini, kulipa makimbikizo ya wafanyakazi etc. Sasa kama serikali ilikuwa haina hela hao waliokuwa wanaajiriwa maelfu kwa maelfu hela ya kuwalipa ilitoka wapi?
 
Kuwa na akiba iliyorundikana benki bila kuzunguka hakuna faida yoyote kwa yeyote bali ni hasara kubwa kwa wananchi. Hiyo hutumika kama dhamana za benki kuweza kuiingiza nchi kwenye hasara za kukopa zaidi.
Ulichokiandika sio sahihi,

Ni takwa la kisheria kwa nchi kuwa na akiba kwa ajili ya dharura pindi yanapotokea majanga ya aina flani.

Wenzetu huwa wanaweka akiba ya fedha na dhahabu,

Mzunguko wa fedha ni swala tofauti na akiba ya aina hii.
 
Sisi wanannchi tutawapima baada ya miaka kadhaa. Ikae hapo hapo ama iongezeke
 
Aaaaaaaaaaaaaaa........miezi 6 tu, nilifikili kwa mwaka 1

Miezi 6 ni muda mchache sanaπŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Mimi huwa nasikitika sana nikisikia kiongozi au mtaalamu anaongea namna hii inasikitisha sana kwa kweli, anajuwa madhara yake? hiyo pesa ikipungua kwa miezi miwili tu Tsh itaanza kupoteza thamani kiwango cha lami mpaka ufike hiyo miezi sita basi tutakuwa tunafungia vitumbua haina thamani. Ukiona unatumia akiba basi ujuwe hali ni mbaya na inaleta mshtuko katika uchumi sasa hizi kauli ni mbaya sana kuongelewa na nani alimuuliza? kuna haja gani ya kuongea au wasiwasi wa nini? mimi nadhani kuna watu wamezipitia huko sababu kauli ya kijinga sana tena naibu Gov. ujinga mtupu
 
Wewe ndio njinga,nitajie nchi gani iliyoendelea inayobembereza mfanyabiashara kulipa kodi?tena nchi kama china ukibainika unakwepa kodi unanyongwa kabasa,Italy, Marekani na baadhi ya mataifa ya ulaya ukibainika kukwepa kodi unafungwa na kufirisiwa.Ni Tanzania tu inayobembereza mfanyabiashara kulipa kodi watakavyojisikia.
 

Wapi kasema kubembeleza? Kutumia akili ni kubembeleza. Kama unatumia nguvu kuliko akili wapishe wengine wakuonyeshe faida ya akili.
 
Aliacha hakuna kitu, serikali ilikuwa inakopa kwa wafanyabiashara kina rostam!
Safari kila uchao unadhani fedha za kigeni zitabaki?

Na kukopa kote miaka 10 yake yote hajazidi miaka 5 ya mwendazake kwa ukubwa wa deni la taifa.
 
Nani anabembelezwa kulipa kodi? Tunazungumzia mechanisms zinazotumika kukusanya kodi hatuzungumzii mambo ya kubembeleza. Kutumia nguvu kufunga akaunti za wafanyabiashara au kuwapigia hesabu ambazo halizingani na turnovers katika biashara hapo mzee unaua walipa kodi siyo unaongeza. Nisuala la kutumia akili tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…