Benki Kuu Tanzania: Mlioficha Dola zirudisheni kwenye mzunguko

Benki Kuu Tanzania: Mlioficha Dola zirudisheni kwenye mzunguko

Unanunua kwa pesa ya Japan sio lazma Dollar
Hiyo pesa ya Japan [emoji384] unaitoa wap wakati hakuna chochote unachouza Japan.

Mlinganyo wa fedha za kigeni ni mwepesi tu; Zalisha sana na Uza nje sana = Fedha za kigeni, alafu zitumie vizuri Kwa Kuagiza/nunua Nje vitu Muhimu na vya Lazima tu. Tena ikiwezekana uku unafuatilia akibika yako vizuri.
 
Afrika ikisimama yenyewe anaweza kuwa mzalishaji mkubwa wa tatu duniani ,baada ya Marekani na china.

Tunaweza kufanya kama ulaya wanavyotumia EURO na hiyo currency ndio itatumika kuleta balance of payments
Hizo akili zakufabya hivyo zipo sasa.
 
Benki kuu na waziri wa fedha wanapaswa kulaumiwa. Kwa muda mrefu walifix thamni ya shilingi kwa dola wakidhani wanalinda thamani ya shilingi. Kumbuka kuna wakati dola ilisimama kwenye zaidi kidogo ya shs 2,300 wakati matatizo ya vita vya Ukraine yalifanya uchumi wa dunia uyumbe. Cha kushangaza thamani ya shilingi ilibaki pale pale bila kuyumba - kumbe ilikuwa fix. Kumbuka hapakuwepo (nadhani hadi sasa) na vyombo binafsi na huru vya kununua na kuuza fedha za kigeni. Ilikuwa ni BOT na Benki zenye mkono wa serikali tu.
Wajanja walipoona hivyo kuwa thamani halisi ya shilingi siyo hiyo, wakaamua kununua hizo dola kwa bei ya fix iliyowekwa. Yaani waliona kuwa ndani ya muda mfupi bei ya kuuza dola itakuwa zaidi ya bei ya kuuza ya wakati huo.
Labda nifafanue hapo, Bei ya kununua dola (benki kununua ilikuwa 2315, na ukitaka kununua toka kwao yaani kuuza ilikuwa say 2400). Hivyo wajanja wakaamua kuzinunua kwa bei hiyo (2,400) wakijua kuwa punde wataweza kuziuza kwa shs 2,466 sasa na hivyo kutengeneza faisa ya shs 66 kwa kila dola moja.
Hicho naona ndicho kilitokea. Kama wangeacha shilingi ikatafuta thamani yake yenyewe hiyo 2,400 na 2,315 zisingekuwa hizo, zingebadilika kulingana na soko na mwanya wa kupiga ungekuwa umejiziba wenyewe mapema kwa nguvu ya soko
Anyway nisiupige mwingi, ngoja nibaki na uganga wangu wa kienyeji!
 
View attachment 2761849
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba amewataka watu walioficha Dola kwa malengo ya kusubiri zipande thamani na kujipatia Faida zaidi kubwa, waziachie kwenye mzunguko wa Biashara, ili kuondoa uhaba wa Fedha hiyo Nchini.

Kauli ya BoT inakuja ikiwa ni wiki chache tangu Mkurugenzi Utafiti na Sera wa Benki hiyo, Suleiman Misango, aseme upungufu uliopo sasa wa Fedha za kigeni ni himilivu kwakuwa akiba ipo ya kutosha.

Hii kauli hii ya Benki Kuu inakupa tafsiri gani?
Hii Nchi hii!!
 

Attachments

  • IMG_20221031_153403.jpg
    IMG_20221031_153403.jpg
    37.6 KB · Views: 1
View attachment 2761849
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba amewataka watu walioficha Dola kwa malengo ya kusubiri zipande thamani na kujipatia Faida zaidi kubwa...
Ni ngumu sana kwa watu hao kurudisha fedha zao walizoficha kwa urahisi kwa sababu Serikali ya Tz haiaminiki. Nyinyi BOT, Je, mnajua kwa uhakika kwamba "Kinyonga ana rangi?"
 
View attachment 2761849
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba amewataka watu walioficha Dola kwa malengo ya kusubiri zipande thamani na kujipatia Faida zaidi kubwa...
Tangu anateuliwa niliona janga, hivi nani anaweza kuficha fedha isiyo yake hadi ikaadimika?
 
Back
Top Bottom