Benki Kuu ya Tanzania: Hatuuzi dhahabu kufadhili miradi ya Serikali


Utamuachia uhuru mwizi si utakuta kamaliza kihenge chote!! Huyu mama bila kumthibiti wajanja waliomzunguka wataiba kila kitu na yeye wakati yupo anaimba taarab ; ndio maana WATANGANYIKA lazima tupige kelele sana ama sivyo dhahabu yote itapelekwa Oman kwa wajomba.
 
Naona nyundo zimekuwa nyingi hadi wameamua kutoka kusema na kuomba poo!
===========
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) leo tarehe 30 Januari 2026, imesema ina mpango wa kuuza sehemu ya hifadhi yake ya dhahabu kwa ajili ya kusawazisha mizania ya akiba ya fedha za kigeni na siyo kufadhili miradi ya kimkakati ya serikali.

Akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari uliofanyika katika ofisi za BoT jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha wa BoT, Bw. Emmanuel Akaro, ameeleza kuwa kinachotekelezwa ni mpango wa kuuza dhahabu iliyozidi kiwango kilichoidhinishwa, kwa lengo la kusawazisha mizania ya akiba ya fedha za kigeni nchini.

“Sababu ya Benki Kuu kuuza dhahabu ni kujitoa kwenye vihatarishi vya kuwekeza kwenye dhahabu peke yake. Lazima tuhakikishe uwiano wa dhahabu na fedha nyingine za kigeni kwenye mizania ya Benki Kuu zinaendana na matarajio ya Bodi, matarajio ya nchi na matarajio ambayo hayatupelekea sisi kupata hasara”

Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa wastani wa kununua dhahabu wa mwezi ni tani moja na kwa kipindi cha mizezi mitano iliyopita BoT imenunua wastani wa tani mbili,hivyo, kulazimika kuwekeza tani moja ya ziada katika fedha za kigeni mbalimbali.

“Kwa kipindi cha miezi mitano iliyopita kila mwezi tunanunua dhahabu wastani wa tani 2 kwa mwezi ambayo ni kwa mujibu wa sheria. Matarajio yetu mwanzoni yalikuwa ni kununua tani moja kila mwezi kwa hiyo tani moja inayozidi tunaitumia kusawazisha mizania ya akiba za fedha za kigeni”

“Kuna utaratibu wa namna ambavyo Benki Kuu inatoa fedha kwenda serikalini, inapitia Mfuko Mkuu na uidhinishwaji wake unakuwa umefanywa na Bunge na ukiangalia pale hakuna kipengele ambacho kinasema Benki Kuu inaweza kuuza dhahabu ili kuipatia serikali fedha kwa ajili ya kufanya miradi yake”, aliongeza Bw. Akaro.

Hadi kufikia jana Januari 29, 2026, BoT ilikuwa na akiba ya fedha za kigeni yenye thamani ya dola bilioni 6.52, na kati ya hizo, dhahabu inakadiriwa kuwa dola bilioni 1.2, dola za Marekani bilioni 3.8, na sarafu ya China (yuan) dola milioni 735.

 
Acha tu wajikanyagekanyage. Utadhani kununua dhahabu nyingi kuliko kiasi kilichoidhinishwa na Board ni jambo la kheri. Nani amewajibika au kuwajibishwa kwa kukiuka sera ya BOT?
 
Sema tamaa ya kupata kingi ndio kimewaharibu wangekua na nia ya dhati wangependwa sana na Nchi ingeendelea sasa wakaja na mambo ya kuwekana jela kesi hazieleweki mara kutekana ndio tabu ilipoanzia hapo..
Viongozi wetu ni malimbukeni, washamba wa madaraka, nchi hii wangetumia akili kidogo tu basi wangetutawala milele bila ya kelele
 
Wangese hawa wanatuona sisi ni viazi...
 
Jibu jepesi ni njamq za wizi tu.
 

BOT wanapeana kazi kindugu wamejaa vihiyo tu.
 
Mkuu watafutie eneo hapo Kibaigwa watunze dhahabu watu wanatunza dhahabu za kutosha huko Chunya eti serikali inakuja na maneno ya mizania hawa jamaa sijui walisoma wapi shule zao kazi za kupeana hizi kazi kweli kweli.
Syo kibaigwa dumila tu hapo,mm mwenyewe kitambo nakusanya vijigram huko kusini navitunza
Alafu kwa dhahabu tuliyokuwa nayo hao central bank walitakiwa wawe na zaidi ya hizo tani
Kwenye reserve yao

Ova
 
Ameeleza kuwa kinachotekelezwa ni mpango wa kuuza dhahabu iliyozidi kiwango kilichoidhinishwa, kwa lengo la kusawazisha mizania ya hifadhi ya dhahabu ya benki hiyo.😂
Kwani zikizidi zitaoza au nafasi ndogo?
Wanataka kutuambia kwamba dhahabu ni kama machungwa😅
 
Kwa huu mkanganyiko ndo maana hata Machawa wanalala mbele cause hawaelewi waanzie wapi waishie wapi kutete serikali yao haram😁😁😁Endeleeni kupiga spana mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…