Benki ya Amana inahujumiwa

Inaonekana una furaha sana hii benki ife.Nakuhakikishia kama wakifuata ushauri wangu itadumu mpaka kiama. Hakuna historia ya benki za kiislamu kufa kwa kushindwa kujiendesha.
Wala sina furaha. Kwani inanisaidia nn mkuu. Bank za kiislam zinakufa tu na ni kawaida bank kufa usidhani ni mwisho wa dunia zikifa
 
sasa hiyo faida ya 500 si ndio riba yenyewe, kwanini pasiwe nayo kabisa?
 
Mimi ni muislamu na natumia hii Bank kupitishia mshahara
1. Amana sio Benki inayofuata Sheria ya kiislamu, sema Ina jina la kiislamu.

2. Amana Wana riba Kama Benki nyinginezo ila wanaificha tu

3. Waislamu wengi ni wa hovyo katika utendaji, pale wameajiriwa waislamu sawa ila waislamu majina wachumia tumbo (wengi wao)

4. Taasisi ikiingia nembo ya uislamu tu basi utendaji kazi wake lazima utakuwa hafifu, shida sio uislamu shida hao wanaojiita waislamu hawapendi kufuata huo uislamu, na kanuni na taratibu.
 
Wenye akili wakisoma bandiko lako wataishia hapa.

Mambo ya kiuchumi nyinyi mnataka kuingiza udini.... Hata kwenye swala la bandari tumeona ujinga kama huu
Hiyo sio shida, kwenye uislamu Kuna course za uchumi kwa mujibu wa uislamu.


Kuna Sheria na taratibu zake ambazo zikifuatwa mambo yanaenda barabara, shida ni kuzifuata sasa
 
Ishu kubwa tunashindwa kusimamia mambo, tusimtafute mchawi

1. Amana Bank kuchukua advance salary mzunguko Hadi mtu anaghairi

2. Ukichukua advance salary, mshahara ukiingia unakuta hawajakata pesa yao. Yaani inabidi mtu achukue pesa yake halafu awaachie pesa yao watakata muda wanaojisikia, ila mtu akitaka kuchukua yote anaweza kuchukua (japo huifungia akaunti yake)

Wanashindwa kujifunza hata kwenye mitandao ya simu??

3. Kupata mkopo ni mzunguko mrefu Bora hata uende CRDB au NMB

4. Mkopo wanajifanya wanakukopesha thamani (wanakununulia vitu ). Huu ni uongo na udanganyifu na haipo katika uislamu.

Pia riba ipo, tena inakaribiana na CRDB

5. Ukiwa mzembe (hujui hesabu) kwenye mkopo wanakulipisha hela nyingi zaidi

6. Kuna mfanyakazi mwenzetu alienda kutoa 400k ikagoma, Kadi ikatoka, akatoa tena ikagoma Kisha akatoa Mara ya tatu 400k.

Kwenye risiti wamemuandikia katoa 1.2M badala ya 400k


7. Mwezi uliopita Kuna mfanyakazi mwenzetu hajaingiziwa mshahara, kumuuliza HR anaambiwa itakuwa Benki ndio shida, kwenda Benki eti wanasema walimruka

8. Mwezi huu Kuna mfanyakazi mwenzetu, amejaza fomu ya advance salary ila hakupewa akaamua apotezee, umetoka mshahara wamemkata hiyo advance salary ambayo hawajampa


IN SUMMARY

Benki inaendeshwa kihuni, inapoteza wateja, mwisho wa siku mnaanza lawama Kama hizi
 
Kama ni wasikivu watasikia hapa.
 
Basi kama wa riba tuabie rate yao, pia usema huduma zao zingine za ziada zinazo tozwa wateja ili tulinganishe na beki zingine, bila hivo zitabiki kua hujuma kama hujuma zingine za biashara.
Kwanza Amana Bank hawakopeshi pesa

Wanakopesha thamani Kama nyumba, gari, pikipiki nk

Wanachokifanya, mfano Mimi nataka nikope gari

Natakiwa kwenda kwa wauzaji magari, nikubaliane nao Bei Kisha wanipe invoice statement

Mimi nawapelekea Amana, Kisha hao wanamlipa muuza gari directly na Mimi naenda kuchukua gari (watu wengi huwapanga wauzaji, huchukua pesa badala ya kitu kinachouzwa)
_ kwanza huu ni uhuni maana wao haikwepeki wamekopesha pesa sio gari.

Kama gari ni 15M unaweza ukajikuta unalipa 17M kasoro

Pia kupata huo mkopo lazima Kuna wajuba uwape hongo bila ya hivyo wanakuzungusha mno

Nilivyofanya calculation zangu nikapata riba ya 12.5% japo Kuna mfanyakazi mmoja tumemuuliz (kwa simu) anajifanya hajui
 
Nilitaka nikufahamishe kuhusu uendeshaji wa Benki za kiislamu, shida ushaingiza udini, Bora nikuache


Ila tatizo la Benki hiyo sio mfumo wa uislamu, shida ni usimamizi mbovu
 
Amana bank huwa wana ajili vp? Sijawahi kuona tangazo mtandaoni wakihitaji wafanyakazi, hii huenda inasababisha benki kukosa watu wenye weledi na washindani.
 
Mkuu hapo alie sema uongo ndo mwenye kosa sio benki, kwahiyo uaiseme kwamba wanatoza riba, mtu kanunua gari sh 15m kakuuzia 17m hiyo ni biashara na ziada ni faida sio riba.

Tatizo watanzania kila kitu tumezoea kusema uongo sasa utampangaje muuza gari wakati wewe unahitaji gari kabisa, kutoa rushwa ni utashi wa mtu sio sera ya benki.
 
Amana bank huwa wana ajili vp? Sijawahi kuona tangazo mtandaoni wakihitaji wafanyakazi, hii huenda inasababisha benki kukosa watu wenye weledi na washindani.
Wewe ulishawshi kuona mkombozi benki inatangaza na fasi za kazi? Hilo tangazo lilete hapa tulione kama ulisha wahi.
 
Una parochial understanding katika masuala ya uchumi ubongo wako umeja jaziba na chuki za kidini.
 
Alwaz aka @Ami njoo huku...benki yenu ya Amana imepost hasara ya 1.1bil Sept 2023, naona uhujumu umepamba moto....fanyeni mambo muiokoe kabla haijafungwa

Wenzenu wametengeneza faida ya mabilioni lakini Amana banki wao wanatengeneza hasara ya mabilioni
 
Mimi sina la kufanya.Hatutaki watu wazembe na wasiosikiliza maoni.
 
Inayoitwa hujuma ni ya watu wa ndani wala sio ya washindani wa nje, na unaweza kuta ni gross incompetency sio kwamba wanaamua tuhujumu.
Safi sana, you're a great thinker. Hapa Tanzania kila failure tunasingizia hujuma wakati unakuta wafanyakazi hawana professionalism, wanaajiriwa kwa connection, usimamizi mbovu, ufisadi mwingi alafu kampuni ikifa unasikia "hujuma".
 
Kasome islamised economics ujue tofauti ya riba (interest) na faida (profits) tatizo lenu mnakurupuka bila kua analytical katika jambo unalo paswa kujufunza kwanza.
Yaani nahitaji pesa nikanunue passo ya milioni 8 unaninyima ela unaenda kuninunulia hiyo passo na kunidai milioni 10 alafu unaniambia hakuna riba?? Natakiwa niwe mbumbumbu kwanza ndio niamini huo upuuzi, kitu bila riba nipe milioni kumi nikurudishie milioni kumi kwa muda wa miaka mitano, hiyo ndiyo interest free, out of that ni utapeli kama utapeli mwingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…