Benki ya Dunia yachelewesha tena kuipa Tanzania mkopo wa Dola 500M

Benki ya Dunia yachelewesha tena kuipa Tanzania mkopo wa Dola 500M

Hakimu Mfawidhi,
ivi jamani mbona kiki za kuwa makusanyo yako juu na tunaweza kuwa donor kantri inakuwa kinyume na maamuzi ya kuendelea kuombaomba mikopo?
 
Watu weusi tuna shida sana. Nafikiri kuna Tatizo kubwa sana kwenye akili zetu na mioyo yetu. Hivi mtoto aliyepata ujauzito kuna Tatizo gani kwa yeye kuendelea na elimu hii hii ya kawaida kama wenzake ?
 
MsemajiUkweli,
Si kama huu ugumu na ukakasi hauonekani, kelele hizi ni dhidi ya kiongozi anayetaka kuwa yeye ni kilakitu. Kauli zake ndio zinazosumbua. Akubali kumeza matapishi yake. Japo angekuwa na subira Kipindi kile kungekuwa na fursa ya kuangalia namna bora ya kurudi shuleni
 
MsemajiUkweli,
Ni watoto ambao hawawezi kuwa na uamuzi wa ngono as they are minor na kurubuniwa na ma sugar daddy na wengine hutembea umbali mrefu sehemu zenye mapoli na kubakwa na kwa hiyo kisheria ni waathirika wasio na hatia.
 
MsemajiUkweli,
Mkuu, unafahamu kwamba hili la mabinti kupata MIMBA na kuzaa na kuendelea na shule lipo kwenye ILANI ya chama tawala? Hili la kuzuia watoto wasiende shule baada ya kuzaa ni mawazo binafsi ya mtu mmoja but chama kama chama kiliwekwa kabisa kwenye ilani, sijui kwanini hamtaki kusoma. Mambo ya Ndege na lile la umeme ( ni mambo mazuri ) hayapo kwenye ILANI ya ccm but hili la wajawazito na shule, lipo kama AHADI ya ccm kwa wapiga KURA wake.
 
Watu weusi tuna shida sana. Nafikiri kuna Tatizo kubwa sana kwenye akili zetu na mioyo yetu. Hivi mtoto aliyepata ujauzito kuna Tatizo gani kwa yeye kuendelea na elimu hii hii ya kawaida kama wenzake ?
Tuwape muda watabadilika polepole tayari wameanza
 
MsemajiUkweli, Ikifikia mtoto kujifungua na kurudi darasani, yule aliempa mimba pia sifungwe miaka 30, ni kumnyima haki yake, badala yake apumzuke nyumbani asubiri kurudi shuleni pamoja na aliejifungua. Ili wasiachane kielimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MsemajiUkweli,
Acha upotoshaji kijana,awamu zote walikuwa wakirudi shule hawa mabinti,mbona kulikuwa hamna tatizo?
kwani serikali inapata hasara gani kuwasomesha hawa mabinti,mbona awamu zilizopita walikuwa wanasoma na kufunya vizuri tu kwenye elimu?

nina mfano mzuri tu,mtoto wa jirani yangu alipata mimba akiwa form five,akalea mimba na kujifungua baadae alirudi shule na kufanya vizuri akajoin chuo na sasaivi ni muajiriwa wa serikali.
nina mifano kibao ya mabindi waliojifungua na kurudi shule .
 
Mtoto akipewa mimba kuwepo na special schools za wazazi ambazo ni private kama walivyofanya juvenile courts. Wasichanganyikane na wenzao ambao ni fresh.

Na kitendo cha mtoto kupata mimba kinafutia validity ya kuitwa mtoto. Ngumu ku exercise haki za mtoto maana keshakuwa mzazi. Apambane na hali yake maana alipovua chupi alijua kabisa kuwa madhara yake atavimba juu.Tusiendekeze ujinga.
Ndugu lets think beyond our noses,majirani zetu kenya mtoto anatoka darasani na kukimbia nyumbani kunyonyesha ,na wanatuzidi uchumi elimu kasoro madini tu,mbona wako sawa tu sisi,tunafeli wapi?
 
Ndugu lets think beyond our noses,majirani zetu kenya mtoto anatoka darasani na kukimbia nyumbani kunyonyesha ,na wanatuzidi uchumi elimu kasoro madini tu,mbona wako sawa tu sisi,tunafeli wapi?
Baba kasema wote wanaohusika na mimba out! Mmoja jela mwengine kwa baba ake!
 
Hakimu Mfawidhi,
Hao wapinzani bila shaka ndio wanaowapa wanafunzi mimba. Labda benki ya dunia watumie hela hizo kuwasomesha waliyopata mimba ulaya badala ya kulazimisha wasome na watoto wakati wao ni mama watoto.
 
Sikumbuki kama awamu zilizopita kama mwanafunzi aliyepata mimba kama aliruhusiwa kuendelea na shule, mi nilikosoma ilikuwa sheria ya shule ukipatikana umezini au umepata mimba we kwaheri, ila hakuna siku raisi alisimama jukwaani kuutangazia umma na dunia kuwa watoto waliopata mimba hakuna shule sikuwahi sikia.

Kinachotuponza saiv ni ropoka ropoka ya mkuu mwenyewe alikuwa hana haja ya kutamka jukwaani pale akiwa yeye ni mkuu na ndomana saiv inakuwa taabu sasa kutengua kauli, aache kuropoka ili ashingiliwe
 
Kila siku mnajitapa eti nyie ni matajiri na kwamba na miradi mliyoanzisha mnatumia pesa za ndani.

Hilo halitoshi na kila anayewakosoa mnamwita msaliti na eti ametumwa na mabeberu.

Sasa kwa Taarifa yenu Benki ya Dunia ambayo mmeiomba mkopo inamilikiwa na mabeberu ambayo yanawatuma wapinzani kama mnavyodai.

Na Benki ya Dunia ni NGO ya Beberu lililokamaa kuliko mabeberu yote ambalo ni Marekani (CIA revealed Documents).

Sijui nyie ni watu wa aina gani msiokuwa na strategies za kesho.

Yetu macho, labda mjaribu kwa kondoo he can probably grant you the loan.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom