Kwa mkopo huu na miradi yake ni kielelezo kuwa nchi yetu haijakomaa kiutawala/kiuongozi. Haya mambo ya kukopa yatungiwe sheria inayotoa nafasi kwa BUNGE kujadili na kuidhinisha maombi ya mikopo ili kuhakikisha zinaelekezwa mahali ambapo zitaweza kukuza uchumi kwa haraka ili kupunguza mzigo kwa vizazi vijavyo! Mpango wa taifa wa miaka mitano uoneshe maeneo yenye kuhitaji mikopo sio kila kiongozi anaamua kukopa tu.
Hivi unakopa pesa kuboresha mitaala ya vyuo vikuu wakati kila kukicha wafanyakazi waliokopa bodi ya mikopo wanakatwa mabilioni kila mwezi!! yanenda wapi?
Unakopa kuboresha internet (digital) wakati kila huduma ya mtandao serikali inakata asilimia 18 kwa watumiaji kuanzia muda wa maongezi hadi bando!!
Jamani kama taifa tunaingia kwenye shida kwa tamaa ya vitu vizeri bila kuwa na uwezo
Nashauri siku nyingine serikali itupatie mchanganuo wa deni lote tujue pesa zilifanya nini
Nakumbuka nakusitika niliposikia serikali inaombwa kusamehewa deni la Urafiki na Reli ya tazara! kumbe madeni mengine ni ya zamani ila kizazi hiki ndo kinaumia kulipa!!