Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati

Tanzania tupo $ 1,063.Bado sana kufikia Uchumi wenyewe wa kati .Uchumi wa kati ule wenyewe unaanzia $4,046
 
Dah! Ahsante, unajua nilikuwa kimya nikitafuta exact figure kwamba ni ngapi hasa! Sasa kama ndo kwanza $1063, an increase to less than $100, basi kwa speed hii tutafika 2030 lakini bado high middle income ikawa mbali sana kwetu kuifikia!!!
You can change your earlier thoughts I presume.
 
Tangu mwaka 2015 adui wa Tanzania ni

1.Chadema
2.Ujinga
3.Maradhi
4.Umasikini

Kikwete ni ccm kama Magufuli na USD80 za Magufuli zimetosha kuwafanya mabeberu waunge mkono juhudi na kuitangaza Tanzania kuwa sasa ina uchumi wa kati.
 
Unawabishia WB?!
 
Kumbe na wewe mchawi.
Mimi msema ukweli,acheni kudanganya watu. Kwanza ukilinganisha Gain kipindi cha JK ni kubwa kama mara mbili na robo zaidi ya kipindi cha JPM. Tumieni akili sio kupelekwa pelekwa tu.
 
Mimi msema ukweli,acheni kudanganya watu. Kwanza ukilinganisha Gain kipindi cha JK ni kubwa kama mara mbili na robo zaidi ya kipindi cha JPM. Tumieni akili sio kupelekwa pelekwa tu.
Wewe ufipa tulia, Dkt Magufuli kawekeza zaidi kwenye miundombinu likewise JK ila mianya ya rushwa kwa JK ilikuwa mikubwa
 
Watu bado tuna shadadia sana hata hatuendi kwenye ukweli..uchumi wa kati tuliopo ni lower middle ...daraja la chini ...
Hatujafikia nchi kama India na Brazil ...wapo uchumi wa kati lakn daraja la kwanza.
Hivyo tusipojitahdi tunaweza kurudi tena nyuma ....
 
ELEWENI 2014, GDP per capita ya #Tanzania ilikuwa $ 1,030 IKASHUKA ikawa $947 2015. Leo tunambiwa tuko $1,090. Tumepanda kwa $40 Kwenye miaka 6. Tunashukuru sana Mh. Rais. Tukiendelea hivi 2025 GDP per capita itafika $1,130. Kwa mwendo HUU tutakuwa tajiri baada ya miaka 150.🙏🏾.

Kwa sasa inaonyesha kila mnyonge wa tanzanai ana uhakika wa kupata shilingi 7000 kwa siku a kwa mwezi zaidi ya shilingi 205,000. Katika pato hilo ndio mtanzania huyo alipe kodi, ada, chakula, umeme, maji, afya na nk

Tujitafakari ni kweli?
 
Kufuatia hatua hiyo, Rais Magufuli amepongeza Watanzania wote!

Sijui wapinzani watatokea wapi safari hii
View attachment 1494549
Serikali itazikubali hizi takwimu? Kuna nyakati WB ikitoa takwimu za kuonyesha kuwa ukuaji wa uchumi wa Tanzania umepungua watu wanapinga na kufura kama kifutu! Utakutwa WB wanaitwa majina kama 'mabeberu' na mengine kama hayo! Kama mnakubali takwimu hizi kubalini pia wanaposema yasiyowaoendeza.
 
Ulishaambiwa kati ya watu wakikwambia kitu usiamini wote wapo ccm na kinara ni kiongozi mkuu
 
Sasa angekuwa amevuruga si ingeshuka??ebu acha ujinga na upumbavu
 
Reactions: Oii
Hii ni hatua nzuri, pongezi kwa watanzania na serikali ya awamu ya tano. Watanzania tusibweteke, ni imani yangu serikali itakayoundwa baada ya uchaguzi itakuwa na watu makini sana ambao watakao tusaidia kusonga mbele zaid.
Kitu kinachotukwamisha ni katiba tu. Sio serikari ya awamu ya nne,tano au awamu ya kumi.tatizo ni katiba tu
 
Rais muongo huyu. Hapa wajinga watajua tumefika level moja na South Africa yenye GDP ya $6,606 wakati sisi tuna $ 1,063.
 
Tatizo lako ulikuwa unalinganisha kwa miaka 5 ya JPM wakati huna figures za 5 years. I am sure figures za 2019 and 2020 zikitoka kutakuwa na mafanikio mazuri Zaidi, usiwe na haraka yoyote yataonekana tu. Kilicho chini ya jua hakijifichi.
Chifu, nimelinganisha data za miaka mitano mitano!

From 2005 to 2010, From 2010 to 2015, from 2015 to 2020. Mbona hujahoji hiyo ya kuanzia 2005?! Btw, hata hiyo miaka 4 ya JPM kuna nini wakati gni ilishuka from $980 to $970?!

Halafu unadai figures za 2019 na 2020 zikitoka kutakuwa na mafanikio mazuri... figures zipi tena! Hebu shusha pumzi kisha tafakari! WB wamesema low middle income inaanzia 1036, lakini 2018 figure ni 1020! Sasa wameiwekaje kwenye low middle income kama figures za 2019 hazijatoka wakati za 2018 zisingeifanya nchi kuwa kwenye Low Middle?!

Na hapa usisahau kwamba tunazungumzia fiscal year.... kwahiyo figures kuanzia July 2020 zitakuwa accounted kwenye next fiscal year. Za 2019 zimeshatoka na ndizo zimeifanya Tz kutoka kwenye 1020 to Low Middle
 
Kitu kinachotukwamisha ni katiba tu. Sio serikari ya awamu ya nne,tano au awamu ya kumi.tatizo ni katiba tu
Takwimu tu mnashindwa kusoma itakuwa katiba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…