Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati

Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati

Unajua mtaji wa CCM ni waTz ambao hatupendi kusoma. Sijaona uzi mzima watu wakiomba methodology, au classification basis ya hizo takwimu. No wonder hamshangai Zimbabwe ni middle income!!.

Tupende kusoma wanaJF

Kuna wakati najiuliza zitto junior nia na dhamira yako ni nini? Hata kama wewe ni mpinzani kisiasa, ni aibu kuwa na mawazo yaliyomo kwenye hoja yako hapo juu (underlined). Una maana gani kama siyo kutusi jamii, au wewe ndiye hupendi kusoma?

Kwa suala la WB kuiorodhesha Tanzania kwenye nchi zenye kiwango cha chini cha Kipato cha Kati, si jambo la kubeza, ila la kila Mtanzania, kutambua fursa zilizopo za kukuza uchumi binfasi na wa Taifa kuelekea Uchumi wa Kati. Kama wewe ni mwanasiasa, basi kuweka Sera na Mikatati ya maendeleo (Kijamii, kisiasa, Kiuchumi na Kiteknolojia) ambazo zitalinda na kuendeleza kiwango hicho cha "Kipato cha Kati", na si kubishana kama ni kweli au
La.

Tabia ya kupinga kila jambo na/au kujadili matukio inawaondoa kwenye masuala ya kitaifa ili Chama kikubaliwe na wananchi. Hivyo nategemea, Mkuu zitto junior na wenye tabia na mawazo kama yako, utatafsiri mafanikio ya Tanzania kupanda kwa Kipato cha Kati kwa vitendo ili kufikia " Middle Income" kama Zimbabwe uliyoifagilia.

Unanilazimisha kusema yasiyohusika na mada kuu, kwamba viongozi unaodhani wana uwezo wa kuipandisha Tanzania kiuchumi ndio hao wenye tuhuma za ufisadi, uzinzi na ulevi wa kupindukia!!!
 
Chadema bana sijui nani aliwaroga. Yaani mabeberu wakituponda wao wanafurahi ila wakitusifia wanachukia .. Si mwende misitu ya Kongo huko mkaanzishe nchi yenu muishi mnavotaka
 
Leo 1 of july 2020 Tanzania imeingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati "middle income economies "

Tanzania imeweka rekodi hii haraka kuliko ilivyotarajiwa hapo awali

Benki ya Dunia na taasisi nyingine duniani zimeendelea kumwaga sifa za pongezi kwa Rais Magufuli kwa kuongoza vyema Tanzania kupeleka uchumi wakati

Sisi ni matajiri

Soma pia: World Bank to officially declare Tanzania a Middle Income Country (MIC) on July 01, 2020

============

View attachment 1494690View attachment 1494691

Safi sana Mungu Ibariki Tanzania
World Bank Country and Lending Groups – World Bank Data Help Desk
 
Natamani Angekuwepo anaeweza kumzid JP,
Sema hayupo..
JP anajitahid ila sio sanaa, bado bado

Shida ni kwamba anae mzidi hayupo, kwahiyo aendelee tu kuongoza.

SISI WENYEWE WATANZANIA hatufanyi upinzani wa juu.

Natamani JP angekua Bayern München.

Sema ndo hivo Yeye ni Aston Villa na wapinzani wote ni daraja la mwisho.
 
Kama Watanzania tumefurahi sana kuona Tanganzo la Rais mpendwa John Magufuli kutoka bank ya mabeberu, yaani Bank ya Dunia wakitusifia kuwa tumepanda kuwa nchi ya kipato cha kati.

Wengi tumejaribu kuangalia kwenye website yao hiyo habari bila mafanikio.

Tunaomba mwenye reference atupe link ili tulio Ulaya tuwatambie watanj zetu na wengine wanaotuchukulia poa.
 
Leo 1 of july 2020 Tanzania imeingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati "middle income economies "

Tanzania imeweka rekodi hii haraka kuliko ilivyotarajiwa hapo awali

Benki ya Dunia na taasisi nyingine duniani zimeendelea kumwaga sifa za pongezi kwa Rais Magufuli kwa kuongoza vyema Tanzania kupeleka uchumi wakati

Sisi ni matajiri

Soma pia: World Bank to officially declare Tanzania a Middle Income Country (MIC) on July 01, 2020

============

View attachment 1494690View attachment 1494691
Hata mpango naye ameingia kwenye hizi ghiliba? sisi tunatajwa tuko kwenye lower-middle? Lower middle ndio uchumi wa kati?
 
Uchumi wa kati ni kipato cha wastani wa kuanzia dola 1,036 ambayo ni sawa na shs takribani milioni 2,500,000 kwa mwaka.

Mtanzania wa kawaida mnyonge ni kweli anapata kipato kinachofika takribani shilingi 7,000 kwa siku na kwa mwaka shilingi 2,500,000?

Kufika uchumi wa kati unaotangazwa ni kweli ndio hali halisi au makaratasi yanayopelekwa bemki ya dunia yamedanganya?

Ati, makaratasi yanayopelekwa benki ya dunia yamedanganya, kana kwamba benki hiyo ina VIHIYO ila wewe Return Of Undertaker ndiye bingwa wa uchumi, du!

Unauliza swali hilo ukiwa na fikra hasi dhidi ya Serikali iliyoko madarakani au kwa kutokujua vigezo vinavyotumika.

Kwa uelewa wako huo potofu, kwamba hakuna Mtanzania mwenye kipato cha chini anayepata 7,000/- kwa mwezi, ni wazi hujui unalolisema. Kiwango cha Pato hakitafsiriwa kwa kipato cha mtu katika fedha tu ila ni pamoja na unafuu anaoupata kwenye gharama za huduma za jamii km afya, elimu, maji, nishati nk.

Mathalani Elimu kwa sasa ni bure na wanavyuo wanapata mkopo. Huduma za afya siyo tu zimeboresha ila matumizi ya Bima ya Afya kunampungizia mwananchi gharama za matibabu. Isitoshe miundo mbinu iliyo bora na imara inapunguza gharama za usafiri, nk.

zitto junior
tindo
Chige
 
Magu amesha-tweet kwa 'kidhungu' kushukuru!!

Tusubiri magazeti ya kesho na heading watazokuja nazo.

Wakiona watu wanafanya uchambuzi kwa kutumia data mitandaoni,wanatamani wawamalize maana wanaharibu uhundo!!
 
Basi sawa
tapatalk_1593528776616.jpeg
 
Leo 1 of july 2020 Tanzania imeingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati "middle income economies "

Tanzania imeweka rekodi hii haraka kuliko ilivyotarajiwa hapo awali

Benki ya Dunia na taasisi nyingine duniani zimeendelea kumwaga sifa za pongezi kwa Rais Magufuli kwa kuongoza vyema Tanzania kupeleka uchumi wakati

Sisi ni matajiri

Soma pia: World Bank to officially declare Tanzania a Middle Income Country (MIC) on July 01, 2020

============

View attachment 1494690View attachment 1494691

Ni LOWER MIDDLE INCOME jamani sio
Middle Income.

Kuna tofauti kubwa hapo.
 
Wakitupiga za uso wanaitwa majina yote, wakitusifia tunakenua mpaka jino la mwisho.
Btw, hivi kuingia uchumi wa kati (whatever it means) inabidi "watutangazie"? Yaani bila kutangaziwa huingii? Lakini si tulianza kujiita nchi tajiri, sasa hili tangazo "lao" kwa nini litupe raha hivi?
 
Tanzania GNI Per Capita 1990-2020
Hizi data wengi wana zinatufundisha nini? GNI ilikuwa vizuri zaidi miaka 1995 hadi 2005 wakati wa mkapa, pia wakati wa kikwete lakini pia GNI ilikuwa kwa1% tu mwaka 2015, maana yake kulikuwa na anguko/ mdororo wa uchumi mwaka 2015 ambapo effect hiyo iliendelea hadi mwaka 2016 ambapo GNI ilikuwa kwa hasi ndio tena ika pick up in 2017 na 2018, suala la kujiuliza ni kwanini GNI uchumi uliyumba mwaka 2015 hadi kupelekea kuwa na effects katika miaka iliyofuata? so tukisema kikwete uchumi ulipaa ndio na tujue pia mdororo ulianza katika kipindi hicho hicho cha mwisho wa uongozi wake na hivyo aliyempokea lazima kutakuwa na ugumu wa kuanza kufufua uchumi na kuweka musingi upya.

Mkapa Ukiangalia data zote ndio Rais pekee aliye rithi uchumi mbovu na kuleta mageuzi makubwa , ni kipindi chake tu ambapo GNI ilikuwa hadi by 22% lakini mwaka 2001 pia ulishuka nadhani kwa sababu ya effects za uchaguzi za mwaka 2000 na issue za zanzibar , so Magufuli tayari amesha ufufua uchumi kinachotakuwa ni kuongeza kasi na kumantain asishuke.
 
Ukweli uko hivi:

Tanzania imeingia kwenye list ya LOWER MIDDLE INCOME COUNTRY
Na sio MIDDLE INCOME COUNTRY kama wanavyodanganya.

NENO LOWER linaharamisha hizo shamrashamra zao.

Anyway ni mwaka wa uchaguzi lazima wadanganyika wasioelewa wapigwe tu.

Yaani nchi imejaa mazuzu mpaka aibu.

Tungekuwa tumeingia middle Income ingetupasa kuanzia sasa hatuombi tena nje na mara nyingi manunuzi yetu nje ni CASH.

Budget yetu ingepaswa kuwa haina utegemezi 100% na tungekuwa tunalipa madeni sana tunayodaiwa nje.

World Bank Country and Lending Groups – World Bank Data Help Desk

Ngoja niishie hapa....nivae na barakoa yangu.😷😷😷
 
Zambia, Zimbabwe, kenya, cameroon, comoros, senegal, ivory coast, gabon, ghana, lesotho, etc Zote zimo kwenye huo uchumi wa kati tunaojivunia.
Lower middle yaani nchi haipo kwenye nchi zinazohitaji msaada wa dharula
 
Ukweli uko hivi:

Tanzania imeingia kwenye list ya LOWER MIDDLE INCOME COUNTRY
Na sio MIDDLE INCOME COUNTRY kama wanavyodanganya.

NENO LOWER linaharamisha hizo shamrashamra zao.

Anyway ni mwaka wa uchaguzi lazima wadanganyika wasioelewa wapigwe tu.

Yaani nchi imejaa mazuzu mpaka aibu.

Tungekuwa tumeingia middle Income ingetupasa kuanzia sasa hatuombi tena nje na mara nyingi manunuzi yetu nje ni CASH.

Budget yetu ingepaswa kuwa haina utegemezi 100% na tungekuwa tunalipa madeni sana tunayodaiwa nje.

Ngoja niishie hapa....nivae na barakoa yangu.😷😷😷
Hivi ukienda kwenye kampeni ukawaeleza watu kuwa nchi yetu imefikia uchumi huo watakulewa wakati hawana maji,umeme,madawa hospitalini,mishahara duni,madeni ya ndani hayalipwi,n.k?
 
Back
Top Bottom