Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati

Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati

Mwisho wa siku swali ni mmoja tu, je hizo taarifa au acquired status "middle income country" vina impact gani kwenye maisha ya kawaida ya mtanzania anayeishi Dabaga, Iringa?
 
Rais Magufuli atatufikisha tu kama ndani ya miaka minne ametufikisha uchumi wa kati haitachukua muda kumfikia USA
 
Hivi Magufuli ndiye aliyetangaza TZ kuwa middle income au ni WB? Kwa nini anashambuliwa Magufuli?

Watanzania ni wachofu wa kufikili hasa bavicha, wanapenda upambe kwa nchi zingine tu, wanasahau kuwa ni wajibu wao kukuza huo uchumi.
Leo mtu anashangaa wakati wazazi wake wako kwenye madaraka muda mrefu na yeye ni zao la hayao mapungufu alafu ajifanya kushangaa.
 
Hivi kwanini issue kama hzi lazima siasa ziingie? Hatujiamini au ndio ulimbukeni? Issue ya kinchi lakini kwenye mijadala ni chadema na ccm dadeki😆😆😆
 
ELEWENI 2014, GDP per capita ya Tanzania ilikuwa $ 1,030 IKASHUKA ikawa $947 2015. Leo tunambiwa tuko $1,090. Tumepanda kwa $40 Kwenye miaka 6. Tunashukuru sana Mh. Rais. Tukiendelea hivi 2025 GDP per capita itafika $1,130. Kwa mwendo HUU tutakuwa tajiri baada ya miaka 150-Fatma Karume on twitter

Tafsiri halisi ya uchumi sio Per Capita GDP peke yake, kuna mambo mengi, kuna PPP, A variety of measures of national income and output are used in economics to estimate total economic activity in a country or region, including gross domestic product (GDP), gross national product (GNP), net national income (NNI), and adjusted national income (NNI adjusted for natural resource depletion – also called as NNI at factor cost). All are specially concerned with counting the total amount of goods and services produced within the economy and by various sectors.. So uchumi haina hesabu ya straight line
 
Ni sawa na kumwambia mwanafunzi akatafute ujuzi wa kilimo cha korosho Kilimanjaro halafu aka apply huo ujuzi Singida! It's irrelevant maana tunajua kilimo hicho kipo Mtwara.

Huwezi kwenda kujifunza Singapore maana wao wana sera tofauti za uchumi na siasa, wako eneo tofauti kijiografia na hatuendani kwa chochote, vipaumbele katika uzalishaji ni tofauti, number ya population ni tofauti, majirani waliomzunguka kiuchumi na kisiasa wako tofauti na waliotuzunguka sisi pia.

Singapore sio darasa sahihi. Tuumize kichwa humu humu ndani kwa kuendelea kuboresha sekta zetu za uchumi na uzalishaji. Pia kujiwekea miradi ya mkakati ya kuchochea na kuibua sekta nyingi zaidi.
 
Ndugu maisha yako yamekuwa bora kiasi gani pamoja nakushangilia hizo porojo
 
Kuna mtaalamu wa uchumi aliletwa toka Vietnam aje awafundishe uchumi lakini alipofika akatushangaa akasema wao hawalimi korosho ila wana viwanda vya kubangua korosho tatizo sio kwenda Singapore bali ni mfumo mbovu wa elimu yetu na product tunayotoa toka kwenye elimu yetu.
Sijafika Singapore ila najua wao wamefanikiwa kupitia bandari zao lakini sisi tuna bandari ngapi na tunazifanyia nn
 
Back
Top Bottom