Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati

Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati

Huyu chige jana kaja na data nyiiingi kuhusu uchumi hadi unajiuliza kama anajua mambo yote haya mbona hatusikii ni muhadhiri mwandamizi wa uchumi Harvard University 😀😆😀

Chige ni fake I'd. Unaweza kukuta ni governor mstaafu Ben Ndulu, who knows?
 
Hupenda na kuheshimu fikra/hoja za binadamu mwenzangu zilizo pevu na fikrishi tu.
 
Leta data,unafikiri tutawahi kwa uongouongo na ulaghai?acheni kutumia ujinga wa watanzania kuendelea kuwadanganya!!
 
Mabeberu leo wameeleweka juu ya hili suala,sijasikia zile kauli zao tuwe makini na mabeberu hawaitakii mema nchi hii.
Au CCM wataichukua hii taarifa ya mabeberu ajili ya Kampeni katika uchaguzi mkuu.

Mkuu ccm wanatembea na neno uchumi wa kati, hawahitaji kuchakata hiyo taarifa, na hii mitandao ya kijamii ndio inawatilia ndimu kwenye jicho. Si unaona mpaka Yesu katweet kuwa tumeshaingia kwenye uchumi wa kati. Ila hata Yesu mwenyewe akiingia humu mitandaoni akute jinsi MATAGA wanavyorushwa kichura, ni lazima aagize lile jeshi la akiba la watu wasiojulikana likae mguu sawa.
 
Kwani mbona Mh.Zitto Kabwe amekuwa kimya na sio kawaida yake. Mpaka sasa hajasema kitu? Hata shangazi Fatma nae kimya?
 
Kama hutanyi kazi kwa bidii na kama hufanyi shughuli yeyote maalumu ya kukuingizia pesa lazima uendelee kulia lia kwenye mitandao lakini kimsingi wanaochapa kazi tofauti wanaiona..

Mwezi huu ni msimu wa ufata na wakulima wa ufuta mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dodoma, Manyara, Katavi na Rukwa wanafaidi mamilioni kwa minada inayoendeshwa online na TMX..

Majuzi tu nilikuwa vijiji vya Masasi na Nanyumbu jamani hali huko vijijini imeimarika sana, mwezi June na July wanakula ya Ufuta, mwezi August na September wanakula mbaazi alafu kuanzia wa kumi hapo wanakula babalao mwenyewe korosho. Sijazungumzia kuanzia March mpaka May walikuwa wanafaidi pesa ya choroko..

Jamani fanyeni kazi, pesa ipo na wapiga kazi wanatengeneza pesa. Kama wewe unategemea Magufuli atakuletea pesa hapo Manzese au Tandale unajidanganya, rudi kijijini kashike jembe utaacha kulaumu laumu na kupinga kila jambo..
 
Taarifa ya Benki ya Dunia kwamba Tanzania sasa imeingia katika kundi la nchi zenye uchumi wa kati imepokelewa kwa furaha na wananchi wengi japo wapinzani wachache hawajafurahishwa.

Niseme tu hili siyo swala la kiitikadi bali ni jambo jema kitaifa.
Taarifa hii ni ya WB siyo ya CCM wala Twaweza na WB wana data za uhakika za uchumi kuliko chama chetu kikuu cha upinzani yaani Chadema.

Chonde chonde wananchi tushirikiane na serikali katika kuukuza na kuulinda uchumi wetu..... Tusije tukaporomoka.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kwani mbona Mh.Zitto Kabwe amekuwa kimya na sio kawaida yake. Mpaka sasa hajasema kitu? Hata shangazi Fatma nae kimya?
wale ni watu wa data wanafanya kwanza analysis wanakuja cyo kama hawa ccm timu ya kusifu na kuabudu
 
Mkuu zitto junior, hongera kwa kujibu hoja kwa hoja. Tukijenga utamaduni huu ndani ya JF, litakuwa jukwaa maridhawa siyo tu ya kuhabarisha lakini pia kuelimishana.

Nikirejea kwenye hoja yako kuhusu tafsiri au maana ya uchumi wa nchi, kiasi Mkuu zitto junior nakubaliana na wewe kama ifuatavyo.

Vigezo vinavyotumiwa na Benki ya Dunia kiuchumi msingi wake ni fedha ambayo kwa namna nyingi inasemekana kuwa ni kipimo hafifu ambacho hakionyeshi hali halisi ya maisha ya mtu binafsi. Kwa sababu hiyo, hakifai kutumika kutofautisha kati ya uchumi mkubwa "Macro economy" na mdogo "Micro economy".

Licha ya ukweli huo, hoja hiyo kwa ujumla ni chanya na inapaswa kupongezwa. Kwa upande mwingine ni wito kwa Serikali kuweka mikakati mizuri ya kiuchumi ili kukua kwa Kiwango cha Pato kuonekane na kugusa ngazi zote za jamii (micro & macro levels) na kila eneo la kiuchumi, kadri iwezekanavyo.

Tunapoingia kwenye Uchaguzi Mkuu, nategemea viongozi wa vyama vya siasa, wanasiasa na wagombea hawatajikita kujipongeza au kubeza kuhusu uamuzi wa Benki ya Dunia kuiorodhesha Tanzania kwenye nchi ya Uchumi wa Kati. Watumie taarifa hiyo kuweka Sera zinazoweza kutekelezeka ili uchumi wa Taifa uimarike na kugusa maisha ya kila Mtanzania.
 
Mtu anayepiga GPA ya 3.1 huwezi kumuita kilaza
Haimaanishi chochote hata Zimbabwe, Zambia, Djibout wapo pia huu ni upepo wa kawaida wa nchi zote maskini kuinuka kigodo kwa sababu ya mabadiliko ya kiuchumi duniani kwa ujumla wake. Jiwe hajafanya chochote kwa mkulima wa Tanzania.
 
Sisi ni nchi Tajiri....maendeleo si ndiyo utajiri mkuu?
 
It is a scientifically proven economic analysis by World Bank. Haina longolongo tufurahie wote. Your right
 
Kwa takwimu hizo, ni ushahidi tosha kwamba JPM amevuruga uchumi, na JK was far better compared to JPM.

Taarifa hiyo ya Benki ya Dunia inasema kwamba:- Kwa maana nyingine, hatimae ndo tumefika kwenye $1036+!!'

Ukiangalia WB Secondary Data, unakutana na hii kitu (GNI per capita by Atlas Method).
View attachment 1494559

Kumbe, 2015 GNI Per Capita by Atlas Method ilikuwa $980. Kwa maana nyingine, kwa miaka 5 mzima, JPM alikuwa anahangaika kuivusha GNI per capita from $980 to $1036... a difference of ONLY $54.

Kinyume chake, GNI Per capita in 2010 ilikuwa kama ifuatavyo:-
View attachment 1494564

Utaona hapo, in 2010 GNI per capita ilikuwa $720, na kwa maana nyingine, GNI per capita ilipanda from $720 in 2010 to $980 in 2015! Yaani ilipanda kwa $260, wakati miaka 5 ya JPM imepanda around $54+!

On top of that, mwaka 2005 GNI per capita ilikuwa $500, na kwa maana nyingine, miaka yake 5 ya kwanza, Mzee wa Msoga alipandisha GNI per capita from $500 in 2005 to $720 in 2010... yaani $220 wakati JPM miaka 5 yake ya kwanza inaonesha kapandisha for less than $100.

View attachment 1494576

Ama kweli mtaji mkubwa JPM ni Jeshi Kubwa la Wajinga lililopo nyuma yake! And JPM anafanikiwa haya kwa sababu ile ile niliyowahi kuitaja siku za nyuma: Tanzania is full of people with average mind, and many more below the average!
Watu hawaongezeki?
 
Pia masikini huyo huyo akipata ugonjwa wa moyo tajiri humukebehi huyu nae kapata ugonjwa wa moyo akidhani ugonjwa wa moyo Ni kwa tajiri peke yake
 
Back
Top Bottom