Unazungumziaje kupanuliwa na kuboreshwa kwa huduma za jamii na miundo mbinu km za usafiri, katika kuchangia kupunguza gharama za matumizi (siyo kipato) kwa mwananchi mmoja mmoja, kaya na jamii kwa ujumla, sekta ambazo awamu zilizopita hazikutilia maanani?
Chifu...
Upo tayari kuusikia ukweli na kuukubali lakini?! Ni matumaini yangu hautakuwa kama Wafuasi wa Magufuli ambao huwa hawautaki ukweli! Watakuja huku wamejivika ngozi ya kondoo lakini wakiambiwa ukweli tena wenye ushahidi wote, wanaanza ku-panic na matusi juu!!
Kama upo tayari kuusikia ukweli na kuuvumilia, ukweli wenyewe ndo huu hapa chini lakini unahitaji kuwa mvumilivu wa kusoma post ndefu!
Tukianza na suala la Huduma za Jamii! Kwa sasa sitaweka reference lakini nitaweka detailed info ili ukitaka kutafuta uthibitisho, itakupa urahisi kufanya hivyo with few clicks on the web.
Suala la Huduma za Jamii, kwa maana ya Huduma za Afya, wanaotakiwa kushukuriwa ni wafuatao, kwa uzito from top bottom:-
1. MABEBERU... IMF, WB na Paris Club
2. Benjamin Mkapa
3. JK na JPM.
MAELEZO:-
Mwaka 1995 Mabeberu walikubaliana kufuta madeni kwa nchi maskini zaidi lakini kwa masharti. Baada ya majadiliano, wakaona nchi 38 (or 28 sikumbuki sawasawa) ndizo zifutiwe kwa masharti kwamba, lile fungu ambalo walitakiwa kuwalipa Mabeberu walielekeze kwenye huduma za jamii na kuondoa umaskini wa kipato kwa wananchi... yaani income poverty.
Programu husika ilifahamika kama Highly Indebted PoorestCountries- HIPC. Uki-Google hiyo keyword utapata taarifa za kutosha. Sharti la kwanza ambalo Mabeberu walitoa, ni selected countries kuonesha nia ya kulipa... yaani over specified time, walipe kiasi fulani.
Kwa waliokuwa na uelewa kidogo enzi za Mkapa watakumbuka Utawala wa Mkapa ulishitumiwa sana ndani kwamba badala ya kushughulikia kero za kitaifa, amewekeza nguvu kwenye kulipa madeni! Watu ambacho hawakufahamu, Mkapa alikuwa anatekeleza hilo sharti la kuonesha nia ya kulipa.
Na kweli, Mkapa alifanaya vizuri sana kwenye zoezi la ulipaji, na hatimae Tanzania tukawa approved.
Kama ulikuwa na akili kidogo, nadhani enzi zile ulikumbuka the so-called Mkakati wa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini Tanzani- MKUKUTA.
MKUKUTA ika-highlight maeneo ya kuyafanyia kazi kutokana na sharti hilo la Mabeberu. Priority ya kwanza ikawa kuongeza ACCESS to Education. Nimeweka "access' in capital letter kwa sababu lengo ilikuwa ni kuanza kwanza na access (quantity) ndipo lije suala la quality.
Hapo ndipo zikazaliwa Shule za Kata. Zikaanza kujengwa kila mahali bila kujali kama kuna walimu au hapana! Mkapa alianza tu na ujenzi wa Shule za Kata na muda wake ukaishia kijiti akapokea JK! Shule za Kata zikaenea nchi mzima, lakini hapakuwa na walimu wa kutosha!
Baada ya kukamilisha suala la access kwa kujenga mashule kote nchini, ndipo JK akageukia suala la quality kwa maana ya kupata walimu wenye sifa! Kama utakumbuka, baada ya hali kuwa mbaya zaidi, akaanza na kile kilichokuwa kinaitwa Walimu wa VodaFasta.
Kutoka kwenye Vodafasta akaongeza udahiri wa walimu maradufu! Kwa bahati mbaya Utawala wa JK ukagundua kwamba watu hawataki kwenda kusoma ualimu. Wakaamua kutoa incentives.
Incentive ya kwanza ni kuwahakikishia wale wote watakaoenda kusoma ualimu wataajiriwa na serikali. Incentive ya pili ilikuwa kubadili madaraja ya mishahara kwa walimu! Kwa mfano, wakasema Mwalimu wa Sayansi atalipwa sawa na mtumishi yeyote serikalini aliye kwenye taalamu ya kisayansi.
Hali kadhalika, walimu wa biashara na sanaa itakuwa hivyo hivyo, na sio kwamba mtu wa BSc. Environment Science analipwa laki 7 lakini mwalimu wa BSc. Education analipwa laki 4.5.
Na incetive ya tatu ilikuwa kuwahakikishia mikopo ya elimu na ajira.
Incentives zote tatu zilisaidia sana na madogo wakaanza kumiminika vyuo vya elimu kwenda kusoma ualimu na majority ya hawa walikuwa wanaajiriwa.
Mkakati huo ukaja kukumbwa na changamoto ya wanafunzi wachache sana wanaoenda kusoma Ualimu wa Masomo ya Sayansi. Hapa zikatolewa incentives za kila aina including kuwaita ma-jobless waliopo tu mtaani lakini wamemaliza Form VI miaka ya nyuma kwa masomo ya sayansi.
Hapo tena serikali ikawahakikishia kuwasomesha BURE kwa ngazi ya Special Adanvanced Diploma miaka mitatu na guarantee ya ajira!!
Bado serikali ikagonga mwamba kwa sababu waliojitokeza walikuwa wachache sana. Kutokana na hilo ndipo ikaanzishwa ile Special Diploma (Science & Mathematics) ambayo JPM alipoingia tu madarakani akaifuta na kusema waliochukuliwa ni vilaza. Kaleta alternative ipi kukabiliana na uhaba wa walimu wa sayansi... ONLY GOD KNOWS!
Na katika kukamilisha suala la quality, mwaka wake wa mwisho ndipo likaanza zoezi la ujenzi wa maabara nchi nzima!
Nasikia na hizo maabara Magu kazipiga chini.
JK muda wake ukaishia akaingia JPM ambae nae alitakiwa kuanzia alipoishia JK. Remember, priority ya kwanza ya MKUKUTA ilikuwa ni elimu na priority ya pili ilikuwa kuondoa umaskini wa kipato na huduma za afya. Zingine ni food security na huduma za maji.
Kwenye umaskini wa kipato ndipo ilizaliwa TASAF. Kwahiyo JPM alipoingia ndipo akaanzia kwenye huduma za afya, na kuendeleza suala la huduma za maji!!
Huo ndo ukweli wenyewe, hata kama serikali zilizopita zilikuwa hazipiti mbele kwa tambo!!!
Lakni hata ukija kwenye huduma za usafiri!! Are you serious kwamba JPM ndie amedumisha huduma za usafiri kuliko wengine wote?! Hivi huyu JPM alifahamika fahamika vipi Tanzania mzima kama sio safari zake za mara kwa mara mikoani wakati akiwa Waziri wa Ujenzi?
Sasa ikiwa pamoja na yote hayo bado mnaamini wengine woooote hawakufanya hawakutilia maanani sekta ya kijamii except JPM, sina cha kuongezea kwa kweli!
Kikubwa alichofanya JPM kuwazidi wenzake ni kununua ndege na ujenzi wa reli. Na hapa tusisahau ujenzi wa SGR ulikuwa mradi wa awamu iliyopita, lakini alipoingia JPM akapiga chini mpango mzima kwa madai kulikuwa na rushwa!!
Lakini ukisoma ripoti ya serikali kuhusu gharama zilizotumika hadi sasa; na yeye anaelekea kwenye gharama zile zile alizokuwa amedai watu wamepiga! Na asipoangalia, atavuka gharama zilizokuwa zimekubaliwa na mkandarasi wa kwanza!
Kwa mfano, March 01, 2020
Idara ya Habari Maelezo walitujuza kwamba:-
Serikali imetumia kiasi cha Shilingi Trilioni 2.957 kutekeleza mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa kwa kiwango cha Kimataifa (SGR) huku kasi ya utekelezaji ikiongezeka.
Je hizo takribani Trilioni 3 kwa ukubwa gani?! Wanaendelea:-
Mradi wa SGR kwa kipande cha Dar es Salaam na Morogoro umefikia asilimia asilimia 75 wakati kipande cha Morogoro Makutopora Singida kimefikia takribani asilimia 28”
Yaani 75% ya kuelekea Morogoro, na Makutupora Singida 28% lakini tayari SGR imeshabugia takribani Trilioni 3.
Kisha Dodoma Municipal Council wanatoa takwimu zingine kwamba:-
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Bw. Masanja Kadogosa amesema ujenzi wa kipande cha pili cha reli chenye urefu wa kilometa 422 utagharimu Shilingi Trilioni 4.3
Haya piga hesabu mwenyewe hapo bila kusahau suala la on and off linalotokana na ujenzi kukamilika kiasi gani na gharama zake.
Hapo juu kuna Trillion 2.957 na chini kuna Trilion 4.3; ambapo total ni Trilioni 7.26.
Au tusiimize sana kichwa! Hapo juu wanasema ujenzi wa kipande cha pili ambacho ni ONLY 422km kitagharimu TZS Trillion 4.3 wakati Mkataba ambao JPM alisema umejaa ufisadi,
Reuters wanatujulisha kwamba:-
Transport Minister Samuel Sitta told parliament on Saturday a Chinese consortium had been awarded a contract to build a 2,561 km (1,536 miles) standard gauge railway connecting Dar es Salaam port to land-locked neighbours at a cost of $7.6 billion.
Kwamba mkataba uliopigwa chini kwamba wa kifisadi ni ule ambao ungejenga kilometa 2,561 kwa Trillion 17.5 (approximate current exchange rate) na ule usio wa kifisadi utajenga kilometa 422 kwa Trilion 4.3 Trillion!!