mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,670
NImejibu... sana tu!
Kwenye post yangu ya kwanza nilizungumzia issue ya MKUKUTA na yale niliyo-highlight ndiyo hasa anayohitaji mwananchi wa kawaida. Kwa kukumbushia tu nimetaja suala la huduma za elimu, afya, huduma za maji, kuondoa umaskini wa kipato, na kuhakikisha food security.
..
Kuhusu serikali imefanya nini ndo pale niliorodhesha uboreshaji wa huduma za kijamii kutoka kwenye elimu, afya, na maji. Hata zilipojengwa zile grains reserves ni kwenye mkakati ule ule... food security!
Lakini kwenye kupunguza kama sio kuondoa umaskini wa kipato bado tunapiga mark time kwa sababu nilizotaja hapo juu!!
chige una hoja fikirishi hapo juu.
Niamini tu kwamba tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, Viongozi wa vyama vya Siasa vitakuja na Ilani za Uchaguzi zenye Sera, Mikakati na Mipangokazi ya kuwezesha Miradi Mikubwa ya Kiuchumi (Macro-economic projects) inayoendelea nchini isiwe magofu bali isaidie ukuaji wa uchumi wa ngazi za chini (Micro-economic). Ikiwezekana kuwa hivyo umaskini wa kipato utapungua
Pamoja na mapungufu kiuchumi, kama yapo, utakubaliana na mimi kwamba Serikali iliyoko madarakani imeweka misingi ya kuendeleza uchumi hata wa mtu mmoja mmoja?
Kwa mfano, swala la ajira ni uvivu wa mtu kutambua fursa za kiuchumi zinazotokana na miradi mikubwa inayoendelea nchini (km Umeme wa REA na Stiglers - Bwawa la Umeme la Nyerere , SGR, na hivi karibuni bomba la mafuta kutoka Uganda).
Isitoshe kuimarika kwa njia za usafirishaji (ardhini, majini na angani) kunatoa fursa za biashara kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa muda mfupi na gharama nafuu.
Uboreshaji na upanuzi wa huduma za jamii (elimu, afya, maji) kunaimarisha rasmaliwatu kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo wakati uleule gharama za maisha zikipungua.
KUPANGA NI KUCHAGUA (km kujenga Bandari ya B/moyo au kuimarisha zilizopo; kutumia ndege za kukodi au kununua za kwetu?; nk)