Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati

Benki ya Dunia yaitangaza Tanzania kuingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati

Huyu Bwana mkubwa kweli Mwamba. Estimet ilikuwa 2025 yeye kwa miaka tano ametupaisha. Mh Rais Hongera sana pamoja na team yako.
 
Marekani umewahi kusikia wanalalamika kuhusu maji, barabara, matibabu, shule n.k? sisi tunajidanya wenyewe, kuhusu suala la kujituma hilo halikuhusu sababu sijawahi kukuomba chochote na sitakaa nikuombe mimi binafsi wala familia yangu. Ongea vitu vyenye pointi, huo uchumi wako wa kati unasadifu maisha ya wananchi?
Kwani shida ni nini? Hutaki Tanzania kuwa uchumi wa hati au vipi? Uchumi kukua haujawahi kumaanisha wananchi watakuwa na hela mfukoni. Ndio maana nimekutolea mfano marekani ambayo ni giant kwa uchumi lakini bado kuna watu wanaishi maisha duni ndani ya hiyo nchi ambapo nilitegemea wananchi wote wangefurahia maisha. Na kiuhalisia nchi yoyote ambayo inafikia level ya uchumi wake kuanza kuwa katika level hiyo lazima wananchi wapige kazi kiuhakika ili maisha yaende vinginevyo watakuwa maskini wa kutupwa. Fuatilia Afrika ya kusini ambayo ni Giant wa Afrika kiuchumi kama wananchi wake wanapata hizo huduma zote unazozitaja. Nafikiri unakumbuka kwa nini walianza kuwafukuza waafrika wenzao na kuwadhuru wakati nchi inaaminika ina uchumi mzuri na unaokuwa kwa kasi.


Kuhusu kuniomba au kukuomba chochote hiyo ni wewe unaesema na ni msimamo wako wala mimi sikufika huko. Kwa mimi nafikri kuna kazi imefanywa mpaka kufika hapo.
 
Yaani hawa jamaa ni tatizo kweli kweli! Wengine wanakomaa eti data za kupika wakati wanaona kabisa source ni WB! Labda ni kutoelewa kwamba unapofanya trend analysis lazima uangalie data za nyuma kwa sababu ndizo zita-determine your current and future performance
Kwahiyo WB wamekosea?
Mbona hili swali hujibu?

Maana unajiiona wewe ndio umefanya analysis ya maana kuliko hao WB,!
 
Covid 19 bado Ni tishio Niko hospitali moja huku bila barakoa huingii getini. Halafu mdada mmoja aliniambia mzee wake aliugua, familia yote wakaugua
Lakini wao wanataka kuaminisha ulimwengu wote kwamba ugonjwa haupo tena!
 
Unaweza kuonesha ni wapi nimesema Magufuli ana makosa?! Watu for years now tumekua tukisema JPM anavuruga uchumi! Leo hii tumetumia data zile zile ambazo mnazikubali kuonesha ni kweli amevuruga, kwenu inakuwa nongwa!!

Btw, kwani huyo Magufuli ni nani hadi asikosolewe?! Anakosolewa Mungu seuze yeye!!

Acheni habari zenu bhana... nyie endeleeni kufurahia kwamba hatimae uchumi umekua na hivi sasa mpo uchumi wa kati lakini msitake kila mtu awe kama nyie!!
Hakuna ambaye hapaswi kukosolewa kukiwa dosari labda mtoto mchanga, kichaa na mfu. Shida yangu ni kwanini anashambuliwa Jpm kwa kauli ya kusema tujipongeze na si World bank ambao wametoa takwimu? Kwani Tanzania haijawa mentioned kuwa nchi zinazoingia uchumi wa kati?
 
Kutokula wewe haimaanishi mimi sili. Marekani ni nchi namba moja kwa uchumi duniani unafikiri wote wanakula na kulala pazuri? Unafikiri kwa nini baadhi ya wamarekani wanalalamika na kuandamana kuwa ajira zimepungua? Fuatilia utajua nini maana ya uchumi wa nchi kukua. Usipojituma na kufanya kazi hata marekani huli mkuu .
Kakurushia kikofi ukakikwepa,upper cut uliyomrudishia anaugulia nayo,aje atwambie IMEMUINGIAJE.
 
Hakuna ambaye hapaswi kukosolewa kukiwa dosari labda mtoto mchanga, kichaa na mfu. Shida yangu ni kwanini anashambuliwa Jpm kwa kauli ya kusema tujipongeze na si World bank ambao wametoa takwimu? Kwani Tanzania haijawa mentioned kuwa nchi zinazoingia uchumi wa kati?
Sasa wapi nimemshambulia JPM?!

Kuna mahali nimesema Tz haijaingia uchumi wa kati?!

Hivi nimesema TZ haijaingia kwenye low middle income level au nimesema kwa GNI per capita aliyoikuta tulitakiwa tumeingia kitambo na badala yake, GNI per capita badala ya kupanda ikawa inashuka na ku-stuck kama ambavyo tumekuwa tukisema mara kwa mara kwamba JPM anaharibu uchumi!

Shida yenu hamtaki kusikia watu wakisema Magufuli anafanya vibaya, and that's it! Na wakati wengi wenu mkisema tumefikia malengo kabla ya muda (2025) lakini ukweli ni kwamba hatujafikia kwa sababu Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2025 umetaja target kwa figure; na kwa speed hiyo hatuwezi kuifikia!!

Na wataalamu waliokuwa wameweka target figure walifanya hivyo makusudi kwa sababu wanajua hivi vigezo huwa vinabadilika mara kwa mara lakini ukifika higher target, unakuwa na uhakika kwamba hata vigezo vikibadilika, huenda kwa "figure hii" bado tutakuwa tunacheza kwenye low middle income!
 
Leo 1 of july 2020 Tanzania imeingia rasmi katika orodha ya Nchi zilizo katika uchumi wa kati "middle income economies "

Tanzania imeweka rekodi hii haraka kuliko ilivyotarajiwa hapo awali

Benki ya Dunia na taasisi nyingine duniani zimeendelea kumwaga sifa za pongezi kwa Rais Magufuli kwa kuongoza vyema Tanzania kupeleka uchumi wakati

Sisi ni matajiri

Soma pia: World Bank to officially declare Tanzania a Middle Income Country (MIC) on July 01, 2020

============


Hii benk ya dunia iko kisiasa sana Nayo imekutana lini na watanzania ikagundua wanachopitia
 
FAKE NEWS! Sijaona source ya habari hii kutokea World Bank yenye jina la one of the WB’s top officials with authority to issue this report.
 
Hizi ni mvua za rasha rasha tu, tutakapomaliza SGR hadi Dodoma na Bwawa la Mwl Nyerere kuna watu itabidi wahame Tanzania kwa aibu.

1593706497780.png

 
1593707277134.png


Hapa kazi tu, ngoja tumalize reli halafu tuangalie kama uchumi wetu hauwezi kupaa zaidi.
 
Yaani leo magufuli anawasifu MABEBERU!! maajabu kweli sasa wanamdanganya Nani?
 
Back
Top Bottom